Si kwa kuwa wewe pia ni shetani hata hatushangai mkuu!Nikiambiwa nuchague kati ya Ndugai na Shetani. Nitakimbilia kwa Shetani
Si kwa kuwa wewe pia ni shetani hata hatushangai mkuu!Nikiambiwa nuchague kati ya Ndugai na Shetani. Nitakimbilia kwa Shetani
Kwa hiyo kama alikosea kipindi kile ndio afanye kosa hilohilo na kipindi hiki? Ninachokiona wengi humu mnaandika kwa mihemko bila kutafakari kwa kina juu ya issue hii.Pascal Mayalla
Wewe ni mwandishi nguli na pia ni Mwanasheria, ngoja nikuulize swali jepesi, unasema kuwa hao wabunge wamehukumiwa bila kusikilizwa, hivi wakati CCM ilipoleta taarifa ya kumfukuza uanachama wake Sofia Simba na pale Profesa Lipumba alipowavua uanachama wao wale wabunge wa viti maalum, mbona Spika Ndugai aliwatimua ubunge wao papo kwa papo na hapakuwa na hiyo hoja kuwa hao wabunge hawajasikilizwa??
Hivi hizi sheria zina "double standards" katika utekelezaji wake??
Eti huyu nae anajihita Mwandishi wa Habari za Uchunguzi"Msomi". Daaah!!! only in Tanzania...PatheticPascal Mayalla
Wewe ni mwandishi nguli na pia ni Mwanasheria, ngoja nikuulize swali jepesi, unasema kuwa hao wabunge wamehukumiwa bila kusikilizwa, hivi wakati CCM ilipoleta taarifa ya kumfukuza uanachama wake Sofia Simba na pale Profesa Lipumba alipowavua uanachama wao wale wabunge wa viti maalum, mbona Spika Ndugai aliwatimua ubunge wao papo kwa papo na hapakuwa na hiyo hoja kuwa hao wabunge hawajasikilizwa??
Hivi hizi sheria zina "double standards" katika utekelezaji wake??
Mkuu Paschal nimekusoma vizuri sana kwa ulichokiandika ingawa baadhi ya watu wenye uelewa mdogo wanakutukana.Hili suala la wabunge 19 wa Chadema, watu mnahamanika bure tuu. Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, common laws, ambao unafuata kanuni za natural justice. Kanuni ya kwanza inasema, everbody is presumed inocent until proven guilt, 2. no one is condemned unheard 3. The burden of proof, lies with the prosecution, the one who alleges, must prove.
Kwanini kina Halima wamehukumiwa bila kusikilizwa?. Kwa vile Spika kapelekewa majina na NEC, Chadema ndio the ones who alleges kuwa hao wabunge wame foji, and must prove, kuwa hawakuwateua, wala hawakuandika barua. Laiti mgejua Spika ana nini mkononi inayompa kiburi hivyo, CC ya Chadema isinge watimua, kwa pupa na kwa papara bila kwanza kujiridhisha majina hayo, yamefikishwa kwa Tume ya Uchaguzi kwa barua gani, iliyosainiwa na nani. Hapo ndipo kwenye mzizi wa fitna. Spika yeye kapelekewa majina tuu. Na sasa kikao cha BUK la Chadema, kitapindua maamuzi ya CC ya Chadema, mchezo utakuwa umekwisha.
Najua wengi humu, watatoa hoja kuwa wabunge hao waliitwa kupewa haki ya kusikilizwa, lakini sii wengi humu, wameisoma katiba ya Chadema na taratibu za kufuta wanachama, kwa faida ya wengi utaratibu ni huu.
Nawaomba sana Chadema, msishabikie maamuzi ya CC ya Chadema kukaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kuwatimua uanachama wanachama wake shupavu, walio ipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, mkumbuke kuna karma.
- Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?.
- Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?. Kina Halima walipewa hati za mashitaka?.
- Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia, jee hili lilifanyika?, nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, jee huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?.
- Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo kimaandishi ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, jee hili lilifanyika?. Mashitaka yanatolewa kwa maandishi na kujibiwa kwa maandishi, ndipo process ya kuitana na kusikilizwa shauri inafuata.
- Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba ya Chadema na kuwaalika watuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya haki ya kusikilizwa, kwa kujieleza na kujitetea. Kumsikiliza mtuhumiwa kabla ya kufikia maamuzi ya kumhukumu ni moja ya haki muhimu kabisa!. Jee kwenye huo uamuzi huo wa kuwatimua, kwa nini watimuliwe uanachama bila kusikilizaa. Jee sheria, taratibu na kanuni zilifuatwa?!.
