Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

Nimeanza nayo kaka nilivyo press enter ndio ikaniletea hivyo angalia hata kwenye screenshot pale kwenye fx
OK.. Pole Kwa usumbufu ulioupata...
Ongeza column mbili pembeni ya hizo then mwanzo andika =VALUE( F2) then Drag itakuletea value hizo hizo alafu zitumie kutafuta Average... Fanya hivo hivo Kwa columns ingine alafu unipe feedback... Unapokosea ndio unazidi kujifunza
Nimeanza nayo kaka nilivyo press enter ndio ikaniletea hivyo angalia hata kwenye screenshot pale kwenye fx
 
Pia kwa mfano kwenye hiyo screenshot hapo juu post [HASHTAG]#357[/HASHTAG] hapo kwenye column c nataka niweke actual age but nikiweka formula nikipata majibu mawili ninavyohighlist nidrug zilete majibu ya hizo nyingine za chini inacalculate tofauti cjui kwa nin
Umetumia formula gani kutafuta Age ?
 
Wadau,

Kujua Excel Spreadsheets ni muhimu sana...

Tunaweza tukashirikishana tricks mbalimbali katika Excel hapa ili tujifunze wote..

Unaweza pandishwa CHEO au Kupata kazi kirahisi Kwa kujua EXCEL vizuri.. Watanzania wengi udhaifu wao upo hapo.. So Unaifanya WEAKNESS hiyo kuwa Strength kwako.Kwenye Ofisi yeyote mtu ambaye haogopi excel huwa anaonekana ni kichwa sana.. unaweza pia ukamvutia bosi wako kama utaijua kumshinda yeye na atakufanya rafiki yako ili usimuumbue...

Kwenye Interview ndio utawamaliza kabisa ..ukikutana na viherehere wakakuchokoza hapo ndio unawaonesha ujuzi wako wote... wengi huwa hawaijui kwasababu ya uvivu... Kwa hiyo usiogope..Niliwahi ulizwa swali na panelist kwenye Interview nikaenda deep mpaka akaogopa maana kuna vitu alikuwa havijui na yeye akaamua apotezee hilo swali akarukia kitu kingine kukwepa aibu..

Weka Trick yako hapo chini ili wengine wafaidi au kama unaswali uliza nitakujibu mimi au wadau wengine...

Ingependeza sana pale unapokwama uulize swali hapa.. Ili tujadiliane vitu ambavyo ni useful katika mazingira yetu ya shule au kazini...

Dunia ya sasa sio lazima uende darasani.. Unaweza tumia muda wako na MB zako vizuri mtandaoni na ukaongeza Ujuzi polepole

**Kama unatafuta kazi na umeandika Kwenye CV kwamba una ujuzi na Excel fuatilia huu uzi na group uwe updated na vitu mbalimbali ili usije umbuka siku ukiwa unafanya written au Oral Interview

** Nitakuwa naelezea Common questions ambazo waajiri hupenda kuuliza kukupima uelewa wako katika Spreadsheets.. Ni Muda na MB zako tu.. Sihitaji kingine...

Please NOTE

** Usiulize kitu unachokijua kupima watu Bali andika trick unayoijua ili wengine wafaidi na kama unaswali ULIZA wataalam tutakusaidia

PS:
Kama upo Telegram unaweza Ingia Kwenye Public Channel ipo hapo chini Kwa vitu ambavyo haviwezekani kuelezewa hapa vizuri..Kama video na files. Ni public channel ya kusoma na Sio sehemu ya chatting!

gonga hapo >>>> Excel/SpreadsheetsTZ

Naomba kuwasilisha!

Ethos
Naomba kuelekezwa mfano Nina data kwenye Colmn "B" na Zingine Colomn "D" sasa lengo nataka kuangalia zinazomatch kwa kutumia Excel nitatumia njia gani? Ahsante.
 
