Tuondoe aibu hii anayosababisha Spika Ndugai

Kwa hiyo kama alikosea kipindi kile ndio afanye kosa hilohilo na kipindi hiki? Ninachokiona wengi humu mnaandika kwa mihemko bila kutafakari kwa kina juu ya issue hii.
 
Eti huyu nae anajihita Mwandishi wa Habari za Uchunguzi"Msomi". Daaah!!! only in Tanzania...Pathetic
 
Mkuu Paschal nimekusoma vizuri sana kwa ulichokiandika ingawa baadhi ya watu wenye uelewa mdogo wanakutukana.
Katika ulichokiandika nipende kuongezea tu kwa CHADEMA ni kuwa hiki wanachokifanya wasifikiri wanakiimalisha chama nionavyo mimi wanajimaliza wenyewe huku wakijua au kutokujua kwani tumeshuhudia kila siku matamko yasiyo na kichwa wala miguu kutoka kwa viongozi wa BAWACHA kila eneo nchini huku wakiongea maneno yasiyo eleweka na mengine ya kudhalilisha viongozi na hii imenifanya niamini BAWACHA iliyokuwa ikiongozwa na H.MDEE ilikuwa na nguvu ya vitendo na hoja kuliko hawa tunaowana leo ambao ukiwasikiliza kwa makini utagundua mawazo na fikra zao zimejaa chuki na wivu juu ya hao akina Mdee.
Hivyo kwa ushauri wangu CHADEMA kama wanataka kujiimalisha waachane na hii issue ya akina MDEE wajikite kukiimalisha chama, kwani nionavyo mimi CDM imeporomoka sana na mwelekeo wake sio mzuri kama ilivyokuwa hapo zamani.
 
Chama kimetangaza kuwawafukuza watu uanachama, hivyo kwa mujibu wa Ibara 78(e) hawa sio wanachama na sio wabunge kwa sababu ibara hiyo ya 78 (e) imetabanaisha kuwa ili mtu awe mbunge ni lazima atokane na chama cha siasa! Sasa hawa wabunge 19 wanatokana na chama gani?. Si jambo jema kulewa madaraka halafu wakati huohuo mtu anajifurahisha kuwa ana uzoefu wa masuala ya kisheria.

Mama Sofia Simba (mama wa hekima) alifukuzwa na hakuna aliyemkingia kifua, Kachero mbobezi na mchuzi wa masuala ya kidiplomasia ya kimataifa alifukuzwa na hakuna aliyemkingia kifua(Bernard Member kamilius), wale wabunge 8 wa CUF walifukuzwa kwa haraka na sikuona hizi mbwembwe za sasa za natural justice. Ni katika bunge la miaka mitano iliyopita mbunge aliweza kufukuzwa na chana chake halafu baadae anarudisha sijui kwa mizania ipi! Nimalize kwa kusema haki ni tunda la amani and haki ikikosekana hakuna amani.

Ipo Siku ninyi mnaonajisi katiba ya JMT mlioapa kuilinda, kuitetea na kuhifadhi mtakuwa na cha kujibu mbele ya Mungu kama si kwa umma wa watanzania.
 
Kwa hiyo wale watu waendelee kuwa bungeni bila uwakilishi au kivipi Mkuu?
 
1) Wabunge wa CCM wapige kura ya kutokuwa na imani na spika. Wabunge wa kutosha wa aina ya Nape wakipatikaba Ndugai anaweza kutolewa na kutuachia katiba yetu.
nimefikiri sana na kugundua kuwa huyu Spika ni mwepesi mno kutolewa kwenye kiti chake!!
 
Kama huyu wa bungeni atajibu lini wakati muda wowote ana mfuata mtu huko majuu?
 
Huko kote umezunguka sana. Maneno mengiiii, point sifuri.
Mambo matatu fanyeni nyie nyumbu.
1. Andikeni barua kwa kufuata utaratibu wa uandiabi na sio kuandika kipeperushi chenye mihemuko ndani yake.
2. Ambatisheni na katiba yenu mkieleza ni kifungu gani kimekiukwa kwa hao wabunhe kjwwmo bungeni buku mkiendelwa kula euzuku inayotokana na uwepo wao.
3. Ambatisheni na muhtasari wa kikao chenye maamuzi ya mwisho kuwafukuza mkionyesha akidi yake na jinsi mlivyojiridhisha kuwa wana hatia baada ya wao kujitetea katika kikao hicho.

Mbona simple tu?????
 
Huko kote umezunguka sana. Maneno mengiiii, point sifuri.
Mambo matatu fanyeni nyie nyumbu.
1. Andikeni barua kwa kufuata utaratibu wa uandishi na sio kuandika kipeperushi chenye mihemuko ndani yake.
2. Ambatisheni na katiba yenu mkieleza ni kifungu gani kimekiukwa kwa hao wabunge kuwamo bungeni huku mkiendelea kula ruzuku inayotokana na uwepo wao.
3. Ambatisheni na muhtasari wa kikao chenye maamuzi ya mwisho kuwafukuza mkionyesha akidi yake na jinsi mlivyojiridhisha kuwa wana hatia baada ya wao kujitetea katika kikao hicho.

Mbona simple tu?????
 
Huyu dawa yake ni mungu tu ,tumeshamchoka kwelikweli ,mungu mwema atajibu maombi
 
Kwa hiyo wale watu waendelee kuwa bungeni bila uwakilishi au kivipi Mkuu?
Uwakilishi upi unao uulizia? Wabunge waliopo Bungeni wanatuwakilisha sisi wananchi, wale wa kuchaguliwa kwenye majimbo wanawakilisha Majimbo yao na sisi wananchi na hao wengine wa Kuteuliwa na Viti Maalum wanatuwakilisha sisi wananchi tatizo lipo wapi?
 
Yaani wewe Paschal unaijua vizuri katiba ta CDM kuliko Mnyika? wakati mwingime Paschal huwa unalazimisha kutukanwa humu kwenye group
Sijidai kuwa naijua vizuri zaidi katiba ya Chadema, bali katiba ya Chadema ni public document na imeandikwa kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili, mtu yoyote anayejua kusoma na kuandika, anaweza kuisoma. Kitu cha ajabu kuhusu Katiba ya Chadema, kuna taratibu na kanuni za kufuta uanachama uliolekezwa na katiba ya Chadema, lakini katika timua timua zote, sijawahi kuona katiba ya Chadema ikifuatwa!. Jee Chadema wana tatizo gani na kufuata katiba yao?.

P
 
It's too low
 
Soon ata
Soon Mwenyezi Mungu atatuondolea hiyo aibu, tuwe na subira tu.
 
Tumwombwe Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atelekeleze ile "modus operandi" yake kama alivyotekeleza kwa Mwendazake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…