Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Kwanza kabisa Diamond alinichoma na spoke ya baiskeli akilitaka barafu la sh 20 nililokuwa nikilinyonya kijitonyama kisiwani pale uwanja wa mpira miaka ya 1997-99(sikumbuki the exactly year). Tulikuwa tunakawaida ya kucheza mpira tukitoka mazoezi ya uministrant kigangoni kabla ya kujengwa kanisa lililopo sasa. Mashindano ni kati ya watoto tunaotokea upande wa Knyama kuu na wale wanaoishi kuanzia kijitonyama kisiwani mpaka Tandale huko. Padre alikuwa akitokea parokia ya mwananyamala kuja kusalisha kigangoni.
Haha nikaja kukutana nae kwenye event yake 2014-15 pale Mlimani City keshakuwa maarufu, isingekuwa Ruge na mdogo wangu ambaye yuko THT clue yakina Linah, Rachel, Barnabas, Ditto na wengine asingenikumbuka. Tulikumbushana, tukacheka na tumeshayasahau hayo
Pili Nimeisoma na Feruzi wa Daz Nundas Kizuka TPDF sec. School Moro hiyo, Kama atasoma hii post alikuwa anapenda sana kuniita toto tundu maana nilikuwa napenda Sana kuimba nyimbo zao.
Tatu mtaani kwetu akahamia Mangwear akiwa chini ya jamaa mmoja anaitwa Evans na mdogo wake Nancy Kijitonyama wakiwa wanapigisha simu (ile ya waya TTCL unatoa hela kwa dakika kama sijasahau ilikuwa 250). Hapo ndipo lilipozaliwa kundi la East Zoo
Prof J usimsahau dogo lako uliyekuwa ukimshauri maliza kwanza shule ndio uingie kwenye sanaa maana wewe ndio ulikuwa rol modal wangu mpaka kwenda kwa MI Kamwamba Upanga kurekodi. Nilifuata ushauri wako na namshukuru Mungu now ni mhasibu na ni muajiriwa, mambo ya bongo flavor nilishatupa kule
Kwa leo tuishie hapo...
Kwaiyo umeajiriwa sio?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma shule moja Tausi (yule muigizaji mfupi) ana pacha wake anaitwa Rose Mdegera. Mkorofi ni sijawahi kuona.

Sec mi nikiwa primary mshua anafundisha Tosamaganga basi nakaa kota alikua anasoma mdogo wake Prof J Black Rhyno alikua anaimba sana kwenye graduu
Uyo pacha ake tausi ni mfupi kama yeye?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli wewe umesoma Azaboi, ongeza kwenye list hapo watu wakorofi kama man tapa, Pengo, Zinde hukumkuta wewe, muddy kipande nae hukumkuta pia,
Sema pale watu maarufu ni Mohamed yupo Azam pale, Iman Nsamila mpiga picha maarufu wa January Makamba na Samatta, Ben Paul tulisoma nae pale Advance ila yeye hakusoma PCM na kipindi hicho hakua maarufu

Sent using Jamii Forums mobile app
Abdul Mohammed alikua GS bora zaidi Azaboy na alikua anatangaza EATV wkt yupo shule akaja kupata deal BBC London...nilimkuta akiwa form 4 wakati naanza form 1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijiwe niaje!!, Ni wengi ambao tumewajua watu walipokua maarufu ila ni wachache waliwajua kabla ya kuwa maarufufu hususani wasanii.

Binafsi kwa huku Mbeya namkumbuka izo business alikuwa ni mtu moja mchangamfu ila muziki wake alionekana na wengi kama muhuni, Kuna siku nakumbuka aliletwa hadi home hapa kisa ugomvi na msanii mweingine aliyelalamika izo alimuibia biti au mashairi yakawa mabishano ila walimalizana, Nakumbuka pia alikuwa akipita hapa shule ya sekondari sangu tukitoka alikuwa na washkaji zake na vile alivyo staa wa mbeya tulipenda sana kamapani yake,


Karibuni, Muwe mnatia nyama basi, sio unasema tu umesoma au kufahamiana na flani, Jaribu kuelezea kwa undani
Short course flani hivi somewhere wayback ya hobby yangu moja, na dogo London Tyler Holmes,siku ya kumaliza walinialika m2 mzima kwenye sinsin afterparty,daamn kama umeoa unaweza ukataliki mke[emoji23][emoji23]..
Still nina Ka connection nae uchwara ,
Nmekua fan wake sana tho ni kizazi cha madogo, ngoma ikiaza"we got London on da Track" madogo utaskia kasoma na mshua hhh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Short course flani hivi somewhere wayback ya hobby yangu moja, na dogo London Tyler Holmes,siku ya kumaliza walinialika m2 mzima kwenye sinsin afterparty,daamn kama umeoa unaweza ukataliki mke[emoji23][emoji23]..
Still nina Ka connection nae uchwara ,
Nmekua fan wake sana tho ni kizazi cha madogo, ngoma ikiaza"we got London on da Track" madogo utaskia kasoma na mshua hhh

Sent using Jamii Forums mobile app
Ujue watu wengi hawajamfahamu London on the Track. Nilimjua kupitia ngoma ya Young Thug.
 
Ujue watu wengi hawajamfahamu London on the Track. Nilimjua kupitia ngoma ya Young Thug.
Ilo true mkuu,jamaa ni mkali na very humble guy,Sio mpenda umaarufu na life lake anapenda liwe private tho ni bata boy hhh..
Jamaa ana respect ya wahuni kbao,y-thug,t.i,kodak, drake,tyga ,r-h-quan to mention the few

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesona na ROMA mkatoloki pale USAGARA SEC wakati huo yeye ni basketballer anaetegemewa na shule huku mm ndo mwanamuziki bora zaidi pale.
Nakumbuka alikuwa anakuja kunipa ushauri akiwa na ANTONIO NUGAZ huyu wa Clouds (msemaji wa YANGA)
Jamaa walikuw wananikubali sana japo kuwa walinitangulia kidogo ila walinitambua mchango wangu.

Hata ile ngoma ya Roma (TANZANIA ) tumeplay kwa first time mahome SAHARE SEPOCHO 1

Ila chukushangaza wenzangu wametoboa mimi kibarua changu KUBET

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom