Tupac na Biggie wanakuzwa mno

Tupac na Biggie wanakuzwa mno

Waliopata mafanikio zaidi hata ya Tupac kwa muda mfupi kuna Lil wayne, Eminem na hawa wangekufa ingukua zaidi ya story. Mimi sikatai kama jamaa alikua juu ila kifo chake kime mwongezea nyota sio siri kama huyu jamaa ya juzi Nipsey Hussle wengi hata hawaelewi alifanya nini kwenye game ila ndo ka boom ghafla.
Unaongelea mafanikio ya kifedha.... Mtaje mwenye album platinum 9 ..kati yao hao unaowapenda unaoona wanastahili tena akiwa 25 yrs tu .
 
Jiggah mwenyewe anakuambia yeye kwasasa ndo King kwasababu Biggie is no more. Means anatambua Biggie was a King.
Jay z ,Diddy, walikuw na bifu pia na pack,inasemekana nao kama walihusika ktk assassin's ya pack kiasi flani.coz Jay z alikuw secret society na pack alikuw akiwasumbua kwenye game.wakamtengenezea zengwe na big kisha waka m fire.
 
Kulikuwa hakuna mitandao ya kijamii ila Pac alijulikana hadi na watoto, sasa vijana akiyoa ka single hata kama ujaamka umeshasikia

2pac na Big ni wafalme wa hip hop
 
Kwanza hicho kipande cha DEAR MAMA,aiseee
Pac alikuwa mtu hatari!! Acha awe king tu wa hip hop heshima inamfaa, mie naona yeye ndio kama alibadilisha game kutoka ile style ya kurap ambayo dunia nzima ilikuwa inatumia mpaka ikawa kila mtu anarap anavyojisikia!! Ndani ya umri mdogo alifanya mambo makubwa katika game ya hip hop!!

Mziki kama mziki ninavyotafsiri mimi mziki ili uwe mzuri aidha uwe unasikilizika(kuburudisha) ama uwe unafunza(maneno fulani kuntu) au uwe na vyote.

1. Kusikilizika music, namaanisha uwe mtamu masikioni, hapa hata km mtu haelewi mashairi, haelewi kilichoimbwa, lakini uwe mziki mtamu masikioni utapendwa, kina psy na gungnam style, sijui usiniseme kama napenda kula kina ali kiba, sijui despacito, unakuta mtu hajui kilchoimbwa au mashairi hayana kitu ila kwakuwa ni mtamu masikioni mwake unakuwa mziki mzuri

2.kufundisha, sijui nitumie neno kufundisha ama nisemeje sijui hapa nazungumzia mashairi kuwa mazuri, yaani mtu anaupenda muziki kwa mashairi na sio kusikilizika masikioni,hapa inalenga wanaoelewa mashairi, unamkuta mtu anapenda nyimbo fulani we unaweza kuita wa kawaida kumbe ni mtu anasikiliza message ya mule!

Hip hop kama hip hop imebase kwenye mziki mzuri wa aina ya pili, wasikilize kina fid q, sijui jigga, eminem, kendrick na wengineo utanielewa hapa, hata kama mziki sio mtamu masikioni ila mashairi yake tu yanamfanya mtu akakipenda kitu..

Turud kwa tupac, pac alikuwa na mziki mzuri kwa kusikilizika hata kama huelew kinachoimbwa na mashairi mazuri kwa pamoja
Sikiliza
Dear mama
I aint mad at cha
Untill the end of time
Keap ya head up
So many tears
Change
Me n my girlfriend

Nakadhalika nakadhalika.

Binafsi namuelewa mno pac anahitaji heshima yake, naamin jamaa alikufa akiwa bado hajafikia kilele chake, ndio kwnza alikuwa anasogea kwenye peak yake sijui angeipata peak yake ingekuwaje, now angekuwa na heshima zaidi, sijui kama asingekuwa mwanamuziki milionea pia, tizama toka alipoanza mpaka kifo chake jamaa alikuwa kwenye graph yake ndio kwanza anapanda.
 