Tukisubirie Kikao cha Baraza Kuu, kama kita endorse uamuzi huu wa a kangaroo court ya CC, kitakachofuata ni nyote kushuhudia, jinsi karma, itakavyo washughulikia watu.
Kwa msio jua karma, na inafanya nini kwa Chadema, someni hapa, angalieni chanzo kilichosababisha haya yatokee, nini kilikuja kuwakuta hao visababishi?.
![]()
Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
Wanabodi, Hili ni bandiko la wito kwa Chadema na ushauri wa bure, kiwatendee haki wanachama wake, ili ifikapo Octoba 2015, Watanzania waiaminie Chadema kuwa itawatendea haki Watanzania. Kitendo cha kutowatendea haki wanachama wake, kutapelekea wanachama hao kunyanyasika na kulia machozi ya ndani...www.jamiiforums.com
![]()
Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"
Wanabodi, Baada ya Kisa, Mkasa, na Baada ya Chanzo Kitendo!, Sakata la Mbunge Machachari wa Chadema, Zitto Zuberi Kabwe na chama chake cha Chadema limekuwa na visa na mikasa, vyanzo na vitendo na hatimaye leo, limefikia mwisho, limekwisha rasmi, it's over!, the rest is now a history...www.jamiiforums.com
Just wait and see.
P
Kwa hiyo wale watu waendelee kuwa bungeni bila uwakilishi au kivipi Mkuu?Mkuu Paschal nimekusoma vizuri sana kwa ulichokiandika ingawa baadhi ya watu wenye uelewa mdogo wanakutukana.
Katika ulichokiandika nipende kuongezea tu kwa CHADEMA ni kuwa hiki wanachokifanya wasifikiri wanakiimalisha chama nionavyo mimi wanajimaliza wenyewe huku wakijua au kutokujua kwani tumeshuhudia kila siku matamko yasiyo na kichwa wala miguu kutoka kwa viongozi wa BAWACHA kila eneo nchini huku wakiongea maneno yasiyo eleweka na mengine ya kudhalilisha viongozi na hii imenifanya niamini BAWACHA iliyokuwa ikiongozwa na H.MDEE ilikuwa na nguvu ya vitendo na hoja kuliko hawa tunaowana leo ambao ukiwasikiliza kwa makini utagundua mawazo na fikra zao zimejaa chuki na wivu juu ya hao akina Mdee.
Hivyo kwa ushauri wangu CHADEMA kama wanataka kujiimalisha waachane na hii issue ya akina MDEE wajikite kukiimalisha chama, kwani nionavyo mimi CDM imeporomoka sana na mwelekeo wake sio mzuri kama ilivyokuwa hapo zamani.
nimefikiri sana na kugundua kuwa huyu Spika ni mwepesi mno kutolewa kwenye kiti chake!!1) Wabunge wa CCM wapige kura ya kutokuwa na imani na spika. Wabunge wa kutosha wa aina ya Nape wakipatikaba Ndugai anaweza kutolewa na kutuachia katiba yetu.
Kama huyu wa bungeni atajibu lini wakati muda wowote ana mfuata mtu huko majuu?Chama kimetangaza kuwawafukuza watu uanachama, hivyo kwa mujibu wa Ibara 78(e) hawa sio wanachama na sio wabunge kwa sababu ibara hiyo ya 78 (e) imetabanaisha kuwa ili mtu awe mbunge ni lazima atokane na chama cha siasa! Sasa hawa wabunge 19 wanatokana na chama gani?. Si jambo jema kulewa madaraka halafu wakati huohuo mtu anajifurahisha kuwa ana uzoefu wa masuala ya kisheria.
Mama Sofia Simba (mama wa hekima) alifukuzwa na hakuna aliyemkingia kifua, Kachero mbobezi na mchuzi wa masuala ya kidiplomasia ya kimataifa alifukuzwa na hakuna aliyemkingia kifua(Bernard Member kamilius), wale wabunge 8 wa CUF walifukuzwa kwa haraka na sikuona hizi mbwembwe za sasa za natural justice. Ni katika bunge la miaka mitano iliyopita mbunge aliweza kufukuzwa na chana chake halafu baadae anarudisha sijui kwa mizania ipi! Nimalize kwa kusema haki ni tunda la amani and haki ikikosekana hakuna amani.
