Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Katiba ya Chadema inasemaPaskal bwana, Yaani pasua kichwa!! Unasema hawakusikilizwa Eti!! Hawa 19 walipewa nafasi ya kujitetea mbele ya CC ya Chadema, hawakuenda. Ulitaka CC iwabembeleze?? Haiwezekani!!
Halafu mtu ukihukumiwa kwa kosa fulani, ukakata rufaa, adhabu haibadiriki hadi hapo majibu ya rufaa yatakapotoka na hukumu tofauti.
Paskal, unataka kusema kwamba mtu aliyehukumiwa miezi 6 jela akakata rufaa, wakati akisubiri rufaa anatakiwa atoke gerezani?
We jamaa ni fala wa kiwango pitilizifu.Katiba ya Chadema inasema
P
- Watapewa hati ya mashitaka kwa maandishi- hili lilifanyika?.
- Hati hiyo itakuwa na tuhuma specific za makosa yao. Jee hili lilifanyika?.
- Watapewa siku 14 za kujibu tuhuma kwa maandishi. Jee hili lilifanyika?.
- Baada ya siku 14, ndipo kikao halali cha mamlaka yao ya nidhamu, kitaitishwa. Kwa nafasi ya wabunge, ni kweli mamlaka yao ya nidhamu ni CC. Jee hili lilifanyika?.
- Kikao hicho kwanza kitajadili utetezi wa majibu ya zile tuhuma kwa maandishi. Kama wameridhika, uamuzi wa hifanywa. Jee hili lilifanyika?.
- Kikao kisiporidhika na maelezo ya utetezi, ndipo huwaita watuhumiwa kwa barua rasmi za despatch, kuwahoji na kuwapa nafasi ya kusikilizwa.
- Baada ya kuwasikia, ndipo hukumu hutolewa, na kuwapa taarifa rasmi ya hukumu hiyo kwa maandishi na hupelekwa kwa despatch. Katika barua hizo, kama hawajaridhika na uamuzi huo wa CC hupewa haki ya kukata rufaa kikao cha juu, ambacho ni Baraza Kuu. Hili lolifanyika?.
- Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji enyeji. CC ya Chadema ilipomtimua Zitto, CC hiyo haikuwa na mamlaka ya kumtimua NKM, kwasababu, mamlaka ya nidhamu ya NKM ni Baraza Kuu na sio CC, sasa imekutana na wababe wake.
- Kuwatimua kama mbwa, bila kosa lolote, watu waliokipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, kutapelekea Chadema kupata laana ya karma.
- Kwa maoni yangu, Chadema hapo tuu ilipo, tayari ina hali mbaya kutokana na karma za mawazo, maneno na matendo yake maovu, nashauri, they shouldn't add an insult to an injury.
Huyu anajuta kupoteza muda wakati wa mwendazake....sasa anajaribu bahati yake tena kwa mama....ila kuhusu spika ngoja tumsikilizie Mungu afanye yake tena kama kwa mwendazakeUmmemjibu vema mchumia tumbo Pascal,
Pascal anatakiwa awalaumu wajumbe waliomkata kwenye kura za maoni,
Baada ya kuondoka mwenda zake,anafikili anaweza kupata nafasi kwa mwenyekiti mpya,
Lakini Pascal anaahindwa kutambua kuwa Kila zama na kitabu chake.
Tanzania hii hii au Kenya?Ndugai apigiwe kura na wabunge yakutokuwa na imani.amevunja katiba ya nchi.
Lakini Paschal, si huwa nasikia una kaufahamu kidogo ka sheria? Spika from day one "aliamini" barua ile ilitoka Chadema. Baadaye aliambiwa kwa barua kwamba hao watu ulio nao hapo bungeni, chama hakijawateua.Forgery ni kosa la jinai. Kama Chedema haikupeleka majina NEC, maana yake kuna mtu amefoji hiyo barua na kuipeleka NEC, hivyo Spika yeye ameletewa majina from NEC. Swali ni kwanini mpaka sasa, Chadema hawajaripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike, Polisi wataomba nakala ya hiyo barua, na kufanyiwa forensic investigations kama ni kweli hizi saini kwenye barua hizo, zimefojiwa, zikikutwa ni sahihi za halali, then ni barua halali!. Huwezi leo kuwatea wabunge kwa halali, barua halali, halafu kesho wewe wewe ukawatimua, na kupeleka barua nyingine kuwa huwatambui na huitambui ile barua ya awali iliyowateua. The burden of proof lies with Chadema to prove jinai ya forgery.
