Kwa udongo wa aina gani? Yeyote anayekwambia kiasi cha ekari kwa masaa bila kutaja aina ya udongo, hawezi kuwa sahihi. Mi nina uzoefu wa udongo wa mfinyanzi mweusi na kichanga.
Kwa udongo wa mfinyanzi mweusi unaopasuka kiangazi, hakuna trekta ya kulima ekari 30 hata kwa masaa 24 kwa shamba jipya na trekta isiwe chini ya hp 75. Tena mtu asikudanganye trekta za farmtrack wala swalaji.
Kwa udongo wa kichanga peleka hizo farm track na swalaji hata hp. 45 inalima.
Hivyo, jiridhishe kwanza na aina ya udongo.
Kwa wanaolinganisha massey used na farm track, mmmmmhhh!!!!
Car junction pale ubungo plaza, massey used huwezi pata chini ya 45ml. Mpya unazikuta hapo hapo na waweza pata hata chini ya 40, nilishafika pale nina uhakika na nisemayo.
All in all huwezi linganisha massey Used za Uk na new holland, labda kama ni massey za pakistan.
Nimeona mwingine amelinganisha ford 6610 na farm track hp.75 mmmmmmhhh. Hakuna kitu kama hiyo, huyo hiyo ford huwa anaisikia tu, hiyo ford hata kama aliingiza nchini used akaitumia kwa miaka 10, akitaka kuiuza hata muda huu kwa wanaozifahamu bei yake hata haiwezi lingana na farm track iliyokuja mpya na imetumika miaka 3.
Kwa fuel consumption nakubali tractor mpya zinatumia kidogo sana, lakini sio kwa uimara na work load. Bahati nzuri ninalima na wenye hizo tractor mpya, swaraji, farm track na tafe,
Uliza popote massey 375 used za uk yard zote uone jinsi ambavyo bei yake Iko juu sawa na kununua farm track mpya na accessories zake zote, kwa akili yako unadhani wauzaji na wanunuzi hawana akili?