Ipo Siku ninyi mnaonajisi katiba ya JMT mlioapa kuilinda, kuitetea na kuhifadhi mtakuwa na cha kujibu mbele ya Mungu kama si kwa umma wa watanzania.
Huko kote umezunguka sana. Maneno mengiiii, point sifuri.Nianze kwa kumshukuru Nape Nnauye kwa kutoa hoja iliyomtoa nyoka pangoni. Kwa muda sasa Watanzania wamekuwa wakijiuliza ni lini spika atajitokeza na kutoa kauli juu ya wabunge hao 19 wasio na chama.
Alipojitokeza amekuja na hoja zilizoongeza mkanganyiko ambazo zinahitimisha kwa msimamo kuwa wabunge hao anawatambua na ni wabunge halali.
Hajasema ametumia kipengele gani cha katiba, kanuni au mwongozo unaompa mamlaka hayo. Kwa mtazamo wangu mimi Ndugai amevunja katiba na anatumia ubabe kuendelea kuvunja katiba.
Katiba ni mali ya watanzania wote na kila mmoja wetu ana wajibu wa kuilinda. Kwa muktadha huo mimi ningependekeza mojawapo ya mambo yafuatayo yafanyike;
1) Wabunge wa CCM wapige kura ya kutokuwa na imani na spika. Wabunge wa kutosha wa aina ya Nape wakipatikaba Ndugai anaweza kutolewa na kutuachia katiba yetu.
2) Mwenyekiti wa chama chake cha CCM mama Samia Suluhu Hassan aitishe kikao cha CC cha chama jumjadili na kumshinikiza Ndugai achukue hatua staiki. Aibu anayofanya Ndugai ni kwa chama chake pia
3) Ili kufifisha aibu ya kulazimika kubadili msimamo spika awaombe hao wabunge wake wajiuzulu ili tuanze ukurasa mpya. Utaratibu uanze kwa CHADEMA kufuata taratibu zote zinazohusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum.
4) Halima Mdee ni mwanasheria. Nakumbuka katika moja ya mijadala ya bunge lilopita Halima aliwahi kumtambia Prof. Kabudi kuwa yeye Halima ana Cheri cha uwakili. Nashauri aonyeshe umahiri wake wa sheria kwa kuheshimu katiba na kuamua kujiuzuru ili mchakato wa kikatiba na kisheria uchukue mkondo wake.
5) Spika wastaafu mama Anna Makinda na mzee Pius Msekwa mwiteni chemba kijana wenu huyu ambae mwenyewe anajigamba kupata uzoefu toka kwenu mwambieni anayoyatenda anakinajisi kiti cha spika aache na atekeleze matakwa ya kikatiba. Najua mzee Msekwa ukishalitolea ufafanuzi suala hili lakini ingefaa iwe ya mojakwamoja zaidi.
Nihitimishe kwa kutoa msisitizo kwamba mambo anayofanya Ndugai yanatuaibisha sisi sote kama taifa na kuonekana kuishi katika nchi ambamo viongozi wetu tumewaacha watuongoze kifalme bila kufuata taratibu za kikatiba.
Naomba kuwasilisha.
Huko kote umezunguka sana. Maneno mengiiii, point sifuri.Huko kote umezunguka sana. Maneno mengiiii, point sifuri.
Mambo matatu fanyeni nyie nyumbu.
1. Andikeni barua kwa kufuata utaratibu wa uandiabi na sio kuandika kipeperushi chenye mihemuko ndani yake.
2. Ambatisheni na katiba yenu mkieleza ni kifungu gani kimekiukwa kwa hao wabunhe kjwwmo bungeni buku mkiendelwa kula euzuku inayotokana na uwepo wao.
3. Ambatisheni na muhtasari wa kikao chenye maamuzi ya mwisho kuwafukuza mkionyesha akidi yake na jinsi mlivyojiridhisha kuwa wana hatia baada ya wao kujitetea katika kikao hicho.
Mbona simple tu?????
Uwakilishi upi unao uulizia? Wabunge waliopo Bungeni wanatuwakilisha sisi wananchi, wale wa kuchaguliwa kwenye majimbo wanawakilisha Majimbo yao na sisi wananchi na hao wengine wa Kuteuliwa na Viti Maalum wanatuwakilisha sisi wananchi tatizo lipo wapi?Kwa hiyo wale watu waendelee kuwa bungeni bila uwakilishi au kivipi Mkuu?
Shetani mwenzangu ameshatangulia ambaye mpaka kuzikwa ikawa siri.Si kwa kuwa wewe pia ni shetani hata hatushangai mkuu!
