SankaraBoukaka
JF-Expert Member
- Jul 2, 2019
- 1,213
- 1,918
Wengi wenu hamjui yeye ni nani lakini yeye ni muhimu. Latasha Harlins. Mnamo 1991, akiwa na umri wa miaka 15, alienda kwenye soko lake la chakula linalomilikiwa na Wakorea na hakufanikiwa kutoka kurudi kwao akiwa mzima. Mke wa mwenye duka, Soon Ja Du, alidhani Latasha kaja kuiba chupa ya juisi ya machungwa na mkwaruzano kati yao ukatokea.
Du alimshika Latasha na kuishia kusukumwa chini. Du kisha akaenda kuchukua bunduki yake na kumuelekezea Latasha. Latasha aliinama, akachukua juisi ya machungwa, na kuiweka kwenye counter. Latasha aliwa anaondoka dukani, Du alimpiga risasi nyuma ya kichwa kwa umbali wa futi 3, na kumuua mara moja. Du alijaribu kudai kujitetea, lakini kulikuwa na watu 2 walioshuhudia na kamera ya usalama ya duka ilionyesha vinginevyo.
Mahakama ilimtia hatiani Du na kumshauri hakimu ampe kifungo cha juu cha miaka 16. Du aliishia kuhukumiwa saa 400 za huduma ya jamii, na kuwa chini ya Uangalizi kwa miaka 5, na faini ya $500, pia jaji alisema ingawa Bi. D alitenda isivyofaa, matendo yake yalikuwa ya haki. Jaji Joyce Karlin anasema kuwa Bi. Du alikuwa mwathirika, Latasha ndiye mhalifu na angekuwa amesimama mbele yake kwa kumpiga karani wa duka kama hangekufa. Kuuawa kwa Latasha Harlins ni moja ya sababu kuu za kuanzishwa kwa Machafuko ya LA.
Tunasikia tu kuhusu Rodney King lakini yeye ndiye #SayHerName asili. Tupac aliumizwa sana na hiki kifo cha Latasha na ametaja jina lake katika nyimbo kadhaa na pia aliweka wakfu wimbo wa "Keep Ya Head Up" kwa Latasha. Kwa hivyo tunasema Latasha Harlins, huko uliko tambua kuwa dunia inakukumbuka, na leo, kuna mtu ameisikia hadithi yako ❤️