Tupatiane True Story yoyote ila iwe Fupi na Precise

Huu uzi umefichua maadui walokua hawajuaniπŸ˜‚πŸ˜‚
 
KISA CHA PILI
Baada ya Isha kuwekwa relini kiberenge kimkanyage akatokea msamalia mwema akamuokoa..!!
Isha akarudi nyumbani kwao, alivyofika hakumkuta mama yake, akamkuta mama mwingine ambaye ni bi mdogo akimtazama wako same age.!! (Likawa tatizo jipya)

Wakaanza kila mara wanagombana, Yule bi mdogo anamtukana Isha ndoa imemshinda kaja kuvunja na ndoa ya baba yake..!!

Baba yake akipelekewa mashtaka anatukana na kusema kama wanashindwa kupatana basi atawakaza wote 😹(Isha alisema baba yake ni wale wababa wanaolima bhang hivyo yupo km chizi fresh) Kuna kipindi polisi walivamia shamba lake wakamwambia, β€œKwanini unalima madawa ya kulevya?” Aliwajibu yeye anatumia km mboga..!! Wakamwambia km ni mboga basi ipike ule, kweli bhana yule baba yake Isha akapika bhangi km inavyopikwa mchicha akala na ugali. 😹

Sasa kuna siku mama yake mdogo akapotelewa na chachandu zake, mtu wa kwanza kumtuhumu ni Isha coz adui yake mkubwa..! Baba yake alivyosikia bila ustaarabu akavamia chumba cha Isha akaanza kupekua huku anafoka anataka chachandu za mkewe zirudishwe chap, hizo ndo zinafanya yeye aone dunia tamu..!!

Isha anasema alilia sana ile siku baba yake anamdhalilisha, baba yake bila aibu akamvua shanga Isha akampa mkewe na akamfukuza Isha nyumbani na kipigo juu.!!
 
Nakumbuka tupo form six mbeya,Kuna rafiki yangu aliniomba nimsindikize sehemu mitaa ya nonde, kumbe ni kwa mganga wa kuonesha kwenye "Tv", sasa jamaa akanyweshwa dawa akaambiwa akae saa nzima itakuwa imekua active tayari kwa kuangalia jambo lake kwenye hio"Tv", inakua sio Screen,ni kitambaa tu . Sasa jamaa alikua ni mnywaji wa pombe kali ile dawa ikawa inachelewa kuwa activated.

Mganga akamwambia kama rafiki yako atumii pombe, anywe hii dawa wewe utakuwa unamwelekeza tu unataka uone nini awe anauliza,nikanywa,haikupita nusu saa nikawa tayari tukaingia kale kachumba kana giza,ila nikawa naona vzr kwenye kile kitambaa matukio na alioitaji jamaa kuona na nakumbuka wale wachawi kwenye kile kioo walikua wanakuja wamegeuzia kisogo hawataki kuonekana,ila unawafosi...kuna mmoja mpaka alikuja palepale tulipo kupambana.

Ile kuondoka ile dawa ilikua haijaisha vzr kichwani, njiani nilikua naona mambo ya hatari sana, viumbe wa ajabu,watu wapo uchi ,mavichuguu makubwa,aisee ile siku .
 
Nimemaliza zangu form 4 nikawa nipo tu home napiga vyuma nikatanuka bonge la kono,mwaka ujao nikaenda kusoma makongo one day navuka zangu Road naona wachumba wa makongo wale wa A Level wananikata jicho mtoto mmoja mkali akaniambia kwa sauti ya juu I like your body du! Mpaka leo hiyo sauti haitoki kichwani mwangu
 
🀣🀣🀣🀣🀣🀣
Aisee kwli huyu baba ni nommaaa
 
Hahahah
Sasa hivi ni single maza ana watoto wa 3 😁😁
 
Stori za Vijiwe vya kahawa hizi pale Kariakoo
 
πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€” Aiseee
 
Kuna mtoto wa jirani yetu kama form 3 hivi(me), aligombana na mama yake, akaenda kujinyonga , mama yake kwa hofu na kilio akaja speed kuniita, njoo nisaidien mwanangu anakufa, ile kukimbilia nakuta chalii linaning'inia, nikadaka ile miguu kama kumnyanyua hivi ili kamba isiendelee kumuumiza, alafu tukaita watu wakaja na ngazi wakakata ile kamba, ndo ikawa ameokolewa,,, alizimia kama 45mins ndo akazinduka hajitambui na wenge kama lote,,,alikuwa keshakojoa, nadhan alikuwa ameshamuona Israle mtoa roho live ,,, ! Yule chali nimempita kama 8yrs, since then mpk Leo yule dogo kama ananiogopa ama kunionea aibu, hAyupo huru akiniona, ananiamkia anapita hivi,,,



Yule ni first born, mama yake ni teacher, mjane,,after lile tukio mama yake alileta mazoea mazoea,,,nadhan alitaka kunipa ahsante lkn sikuipokea,,, ! Tunaheshimiana mpk Leo
 
πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿πŸ’ͺ🏿 Hongera sanaaaaaa pia hongera zaidi kuwa kutokuwa kijana wa ovyo kumtafuna mama wa watu πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ₯³
 
Chai
 
Story yangu fupi...

Nilizaliwa, nikabalehe na sasa naendela kuishi.

Hiki ni kisa cha kweli🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…