Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Kweli wewe umesoma Azaboi, ongeza kwenye list hapo watu wakorofi kama man tapa, Pengo, Zinde hukumkuta wewe, muddy kipande nae hukumkuta pia,
Sema pale watu maarufu ni Mohamed yupo Azam pale, Iman Nsamila mpiga picha maarufu wa January Makamba na Samatta, Ben Paul tulisoma nae pale Advance ila yeye hakusoma PCM na kipindi hicho hakua maarufu

Sent using Jamii Forums mobile app

Zinde yule msela mavi wa kuwapiga makonda?
 
2010 naingia Tandika sec, namkuta Hamisa mobetto yupo form 2 asee yule demu alikua hatulii anapiga misele shule nzima na viswaswadu wenzie.
Siku za dini utamkuta kwa walokole anaimbisha kwaya hadi nilijuaga mlokole kumbe wapi.
Mobeto 2010 alikuwa form 3, shule ya msingi amesoma Muungano temeke.
 
Kwanza kabisa Diamond alinichoma na spoke ya baiskeli akilitaka barafu la sh 20 nililokuwa nikilinyonya kijitonyama kisiwani pale uwanja wa mpira miaka ya 1997-99(sikumbuki the exactly year). Tulikuwa tunakawaida ya kucheza mpira tukitoka mazoezi ya uministrant kigangoni kabla ya kujengwa kanisa lililopo sasa. Mashindano ni kati ya watoto tunaotokea upande wa Knyama kuu na wale wanaoishi kuanzia kijitonyama kisiwani mpaka Tandale huko. Padre alikuwa akitokea parokia ya mwananyamala kuja kusalisha kigangoni.
Haha nikaja kukutana nae kwenye event yake 2014-15 pale Mlimani City keshakuwa maarufu, isingekuwa Ruge na mdogo wangu ambaye yuko THT clue yakina Linah, Rachel, Barnabas, Ditto na wengine asingenikumbuka. Tulikumbushana, tukacheka na tumeshayasahau hayo
Pili Nimeisoma na Feruzi wa Daz Nundas Kizuka TPDF sec. School Moro hiyo, Kama atasoma hii post alikuwa anapenda sana kuniita toto tundu maana nilikuwa napenda Sana kuimba nyimbo zao.
Tatu mtaani kwetu akahamia Mangwear akiwa chini ya jamaa mmoja anaitwa Evans na mdogo wake Nancy Kijitonyama wakiwa wanapigisha simu (ile ya waya TTCL unatoa hela kwa dakika kama sijasahau ilikuwa 250). Hapo ndipo lilipozaliwa kundi la East Zoo
Prof J usimsahau dogo lako uliyekuwa ukimshauri maliza kwanza shule ndio uingie kwenye sanaa maana wewe ndio ulikuwa rol modal wangu mpaka kwenda kwa MI Kamwamba Upanga kurekodi. Nilifuata ushauri wako na namshukuru Mungu now ni mhasibu na ni muajiriwa, mambo ya bongo flavor nilishatupa kule
Kwa leo tuishie hapo...
Hiki ndo kisa Cha kugombana na Evancy aliponikuta Ghetto na mdogo ake Nancy_ CowObama
 
Back
Top Bottom