Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

ndio mkuu
mfano
john 70 70 60 80 =100
lucy 30 20 50 10 =200
60 50 59 78 =500
huyo mwenye namba kubwa apande juu mwenye ndogo ashuke
Nimekuelewa... Ni rahisi sana highlight data zako zote halafu nenda Kwenye DATA >>>> SORT itakuletea Diolog box

Hakikisha umechagua VALUE na Column ya Jumla ambayo unataka ndio itumike then hapo hapo chagua From large to small then Gonga enter
 
Alama ya dola kazi yake ni nini hasa? Na alama ! je?
Alama ya dola inatumika ku hold cell isibadilike pale unapo drag down

Alama ya ! Mara nyingi huonekana pale unapotaka data katika Sheet Moja ionekane Kwenye Sheet ingine

Mfano.. Kama A1=10 Kwenye sheet1 ukitaka ionekane katika sheet2 andika

=sheet1!A1
 
Hii Office unayotumia ya mwaka gani mkuu? mi imenipa shida kidogo kupata "custom" kwenye "number"
Issue hapo ni namna ya kwenda kwenye opt ila ni very simple

Kama unapata ugumu tumia ile ya '00.0....kulingana na idadi ya 0 ambazo unazihitaji
 
Sasa kwa mimi nisiejua kabisa inakuwaje? Maana juzi kuna jamaa yangu aliniambia nijifunze Excel kwa sababu wanahitaji mtu wa IT ofisini kwao
 
Sasa kwa mimi nisiejua kabisa inakuwaje? Maana juzi kuna jamaa yangu aliniambia nijifunze Excel kwa sababu wanahitaji mtu wa IT ofisini kwao
Ndio uanze kujifunza
 
Alama ya dola inatumika ku hold cell isibadilike pale unapo drag down

Alama ya ! Mara nyingi huonekana pale unapotaka data katika Sheet Moja ionekane Kwenye Sheet ingine

Mfano.. Kama A1=10 Kwenye sheet1 ukitaka ionekane katika sheet2 andika

=sheet1!A1

Mkuu habari! nimefatilia ile clip ya kirekebisha marks ila tatizo pale sjaelewa vizuri mfano;-
  1. Nachoomba kujua kama nikiwa nataka kuwaongezea wanafunzi marks 7 kila mwanafunzi kwenye somo la maths na wapo 65?
  2. Kingine pale napotaka kurekebisha marks za wanafunzi watano tu katika 65 ambao baada ya kusahihisha upya nimegundua nimewakosesha marks mmoja 18,14,19,5 na 23 respectivelly. Naomba msaada hapo mkuu wangu.ahsanteh.
 
Mkuu Asante Kwa Swali lako zuri

Tumia Function ya

=EXACT (A1, B1)

A1 na B1 ndio CELL za Column unazolinganisha then Drag down

Angalia video ipo Kwenye Group Letu pia
Mkuu nimejaribu inaniandika False basi. Yaani Hizi data siyo kwamba ziendana kwa Row, hapana zipo shagalabaghala. Unaweza kutu data iliyo kwenye Colomn A Rowa ya 3 ikafanana na iliyo kwenye Colomn B Row ya 1.
Ahsante.
 
Naomba picha tafadhali nizione
 
Unaweza uka
Mkuu habari! nimefatilia ile clip ya kirekebisha marks ila tatizo pale sjaelewa vizuri mfano;-
  1. Nachoomba kujua kama nikiwa nataka kuwaongezea wanafunzi marks 7 kila mwanafunzi kwenye somo la maths na wapo 65?
  2. Kingine pale napotaka kurekebisha marks za wanafunzi watano tu katika 65 ambao baada ya kusahihisha upya nimegundua nimewakosesha marks mmoja 18,14,19,5 na 23 respectivelly. Naomba msaada hapo mkuu wangu.ahsanteh.
ongeza column pembeni na kuandika mfano =B1+7 na B1 ndio marks za zamani then drag down

hao watano nadhani unatakiwa u edit tu..Kumbuka primary data inatakiwa iwe sahihi siku zote Excel inakusaidia tu kufanya uchambuzi na uchakataji
 
Napenda kutoa pongezi za dhati kwa bw. Ethos kwa msaada anaotupatia nilikuwa kapa kwenye kutumia Program jedwali lakini kwa msaada wake hadi sasa hv nimepata ABC Kuhusu exel. Mungu akuzidishie moyo wa majitoleo uzidi kutuelimisha.
 
Kwenye Invoice au Risiti. Kama unataka idisplay tarehe na muda wa kuiandika, enter the following formula. =now() . Hapa kila kitu utachofanya itajiupdate muda automatically.
Sasa hz formula utakalili au kuna namna ya kujua kuziandika?
Asante Kwa Swali Lako Mkuu..

Nenda Kwenye Cell unayotaka iwe affected.. Right Click nenda hadi Kwenye FORMAT CELLS then click baada ya hapo zitatokea options nyingi chagua CUSTOM then upande wa kushoto inatokea options kibao ambazo zinaanza na ## futa weka 0 kulingana na idadi unayotaka then Drag..

Natumaini nimeweza kukujibu. Karibu Kwa Swali lingine...
eeb636925330c0bc626d85e01dd54f9c.jpg
 
Unajuaje kazi y inatumika formula x? Then binafsi ni beginner mkinipa maujanja ya kuandika hzo kanuni itakuwa safi sana
 
Unaweza uka

ongeza column pembeni na kuandika mfano =B1+7 na B1 ndio marks za zamani then drag down

hao watano nadhani unatakiwa u edit tu..Kumbuka primary data inatakiwa iwe sahihi siku zote Excel inakusaidia tu kufanya uchambuzi na uchakataji

Ahsanteh mkuu na hii z sore hpo kwenye video kwa group ina kazi gani ni kufanya standardization au ni vipi maan nmeona kuna mtu alikuwa ana 48 ikaja 40 sasa je ni kazi yake kupunguza tu au na kuongeza ebu nichambulie hapo mkuu upande wa z score
 
Naomba kuuliza nataka niprint data zangu zipo nyingi sana ila nataka kichwa cha habari kitokee katika kila page nimefreeze panel but imegoma kutoa kichwa cha habar kwenye page zingine
 
Naomba kuuliza nataka niprint data zangu zipo nyingi sana ila nataka kichwa cha habari kitokee katika kila page nimefreeze panel but imegoma kutoa kichwa cha habar kwenye page zingine
Ziko kwenye excel or word
Kama ziko kwenye word fanya hivi:-
1. Insert>header> sasa kwenye header utachagua uandike kichwa cha habari na kinaonekana kila page
 
Back
Top Bottom