Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Nimesoma na shamia shughuli msasani.

Darasa na sita kizimkazi primary school.

Nilikua kiranja wao nawapiga makonzi darasa zima.
 
Mwasiti almasi alikua jirani yetu enzi maishi mwenge tangu akiwa mdogo alikua anapenda sana kuimba
 
Ndio kakakimbilia kwenye sanaa. Kamshukuru sana Kanumba kukaingiza huko baada ya kukalamba mzigo alafu akajimilikisha. Ila wasanii wa bongo bhana dah[emoji1787][emoji119]
Lulu kaanza sanaa akiwa mdogo sana nadhani alikuwa shule ya msingi
 
Kwanza kabisa Diamond alinichoma na spoke ya baiskeli akilitaka barafu la sh 20 nililokuwa nikilinyonya Kijitonyama Kisiwani pale uwanja wa mpira miaka ya 1997-99 (sikumbuki the exact year). Tulikuwa tuna kawaida ya kucheza mpira tukitoka mazoezi ya uministrant kigangoni kabla ya kujengwa kanisa lililopo sasa. Mashindano ni kati ya watoto tunaotokea upande wa Knyama kuu na wale wanaoishi kuanzia kijitonyama kisiwani mpaka Tandale huko. Padre alikuwa akitokea parokia ya mwananyamala kuja kusalisha kigangoni.

Haha nikaja kukutana nae kwenye event yake 2014-15 pale Mlimani City keshakuwa maarufu, isingekuwa Ruge na mdogo wangu ambaye yuko THT clue yakina Linah, Rachel, Barnabas, Ditto na wengine asingenikumbuka. Tulikumbushana, tukacheka na tumeshayasahau hayo

Pili Nimeisoma na Feruzi wa Daz Nundas Kizuka TPDF Sec. School Moro hiyo, kama atasoma hii post alikuwa anapenda sana kuniita toto tundu maana nilikuwa napenda sana kuimba nyimbo zao. Tatu mtaani kwetu akahamia Mangwear akiwa chini ya jamaa mmoja anaitwa Evans na mdogo wake Nancy Kijitonyama wakiwa wanapigisha simu (ile ya waya TTCL unatoa hela kwa dakika kama sijasahau ilikuwa 250). Hapo ndipo lilipozaliwa kundi la East Zoo

Prof J usimsahau dogo lako uliyekuwa ukimshauri maliza kwanza shule ndio uingie kwenye sanaa maana wewe ndio ulikuwa rol modal wangu mpaka kwenda kwa MI Kamwamba Upanga kurekodi. Nilifuata ushauri wako na namshukuru Mungu now ni mhasibu na ni muajiriwa, mambo ya bongo flavor nilishatupa kule
Kwa leo tuishie hapo...
wew mbona kama black rhino
 
Nmesoma nawaziri mmoja kwenye selikali hii ya samia. Tumesoma pale udsm. Mwaka wa tatu tukapanga geto msewe.. tukawa tunacheki nae porn na kwenda kimboka. Ila kwa sasa ni mheshimiwa. Tunafahamiana fresh ila hatuwasiliani.
Labda kama unajiwezaaa na una mishe ya maaan..!! Hiyo cennection muhimu sana.
 
Nimesoma na deus kaseke &Walter chilambo s/m jitegemee mbeya, deusi alikuwa mtundu mno comedy nyingi ukae naye usicheke utakuwa na
matatizo,alikuwa anapenda kunionea[emoji30]kipaji cha kucheza mpira..
Walter alikuwa anapendwa na wasichana hatarii..yaani ukiwa naye hee unajiona wewe ndo queen wa darasa[emoji1787] hadi walimu walikuwa wanampenda alikuwa na nyota ya kupendwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Me nakuuliza tu... Hii Jitegemee ndy ile imepakana na Shule ya Msingi Mlina reli au jitegemee gani???
 
Huu uzi ukiendelee hivi hvi..
Hapo 2028 kuna mtu atakuja kusema alisoma na Director Poor brain 😂😂😂😂😂😂😂😂
Dadek enzi hizo mimi sishikiki...
 
Nilisoma kidato cha 5&6 na wasanii wawili wa gospel na tukawa close Goodluck Gozbert-mwakavuta high school makete na Joel lwaga-njombe secondary school. kiukweli kama Good alikuwa anajuhud sana kulikuwa na mshkaj anajiita barl kiss wa mafionso ndo alikuwa mpinzani wake na jamaa alikuwa na kipaji kikubwa na walikuwa wanashindana kwenye night of talents na siku za graduations au welcome form5 cjui yeye kapotelea wapi alikuwa anaimba sanaaaa mastyle kama chege na kuhusu joel lwaga huyu wala hakuna mtu alijua atakuja kuwa msanii mana alikuwa mtu wa mpira sana, mkimya daily anashinda Gora anasali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesoma shule gani sasa njombe boy au mwakavuta
 
Huu uzi ukiendelee hivi hvi..
Hapo 2028 kuna mtu atakuja kusema alisoma na Director Poor brain 😂😂😂😂😂😂😂😂
Dadek enzi hizo mimi sishikiki...
Umeuongoza vyema Mkuu unastahir respect ya P.Funk au Master J katika uzi huu😅
 
Back
Top Bottom