Jay z ,Diddy, walikuw na bifu pia na pack,inasemekana nao kama walihusika ktk assassin's ya pack kiasi flani.coz Jay z alikuw secret society na pack alikuw akiwasumbua kwenye game.wakamtengenezea zengwe na big kisha waka m fire.
bado hii sio justification.
pia hayo mastory ya kifo cha biggie na 2pac kila mtu ana theory yake anayopenda kuamini.
 
Du,kwa hiyo jamaa anaish hapa bongo
Tupac na Notorious BIG walikuwa violent kweli, makundi yao yalikuwa ya kihuni Sanaa

Lakini hakuna muhuni kabla yao kama EAZY E then ndio kina DRE na 2PAC

NI KWELI, Vifo vyao vilifanywa na serikali ya marekani....askari wa kizungu ndio aliyempelekea rafiki yake Wallace risasi za kumshoot Tupac usiku ule Tyson akiwa anajiandaa kuingia ulingoni

Huyohuyo akatengeneza mazingira ya BIG kuuwawa.

Hata wale washkaji zake Tupac aliochana nao kwenye nyimbo nyingi...wale. Wahuni wote waliokuwa wanajiita Idd Amin, San Abacha, Mobutu n.k. wote walikuja kuuawa kinamna namna.....!

Mmoja wao alitoroka akaenda kuishi Nairobi then akaishi Arusha, pale uzunguni nyumba yake ya ghorofa moja inaangaliana na uwanja wa uzunguni pale karibu na shule ya Prime...!

Yeye ndiye alikuwa anawapa itikadi na kampani kina JCB, Spark na wana hiphop wa mwanzoni Arusha.

Hahaha...alikuwa anasema wazi kabisa akiwa serious kuwa ukikuta Mtu mweupe (Mzungu) mahali popote muue tu, na alishamtemea mate usoni mzungu pale mbele ya NBC bank akiwa anatoka nje.

Kauli yake ilikuwa ''Just kill them All n I ll take your case''

Alikuja kuwa rasta na mama yake ni Mjamaica.

Ukipata wasaa wa kukutana naye atakueleza mengi sana kuhusu BIG na 2PAC na vifo vyao na atakuonesha picha tangu wakiwa wadogo shuleni na kina 2pac.
 
Walikuwa Violent sana hasa Tupac na Suge Knight na waligawa jamii ya waafrika nchini Marekani....hasa makundi kama Blood and Clip vijana wakawa wanauana sana......nadhani hata vifo vyao kuna mkono wa Serikali ya Marekani
Katika suala la violence, basi kulikuwa na kiumbe Eric Wright au Easy E, huyu jamaa alikuwa mtata sijaona tena!
 
Du,kwa hiyo jamaa anaish hapa bongo
Ndio Mkuu, japo sijamuona muda ila wana nyumba kabisa Uzunguni anaishi na mama yake Mjamaica mwenye dread....!

Yule alisoma shule moja na Tupac na wamekuwa pamoja na kuna picha mama yake tupac anawakumbatia wawili wakiwa machalii wadogo kabisa.

Nenda Mitaa ya Gymkhana barabara ya kuelekea mahakama kuu / Ikulu ndogo ulizia kwa BLACKII.
 
Katika suala la violence, basi kulikuwa na kiumbe Eric Wright au Easy E, huyu jamaa alikuwa mtata sijaona tena!
Ni Eazy E...sio Easy E

Alimtukana Dre mpaka anakata roho kutokana na HIV

Alizikwa na jeans, raba, T-shirt kubwa na kofia yake ya NWA

Huyu alikuwa na watoto zaidi ya 10 kwa wanawake tofauti.
 
Pamoja sana
Ndio Mkuu, japo sijamuona muda ila wana nyumba kabisa Uzunguni anaishi na mama yake Mjamaica mwenye dread....!

