Tuongee kuhusu madhara ya kumchoma mtoto wa kiume ganzi kwenye uume wakati wa kumtahiri

Tuongee kuhusu madhara ya kumchoma mtoto wa kiume ganzi kwenye uume wakati wa kumtahiri

Kumtahili mtoto kwa kumchoma ganzi kwenye kiuume chake , ni ukatili fulani hivi.

Mpe dawa ya usingizi, alale akiamka , anakuta kwisha habari.
Hii si inafanyika hospitali na hospital ama ni hospital zote wanafanya hivyo? Nilitaka kufanya hivyo lakini ni kuogopa mtoto anaweza kupitiliza
 
Aiseee!! Kuuliza sio ujinga lakini. Humu Kuna watu wanahizo taaluma. Sidhani kama ni busara kumshambulia mtu aliyehitaji msaada wa ushauri.
🙏🙏🙏🙏
 
Namna hiyoooo, sio kwa mkasi wala wembe wa dk leakey!
Ilikuwa ni kwa kisu kilichonolewa na jiwe la babu!
Du aisee so ilikuwa ukisha katwa unapakwa dawa au utajijua Mwenyewe?
 
Kizazi suna ganzi tabu kweli, yaan kiukweli nashangaa sana kuskia mtoto anatahiriwa kwa kutumia ganzi! Nimepata tohara bila ganzi, mtoto wangu pia kapata tohara bila ganzi, nadhani ni vyema zaidi aanze kufeel uanaume wake tangu enzi za tohara. Kwa kawaida namuacha mtoto afike miaka 6 hadi 7 ndo apate tohara, kuna kaheshima fulani kanajengeka akisikia maana kuwa mwanaume huanzia katika machungu ya tohara
Wewe ni baba mkatili kwa watoto. Dah yani unampeleka mtoto wako atahiriwe bila ganzi? Duh 🙌🙌🙌
 
Haina madhara.

Watumie dawa walizoandikiwa na daktari aliyewatahiri.

Kila la kheri.
Asante sana mkuu.

Nakesha silali nawaangalia wasije jitonesha.

Asubuhi ndo nalala wakisha amka
 
Kumtahili mtoto kwa kumchoma ganzi kwenye kiuume chake , ni ukatili fulani hivi.

Mpe dawa ya usingizi, alale akiamka , anakuta kwisha habari.
KItendo tu cha kumtahiri mtoto ni ukatili kwa 100%.
Kwanini umkate mtoto kiungo chake alichozaliwa nacho, tena unafanya hivyo bila ridhaa yake?

Tohara kwa mtoto ni ukatili mkubwa.
 
KItendo tu cha kumtahiri mtoto ni ukatili kwa 100%.
Kwanini umkate mtoto kiungo chake alichozaliwa nacho, tena unafanya hivyo bila ridhaa yake?

Tohara kwa mtoto ni ukatili mkubwa.
Duh ! But u make sense
 
Hii si inafanyika hospitali na hospital ama ni hospital zote wanafanya hivyo? Nilitaka kufanya hivyo lakini ni kuogopa mtoto anaweza kupitiliza
Kupitiliza kwenda wapi? Yaan kukata govi apewe nusu kaput? Huyo Dr atakayefanya hivyo labda atakuwa amesomea agricultural engineering 😀 na nani alisema mtu akipewa dawa ya usingizi anapitiliza? Makosa ya kiufundi huwa yapo juu ya hizo dawa ila ni mara chache.
Kuhusu bila ganzi wakurya wanatahiri bila ganzi tena kwa kisu alichonunua sokoni na hawana shida
 
Lakini naona kama yafaa uzingatie ya wataalamu wa hapo ulipomfanyia tohara mwanao......mbona kama unaonekana kama huwaamini wataalamu uliowachagua kumfanyia mwanao kazi hiyo..??
 
KItendo tu cha kumtahiri mtoto ni ukatili kwa 100%.
Kwanini umkate mtoto kiungo chake alichozaliwa nacho, tena unafanya hivyo bila ridhaa yake?

Tohara kwa mtoto ni ukatili mkubwa.
Wewe umetahiriwa ? Unajua madhara ya kutokutahiriwa?
 
Yaani wanawake ni shida sana.

Kama unaonea huruma sana hao watoto wako wa kiume wanapo chomwa sindano ya ganzi basi wapeleke kule Tarime. Wakurya wanatahiri watoto wao wa kiume bila ganzi tena kwa kisu, kazi kwako.
 
Maumivu ya kutahiriwa ukiwa mkubwa yasikie kwa jirani tuu,nilijuta dudu inasimama usiku kucha make ni kunipepelea kwa kitenge laaa acha tuu
 
Back
Top Bottom