Kwanini Chadema, kazi yao kubwa ni kupiga tuu kelele, badala ya kuchukua hatua, and do the right thing?!.
P
Pale Ubungo Meya alifukuzwa kwa barua ya kuokota na DED hakusubiri ku-prove chochote, Paschal ni msaka tonge achana nayeLakini Paschal, si huwa nasikia una kaufahamu kidogo ka sheria? Spika from day one "aliamini" barua ile ilitoka Chadema. Baadaye aliambiwa kwa barua kwamba hao watu ulio nao hapo bungeni, chama hakijawateua.
Ambacho Supika alitakiwa kufanya ni kuwarudisha kwenye chama chao wanachodai kiliwateua, kwa maelezo kwamba chama chenu kimekana kuwateua, na from there spika anakuwa amenawa. Ngoma inabaki kati ya NEC na CDM, mchezo unaishia hapo, kwanini spika analazimisha kuitambua barua toka tume, na anashindwa kuamini barua toka CDM??
Paschal, acha kujitoa ufahamu, teuzi zenyewe naona kama zimeisha zinazokufaa, na sidhani kama mama anashawishiwa kwa mtindo huo.
Kalaga Baho!!!
Paschal usimwamini tena achana naye akili yake iliishia 2017 kurudi nyumaPana mambo unayaruka mkuu:
1. Chadema hawakuwasilisha majina ya watakaokuwa wabunge wao wa viti maalumu kama utaratibu rasmi unaoafahamika unavyotakikana.
2. Si kuwa wamehukumiwa bila kusikilizwa bali kwa uamuzi wao wenyewe, hawakutokea kusikilizwa pamoja na kuwa walikuwa wamepewa wito rasmi wa kuhudhuria ili kusikilizwa.
Mkuu wangesikilizwa vipi bila wao kutokea kunako uliko wito?
Kama kutotokea kwenye wito ni halali unadhani nini kingewafanya watokee ili kusikilizwa kama kwao hiyo itakuwa ni kinga ya kudumu kuhalalisha kwao kutokusikilizwa?
Wenyewe 19 wanajua kuwa Chadema wametimuliwa isipokuwa Supika, Naibu supika na baadhi ya ma CCM!
Wajameni inaingia akilini kweri?
Wewe ndiyo unaijua katiba ya CHADEMA kuliko Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake? ndiyo maana siku hizi jamii inakudharau sn, heshima ambayo uliijenga kwa miaka mingi umekuja kuibomoa kwa dak 2 tu.Hili suala la wabunge 19 wa Chadema, watu mnahamanika bure tuu. Tanzania tunafuata mfumo wa sheria wa Uingereza, common laws, ambao unafuata kanuni za natural justice. Kanuni ya kwanza inasema, everbody is presumed inocent until proven guilt, 2. no one is condemned unheard 3. The burden of proof, lies with the prosecution, the one who alleges, must prove.
Kwanini kina Halima wamehukumiwa bila kusikilizwa?. Kwa vile Spika kapelekewa majina na NEC, Chadema ndio the ones who alleges kuwa hao wabunge wame foji, and must prove, kuwa hawakuwateua, wala hawakuandika barua. Laiti mgejua Spika ana nini mkononi inayompa kiburi hivyo, CC ya Chadema isinge watimua, kwa pupa na kwa papara bila kwanza kujiridhisha majina hayo, yamefikishwa kwa Tume ya Uchaguzi kwa barua gani, iliyosainiwa na nani. Hapo ndipo kwenye mzizi wa fitna. Spika yeye kapelekewa majina tuu. Na sasa kikao cha BUK la Chadema, kitapindua maamuzi ya CC ya Chadema, mchezo utakuwa umekwisha.
Najua wengi humu, watatoa hoja kuwa wabunge hao waliitwa kupewa haki ya kusikilizwa, lakini sii wengi humu, wameisoma katiba ya Chadema na taratibu za kufuta wanachama, kwa faida ya wengi utaratibu ni huu.
Nawaomba sana Chadema, msishabikie maamuzi ya CC ya Chadema kukaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kuwatimua uanachama wanachama wake shupavu, walio ipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, mkumbuke kuna karma.
- Kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA, ili kumvua mtu uanachama kuna mlolongo wa kanuni na taratibu za kufuatwa na miongoni mwake ni hizi nitakazo ziorodhesha hapa chini, jee zilifuatwa?.
- Kuandaa Hati ya Mashtaka kwa maandishi yenye tuhuma zote ambazo mtuhumiwa anakabiliwa nazo. Jee hati hizi za mashitaka kimaandishi ziliandaliwa?. Kina Halima walipewa hati za mashitaka?.
