Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,370
Kijiwe niaje!
Ni wengi ambao tunawajua watu wakiwa maarufu ila ni wachache zaidi tunaowajua kabla ya kuwa maarufu aidha kwa kusoma nao, kujuana nao, kucheza nao utotoni, n.k
Binafsi kwa huku Mbeya namkumbuka Izzo Business alikuwa ni mtu moja mchangamfu ila muziki wake alionekana na watu lazima wengi kama muhuni, huku sisi vijana wadogo tukiwa tunatamani angalau kuwa na urafiki nae au kuchana mistari kama yeye, miaka ya 2005 nakumbuka alifanyiwa interview na Mbeya Tv basi ile interview niliirekodi kwenye mkanda wa deki, huo mkanda ulizunguka sana mitaani watu wamcheki Izzo B anavyohojiwa.
Nakumbuka pia alifahamika shule kibao za sekondari kama Sangu tukitoka alikuwa na washkaji zake na vile alivyo staa wa Mbeya tulipenda sana kampani yake.
Wasanii wengine nliowajua kwa juu juu kuna msamiati huyu alieimba yeye na Rapcha "Moto Unaweka" nae wa mbeya alisomaga mbalizi nahisi, ila alikuwa mtoro na mzee wa wida.
Karibuni, muwe mnatia nyama basi, sio unasema tu umesoma au kufahamiana na fulani, jaribu kuelezea kwa undani.