OK.. Pole Kwa usumbufu ulioupata...
Ongeza column mbili pembeni ya hizo then mwanzo andika =VALUE( F2) then Drag itakuletea value hizo hizo alafu zitumie kutafuta Average... Fanya hivo hivo Kwa columns ingine alafu unipe feedback... Unapokosea ndio unazidi kujifunza
Mkuu ubarikiwe sana imekubali pia tunaomba usichoke kwa maswali yetu
 
Let say inaanzia hapo 662, nimechukua =C1-C662 ikanipa jibu, nikaendelea C1-C663 Ikanipa jibu ninapo hilight na kudrop down inanipa majibu ambayo siyo tena kuanzia 1k inakua na negative
Screenshot 2016-11-28 10.49.19.png
 
Naomba kuelekezwa mfano Nina data kwenye Colmn "B" na Zingine Colomn "D" sasa lengo nataka kuangalia zinazomatch kwa kutumia Excel nitatumia njia gani? Ahsante.
Mkuu Asante Kwa Swali lako zuri

Tumia Function ya

=EXACT (A1, B1)

A1 na B1 ndio CELL za Column unazolinganisha then Drag down

Angalia video ipo Kwenye Group Letu pia
 
Let say inaanzia hapo 662, nimechukua =C1-C662 ikanipa jibu, nikaendelea C1-C663 Ikanipa jibu ninapo hilight na kudrop down inanipa majibu ambayo siyo tena kuanzia 1k inakua na negativeView attachment 440675
Weka Alama ya dola $ katika ya C1 yaani =C$1 alafu drag kama kawaida

Hapo tatizo ni kwamba unapo drag bila Alama ya dola hiyo C1 inabadilika inakuwa C2, C3 na kuendelea.. Ili kuweka iwe constant tumia $

Nipe feedback baada ya kufanya hivo
 
Nahitaji kujua kama nikiongeza data nyingine za bidhaa..je formula itakuwa ivo ivo hapo juu au formula inabadilika
 
Nahitaji kujua kama nikiongeza data nyingine za bidhaa..je formula itakuwa ivo ivo hapo juu au formula inabadilika
Itabadilika mkuu ila ni range tu kutokana na data zilizo ongezeka.. Kama ilikuwa C1 hadi C4 na data zikaongezeka hadi C10 hakikisha una edit Kwenye formula pia... au unaweza weka range kubwa ili hata ukiongeza data isikupe tabu
 
Weka Alama ya dola $ katika ya C1 yaani =C$1 alafu drag kama kawaida

Hapo tatizo ni kwamba unapo drag bila Alama ya dola hiyo C1 inabadilika inakuwa C2, C3 na kuendelea.. Ili kuweka iwe constant tumia $

Nipe feedback baada ya kufanya hivo
Ahsante sana nimefanikiwa mkuu
 
Itabadilika mkuu ila ni range tu kutokana na data zilizo ongezeka.. Kama ilikuwa C1 hadi C4 na data zikaongezeka hadi C10 hakikisha una edit Kwenye formula pia... au unaweza weka range kubwa ili hata ukiongeza data isikupe tabu
Mkuu nimefanikiwa..kwa tatizo la kwanza..
 
mkuu nahitaj kupanga matokea ya mtihan ambapo nimeshafanya total ila nataka mwanafunz mwenye maksi kubwa awe wakwanza kwenye page bila kuwapa namba 1,23... nitumie formula gan
 
Safi sana mkuu.... Hakuna kitu kigumu duniani... Tuweke juhudi tu na jifunze kitu kidogo kila siku... Niliwahi enda sehemu mzungu kashikilia nafasi kisa tu ni mtaalam wa haya madude iliniuma sana
Ni kwel kabisa i wish tutaelewa zaid na zaid..nimekuwa najifunza sana..nimependa sana VLOOKUP..hasa ktk biashara...
Nakumbuka kuna siku nilienda Duka flan la Jeshi Lugalo kununua Dawa..muuzaji Mjeda akawa anatumia hii..kunitajia bei za dawa...nilibaki nashangaa sana nimeduwaa....
Nikamwona mtaalamu sana...

Dah leo na mimi kupitia msaada wenu nimeielewa
 
Safi sana... VLOOKUP hata kama una bidhaa 1000 unaweza Jua bei ya kila kitu au information yeyote ndani ya dakika moja!
 
mkuu nahitaj kupanga matokea ya mtihan ambapo nimeshafanya total ila nataka mwanafunz mwenye maksi kubwa awe wakwanza kwenye page bila kuwapa namba 1,23... nitumie formula gan
Yaani awe wa kwanza Kwa jina.. Uweze kusoma wa kwanza hadi wa mwisho moja Kwa moja?
 
Yaani awe wa kwanza Kwa jina.. Uweze kusoma wa kwanza hadi wa mwisho moja Kwa moja?
ndio mkuu
mfano
john 70 70 60 80 =100
lucy 30 20 50 10 =200
60 50 59 78 =500
huyo mwenye namba kubwa apande juu mwenye ndogo ashuke
 
Back
Top Bottom