- Hati hiyo ya mashitaki kimaandishi inatakiwa ikabidhiwa kwa mtuhumiwa kwa "despatch" ili kuthibitisha imemfikia, jee hili lilifanyika?, nimesikia kuna watu waliitwa kwa simu, jee huu ndio utaratibu kwa jambo zito kama hili?.
- Mtuhumiwa atatakiwa kuzijibu tuhuma za mashitaka hayo kimaandishi ndani ya kipindi cha siku 14 tangu tarehe aliyopokea barua ile ili apate muda wa kutosha kutafakari, jee hili lilifanyika?. Mashitaka yanatolewa kwa maandishi na kujibiwa kwa maandishi, ndipo process ya kuitana na kusikilizwa shauri inafuata.
- Baada ya majibu ya hati ile ya mashitaka kurejeshwa, ndipo mamlaka ya nidhamu ingepaswa kuitisha kikao rasmi kwa mujibu wa katiba ya Chadema na kuwaalika watuhumiwa kwa barua ili kuwapa nafasi ya haki ya kusikilizwa, kwa kujieleza na kujitetea. Kumsikiliza mtuhumiwa kabla ya kufikia maamuzi ya kumhukumu ni moja ya haki muhimu kabisa!. Jee kwenye huo uamuzi huo wa kuwatimua, kwa nini watimuliwe uanachama bila kusikilizaa. Jee sheria, taratibu na kanuni zilifuatwa?!.
Tukisubirie Kikao cha Baraza Kuu, kama kita endorse uamuzi huu wa a kangaroo court ya CC, kitakachofuata ni nyote kushuhudia, jinsi karma, itakavyo washughulikia watu.
Kwa msio jua karma, na inafanya nini kwa Chadema, someni hapa, angalieni chanzo kilichosababisha haya yatokee, nini kilikuja kuwakuta hao visababishi?.
Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
Wanabodi, Hili ni bandiko la wito kwa Chadema na ushauri wa bure, kiwatendee haki wanachama wake, ili ifikapo Octoba 2015, Watanzania waiaminie Chadema kuwa itawatendea haki Watanzania. Kitendo cha kutowatendea haki wanachama wake, kutapelekea wanachama hao kunyanyasika na kulia machozi ya ndani...www.jamiiforums.com Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau, Jiandaeni kwa "Karma!"
Wanabodi, Baada ya Kisa, Mkasa, na Baada ya Chanzo Kitendo!, Sakata la Mbunge Machachari wa Chadema, Zitto Zuberi Kabwe na chama chake cha Chadema limekuwa na visa na mikasa, vyanzo na vitendo na hatimaye leo, limefikia mwisho, limekwisha rasmi, it's over!, the rest is now a history...www.jamiiforums.com
Just wait and see.
P
Yaani wewe Paschal unaijua vizuri katiba ta CDM kuliko Mnyika? wakati mwingime Paschal huwa unalazimisha kutukanwa humu kwenye groupKatiba ya Chadema inasema
P
- Watapewa hati ya mashitaka kwa maandishi- hili lilifanyika?.
- Hati hiyo itakuwa na tuhuma specific za makosa yao. Jee hili lilifanyika?.
- Watapewa siku 14 za kujibu tuhuma kwa maandishi. Jee hili lilifanyika?.
- Baada ya siku 14, ndipo kikao halali cha mamlaka yao ya nidhamu, kitaitishwa. Kwa nafasi ya wabunge, ni kweli mamlaka yao ya nidhamu ni CC. Jee hili lilifanyika?.
- Kikao hicho kwanza kitajadili utetezi wa majibu ya zile tuhuma kwa maandishi. Kama wameridhika, uamuzi wa hifanywa. Jee hili lilifanyika?.
- Kikao kisiporidhika na maelezo ya utetezi, ndipo huwaita watuhumiwa kwa barua rasmi za despatch, kuwahoji na kuwapa nafasi ya kusikilizwa.
- Baada ya kuwasikia, ndipo hukumu hutolewa, na kuwapa taarifa rasmi ya hukumu hiyo kwa maandishi na hupelekwa kwa despatch. Katika barua hizo, kama hawajaridhika na uamuzi huo wa CC hupewa haki ya kukata rufaa kikao cha juu, ambacho ni Baraza Kuu. Hili lolifanyika?.
- Chadema ilizoea kufanya mambo kienyeji enyeji. CC ya Chadema ilipomtimua Zitto, CC hiyo haikuwa na mamlaka ya kumtimua NKM, kwasababu, mamlaka ya nidhamu ya NKM ni Baraza Kuu na sio CC, sasa imekutana na wababe wake.