Yule alisoma shule moja na Tupac na wamekuwa pamoja na kuna picha mama yake tupac anawakumbatia wawili wakiwa machalii wadogo kabisa.

Nenda Mitaa ya Gymkhana barabara ya kuelekea mahakama kuu / Ikulu ndogo ulizia kwa Blackii.
 
bado hii sio justification.
pia hayo mastory ya kifo cha biggie na 2pac kila mtu ana theory yake anayopenda kuamini.
@Daudi Mchambuzi aliyeinjinia vifo vya hawa niggaz ni Mzungu haswaa aliyekuwa anaitwa Adams na alikuwa rafiki na familia ya kina Christopher Wallace (Biggie)

BIG na kundi lake walikuwa wahuni lakini hawakuwahi kununua wala kumiliki Guns kabisa, jiulize walipata wapi usiku ule?

Tupac alikuwa rafiki wa karibu sana na Mike Tyson hata ule usiku anapigwa risasi alikuwa anaenda kwenye pambano la Tyson na Tyson alishawahi kukiri kuwa Adams anahusika.
 
@ Daudi Mchambuzi aliyeinjinia vifo vya hawa niggaz ni Mzungu haswaa aliyekuwa anaitwa Adams na alikuwa rafiki na familia ya kina Christopher Wallace (Biggie)

BIG na kundi lake walikuwa wahuni lakini hawakuwahi kununua wala kumiliki Guns kabisa, jiulize walipata wapi usiku ule?

Tupac alikuwa rafiki wa karibu sana na Mike Tyson hata ule usiku anapigwa risasi alikuwa anaenda kwenye pambano la Tyson na Tyson alishawahi kukiri kuwa Adams anahusika.
Narudia tena, theory za kifo cha 2pac na biggie zipo zaidi ya 10 ni wewe tu unaamua uchague ipi utakayoridhika nayo.
hiyo unayosema hapo ni moja wapo na hakuna mwenye uhakika hata moja, sana-sana Suge Knight ndiyo anasuffer gerezani.
 
Umeongea kinyume mzee cardi B ndio yupo overrated lakini hao wengine ni moto wa kuotea mbali kwenge game la hiphop ya sasa..Migos wana influence kubwa sana kwenye Trap(The new subgenre of hiphop) hata hao wengine kina Travis scott wanajua aisee..anyway bado nafatilia mjadala nilitaka nichangie kuhusu hii tu
Usiongelee influence kwa sababu hata hapa bongo clouds kuna wasanii wasio na uwezo iliwabeba na wakawa na influence ila baada ya kuwatema hawakuweza kufurukuta tena na wametopea kwenye umaskini, yupo wapi mtu kama Best naso? Dullayo? PNC? Gosby?

Media za marekani zinafanya kazi kubwa kuwapush wasanii ili wafikie malengo yao kibiashara tu. Sikufichi, kama bongo biashara ya muziki ingekuwa katika mfumo kama wa marekani ungekuta watu kama kina marehemu Sam wa ukweli, Top C walishapiga hela na wanaishi kifalme japo mtu ana nyimbo 3 tu zinazofahamika.

Nirudi kwa hao Migos, jamaa wanafanya mumble rap ila wanatumia mahadhi ya Trap tu but they are not real hiphop artists ila wamebrandiwa kama hiphop artists binafsi naona wamekuja kuharibu mziki tu. Ni kama wamepenyea kwenye vocal za future wakazibaka na kufanya mutation ya kivyao ila kwa kuwa marekani Biashara ya muziki ni kama open source kila mtu ana chance ya kufanikiwa aki hit media basi kinachotakiwa ni kupata management yenye kukulink na media tu ukitoka umetusua life nawe unakuwa msanii mkubwa.