Sijidai kuwa naijua vizuri zaidi katiba ya Chadema, bali katiba ya Chadema ni public document na imeandikwa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, mtu yoyote anayejua kusoma na kuandika, anaweza kuisoma. Kitu cha ajabu kuhusu Katiba ya Chadema, kuna taratibu na kanuni za kufuta uanachama uliolekezwa na katiba ya Chadema, lakini katika timua timua zote, sijawahi kuona katiba ya Chadema ikifuatwa!. Jee Chadema wana tatizo gani na kufuata katiba yao?.Yaani wewe Paschal unaijua vizuri katiba ta CDM kuliko Mnyika? wakati mwingime Paschal huwa unalazimisha kutukanwa humu kwenye group
It's too lowSijidai kuwa naijua vizuri zaidi katiba ya Chadema, bali katiba ya Chadema ni public document na imeandikwa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, mtu yoyote anayejua kusoma na kuandika, anaweza kuisoma. Kitu cha ajabu kuhusu Katiba ya Chadema, kuna taratibu na kanuni za kufuta uanachama uliolekezwa na katiba ya Chadema, lakini katika timua timua zote, sijawahi kuona katiba ya Chadema ikifuatwa!. Jee Chadema wana tatizo gani na kufuata katiba yao?.
P
Soon Mwenyezi Mungu atatuondolea hiyo aibu, tuwe na subira tu.Nianze kwa kumshukuru Nape Nnauye kwa kutoa hoja iliyomtoa nyoka pangoni. Kwa muda sasa Watanzania wamekuwa wakijiuliza ni lini spika atajitokeza na kutoa kauli juu ya wabunge hao 19 wasio na chama.
Alipojitokeza amekuja na hoja zilizoongeza mkanganyiko ambazo zinahitimisha kwa msimamo kuwa wabunge hao anawatambua na ni wabunge halali.
Hajasema ametumia kipengele gani cha katiba, kanuni au mwongozo unaompa mamlaka hayo. Kwa mtazamo wangu mimi Ndugai amevunja katiba na anatumia ubabe kuendelea kuvunja katiba.
Katiba ni mali ya watanzania wote na kila mmoja wetu ana wajibu wa kuilinda. Kwa muktadha huo mimi ningependekeza mojawapo ya mambo yafuatayo yafanyike;
1) Wabunge wa CCM wapige kura ya kutokuwa na imani na spika. Wabunge wa kutosha wa aina ya Nape wakipatikaba Ndugai anaweza kutolewa na kutuachia katiba yetu.
2) Mwenyekiti wa chama chake cha CCM mama Samia Suluhu Hassan aitishe kikao cha CC cha chama jumjadili na kumshinikiza Ndugai achukue hatua staiki. Aibu anayofanya Ndugai ni kwa chama chake pia
3) Ili kufifisha aibu ya kulazimika kubadili msimamo spika awaombe hao wabunge wake wajiuzulu ili tuanze ukurasa mpya. Utaratibu uanze kwa CHADEMA kufuata taratibu zote zinazohusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum.
4) Halima Mdee ni mwanasheria. Nakumbuka katika moja ya mijadala ya bunge lilopita Halima aliwahi kumtambia Prof. Kabudi kuwa yeye Halima ana Cheri cha uwakili. Nashauri aonyeshe umahiri wake wa sheria kwa kuheshimu katiba na kuamua kujiuzuru ili mchakato wa kikatiba na kisheria uchukue mkondo wake.
5) Spika wastaafu mama Anna Makinda na mzee Pius Msekwa mwiteni chemba kijana wenu huyu ambae mwenyewe anajigamba kupata uzoefu toka kwenu mwambieni anayoyatenda anakinajisi kiti cha spika aache na atekeleze matakwa ya kikatiba. Najua mzee Msekwa ukishalitolea ufafanuzi suala hili lakini ingefaa iwe ya mojakwamoja zaidi.
Nihitimishe kwa kutoa msisitizo kwamba mambo anayofanya Ndugai yanatuaibisha sisi sote kama taifa na kuonekana kuishi katika nchi ambamo viongozi wetu tumewaacha watuongoze kifalme bila kufuata taratibu za kikatiba.
Naomba kuwasilisha.
Na akiondoka mwenyewe walewale jamaa zake CCM wanaanza kumnangaYaani ukoo wa panya wakamatane? Bado hatujafika huko. Kwa sasa wataendelea kumpigia makofi hadi atakapoondoka mwenyewe