- Kuwatimua kama mbwa, bila kosa lolote, watu waliokipigania Chadema kwa machozi, jasho na damu, kutapelekea Chadema kupata laana ya karma.
- Kwa maoni yangu, Chadema hapo tuu ilipo, tayari ina hali mbaya kutokana na karma za mawazo, maneno na matendo yake maovu, nashauri, they shouldn't add an insult to an injury.
Jibu hoja zake acha kuchangia kimbumbumbu mkuu!!Mungu anisaidie, nisizeeke vibaya kama Pascal Mayala. Kama moja ya athari ya uzee ni kuwa hivi, hakika uzee unatisha.
Jibu hoja kama kanuni hizo alizozitaja Mayalla hazipo?Wewe ndiyo unaijua katiba ya CHADEMA kuliko Mwenyekiti na Katibu Mkuu wake? ndiyo maana siku hizi jamii inakudharau sn, heshima ambayo uliijenga kwa miaka mingi umekuja kuibomoa kwa dak 2 tu.
Kwani Mnyika ni Mungu wako au?Yaani wewe Paschal unaijua vizuri katiba ta CDM kuliko Mnyika? wakati mwingime Paschal huwa unalazimisha kutukanwa humu kwenye group
Mungu anahusishwa na matatizo ya chadema sana siku hizi.Au Ndugai aachiwe Mungu kama ilivyofanyika kwa mbabe flani
Nianze kwa kumshukuru Nape Nnauye kwa kutoa hoja iliyomtoa nyoka pangoni. Kwa muda sasa Watanzania wamekuwa wakijiuliza ni lini spika atajitokeza na kutoa kauli juu ya wabunge hao 19 wasio na chama.
Alipojitokeza amekuja na hoja zilizoongeza mkanganyiko ambazo zinahitimisha kwa msimamo kuwa wabunge hao anawatambua na ni wabunge halali.
Hajasema ametumia kipengele gani cha katiba, kanuni au mwongozo unaompa mamlaka hayo. Kwa mtazamo wangu mimi Ndugai amevunja katiba na anatumia ubabe kuendelea kuvunja katiba.
Katiba ni mali ya watanzania wote na kila mmoja wetu ana wajibu wa kuilinda. Kwa muktadha huo mimi ningependekeza mojawapo ya mambo yafuatayo yafanyike;
1) Wabunge wa CCM wapige kura ya kutokuwa na imani na spika. Wabunge wa kutosha wa aina ya Nape wakipatikaba Ndugai anaweza kutolewa na kutuachia katiba yetu.
2) Mwenyekiti wa chama chake cha CCM mama Samia Suluhu Hassan aitishe kikao cha CC cha chama jumjadili na kumshinikiza Ndugai achukue hatua staiki. Aibu anayofanya Ndugai ni kwa chama chake pia
3) Ili kufifisha aibu ya kulazimika kubadili msimamo spika awaombe hao wabunge wake wajiuzulu ili tuanze ukurasa mpya. Utaratibu uanze kwa CHADEMA kufuata taratibu zote zinazohusu uteuzi wa wabunge wa viti maalum.
4) Halima Mdee ni mwanasheria. Nakumbuka katika moja ya mijadala ya bunge lilopita Halima aliwahi kumtambia Prof. Kabudi kuwa yeye Halima ana Cheri cha uwakili. Nashauri aonyeshe umahiri wake wa sheria kwa kuheshimu katiba na kuamua kujiuzuru ili mchakato wa kikatiba na kisheria uchukue mkondo wake.
5) Spika wastaafu mama Anna Makinda na mzee Pius Msekwa mwiteni chemba kijana wenu huyu ambae mwenyewe anajigamba kupata uzoefu toka kwenu mwambieni anayoyatenda anakinajisi kiti cha spika aache na atekeleze matakwa ya kikatiba. Najua mzee Msekwa ukishalitolea ufafanuzi suala hili lakini ingefaa iwe ya mojakwamoja zaidi.
Nihitimishe kwa kutoa msisitizo kwamba mambo anayofanya Ndugai yanatuaibisha sisi sote kama taifa na kuonekana kuishi katika nchi ambamo viongozi wetu tumewaacha watuongoze kifalme bila kufuata taratibu za kikatiba.
Naomba kuwasilisha.
Mbabe alichomolewa faster na hila zake mbaya za kutaka kutawala milele.Au Ndugai aachiwe Mungu kama ilivyofanyika kwa mbabe flani