Trap ilianzishwa na T.I wayback kabisa nadhani ilikuwa 2003, ilikuwa ni mahadhi ya hiphop ambapo msanii analink muziki, lifestyle na maisha ya mtaa kwenye mashairi kukawa na specific kind of beats (Crunk beats) zinazotumiwa ndio T.I akaupa jina huo mziki ni trap music. Ulifika kwenye peak mnamo 2007 alipo release album yake ya papertrail. Hio style ya mziki ikazidi kwenda far wasaanii wakawa wanaongezeka taratibu Ace Hood, Rick Rozay, Dj Khaleed, Playaz Cirlce, Lil wayne, Glasses Malone, Bun B,Gucci Mane hao ni baadhi ya ninaowakumbuka.

Kuanzia 2009 mziki wa Trap ukaboreshwa zaidi na mahadhi yake ya beats yakabadilika kabisa. From there on mapigo yakabadilika na emergence ya vizazi vipya vya producers binafsi naweza sema bwamdogo "LEX LUGER" pongezi sana kwake na band yao ya production wanaojiita "808 MAFIA" ndio waliofanya transformation toka Crunk kuja mahadhi mapya ya trap musik ambayo ndio Trap Beats. Pia kuna mwamba wa kuitwa "Drumma Boy" huyu nae ni guru wa 2nd gen trap music.

Tazama mwenyewe kuanzia nyimbo ya Rick Ross ya "Blowing money fast!" nyimbo zote zilizofata zilianza ku sound kama instrumental ile. Msanii aliweza kuspit vitu vya kueleweka ila mziki ulibadilika vionjo tu. Wakaja kina Pill, Drake,Meek mill, kina kendrick lamar, kina Future,Cashout, Big Sean, French Montana, 2 chainz (tity boi) akaenda nae mainstream na ule mziki ndo ukawa kama 2nd generation ya Trap musik. Pia zimefanyika copy za rnb kwa trapbeats zikawatoa watu kama kina August Alsina na yule fetty wap still mziki ulikuwa unaeleweka.

Binafsi kuanzia 2015 naona mziki wa hiphop umekufa na sijaufuatilia tena tokana na lindi la mumble rappers kufululiza kuanzia wale madogo Husikii kinachoimbwa ni shouting tu, beats mbovu yani hakuna raha tena. Maana bora mtu asifie malaya, nyumba na magari ila beat iwe kali uinjoy mdundo. Sasa mashairi F na beats 0 nikakacha nikarudi kumsikiliza P.Funk kwanza.

Kurudi 2018 nikafarijiwa na Nipsey Hustle, pia kuna dogo nae anaitwa Roddy Ricch yuko vizuri mno. Kama kuna kizazi kipya cha rapper ambaye anastahili kupewa nafasi kwa sasa basi ni huyu chalii Roddy Ricch. He has Good sounding music na mashairi yanaeleweka, kwa mpenzi wa hiphop tafta mixtape yake inaitwa "Feed tha Streets 2"
ili uone kama hao kina Migos e.t al mna chochote. Cardi B pia ana flow ila sijawahi mkubali akisimama mwenyewe zaidi ya kwenye features tu.
 
Ni Eazy E...sio Easy E

Alimtukana Dre mpaka anakata roho kutokana na HIV

Alizikwa na jeans, raba, T-shirt kubwa na kofia yake ya NW

Huyu alikuwa na watoto zaidi ya 10 kwa wanawake tofauti.
Mkuu ilikuwa vipi jamaa kumtukana Dre ,wakati anakata roho ,chimba kidogo mkuu
 
Hawa jamaaa vifo vyao tutayazungumza mengi sana,cjui itachukua miaka m8ngapi ambapo mtu atajitokeza na kusema ukweli huu
Narudia tena, theory za kifo cha 2pac na biggie zipo zaidi ya 10 ni wewe tu unaamua uchague ipi utakayoridhika nayo.
hiyo unayosema hapo ni moja wapo na hakuna mwenye uhakika hata moja, sana-sana Suge Knight ndiyo anasuffer gerezani.
 
Back
Top Bottom