Tupeane maujanja ya Dream League Online/Offline

Wang Shu

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
2,562
Reaction score
3,715
Wakuu,
Wadau na wapenzi wa games njoeni tupeane maujanja ya kucheza Dream league game online,offline na local multiplayer.
Natumia kikosi cha Liverpool hiki hapa

Sifa ya wachezaji wangu wote wana urefu wa 204CM inaniwezesha kucheza kwa kujiamini wana kasi,mipira ya juu naichukua vizuri.

Pia wachezaji wote wanapiga miguu yote kulia na kushoto kwaiyo hainipishida shida kupanga kikosi kila mfumo ninaotaka.

Sijawai kuvuka division 5 naishia hapo nikiwa na stress nacheza sana nafungwa sana nashuka mpaka tier 10 naanza upya kupandisha division πŸ˜‚

Karibuni wajuzi wa ku-Hack nakadhalika,tunasubili toleo jipya 2020/2021.
 
Ninalo tatizo me huwa silichezi sana hasa online. Niko division 7.
Yeah huwa huchezwa wakati wa utulivu umekosa la kufanya mi mara nyingi nikiwa siko sawa inanisaidia kunipunguzia stress nakutana na mtu online nacheza uku nachati nacheka kidogo,nakasirika nikishinda nafurahia mda unaenda.
 
Online kuna watu wanafumua mpk unajiuliza walio division ya kwanza wapoje wapoje..πŸ˜‚
Maana unakutana na division ya 6 watu wanagada..

Hili gemu mi naona lina kaudhaifu fulani hasa kwa mabeki hata wawe na spidi 100 lkn bado kuwapata maforward inasumbua! Ni lzm ufungwe tu!.. ndio maana wengine huchukua wachezaji wa Kati au ma forward huwaweka kama mabeki!..
 
Sio mchezo online unatandikwa mpaka simu unatmani huivunje πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mkuu we umewai kuwe forwards nyuma matokeo yalikuwaje?
 
N
Niliwai kuhack nikafika division 1 nilifungwa lakini ni nili survive kiugumu saaana,ili ubakie unatakiwa ushinde mechi 6 jumla ya mechi zipo kama 12
 
Sio mchezo online unatandikwa mpaka simu unatmani huivunje πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mkuu we umewai kuwe forwards nyuma matokeo yalikuwaje?
Sijawahi kuwaweka mi nachezaga tu kawaida hata sahivi kuna njemba nimetoka kulitwanga 4 kwa 3 jamaa lilikuwa limenipania!
Ila ndo nimemzidi hako ka moja..πŸ˜…
 
Sijawahi kuwaweka mi nachezaga tu kawaida hata sahivi kuna njemba nimetoka kulitwanga 4 kwa 3 jamaa lilikuwa limenipania!
Ila ndo nimemzidi hako ka moja..πŸ˜…
Nishawai kufungwa 6 -0πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚nikimpata mnyonge najipozea
 

Maelezo ya kulihack tafadhari nateseka sana
 
Ulikuwa wapi ku kanseli ndugu..?
πŸ˜‚πŸ˜‚sijawai ku kaseli ndugu napambana mpaka mwisho, alafu ukizoesha kukata kata app ya game inaleta shida inakuwa nzito ukicheza na kugandaganda
 
Mkuu download hivi kitu alafu rename hivi profile.dat
Kama umefanikiwa kukidownload na kurename fuata maelezo ya picha click kwenye kila alama nyekundu tumia App inaitwa ZArchiver kufungulia file maneger alafu fanya hivi

Usisahau iyo kwenye picha ya mwisho ni hatua ya mwisho usisahau kuweka kuweka tiki kwenye "Apply to all files" Ukishafanikiwa ivyo cancell app zote zinazorun underground kisha kafungue game utaona game limebadilika kuanzia wachezaji na coins zitakuwa unlimited haziishi wala haziongezeki.
Jalibu alafu nipe mrejesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…