Tupeane maujanja ya Excel

Wakuu nina excel workbook ziko 168(Invoices), sasa kila workbook ina details zifuatazo

-Invoice date
-Purchases Order # (PO)
-Invoice #
-Description
-Amount (Exclusive)
-Vat
-Amount (Inclusive)

Nisaidieni kama Naweza zi-link au kuziweka kwenye template moja itakayokuwa na mtiririko wa hapo juu. Lengo la kufanya hivo ni kutaka kujua total value ya Invoices zote (168)

Naweza kulinki,au kukopy na kupaste data hizo lakini hilo zoezi linaweza chukua muda mrefu

cc😡 Njuka II ,Tutor B
 
@Njuka II
 
Nadhani ulikuwa unamaanisha workbook yenye worksheet 168
Nakumbuka nilishawahi kuelekeza jinsi ya kulink worksheets, soma comment no 618
Asante kwa maelezo mkuu, but hizi ni Invoices ambazo ziko kila moja na workbook yake, sio workbook moja yenye sheet 168
 
Asante kwa maelezo mkuu, but hizi ni Invoices ambazo ziko kila moja na workbook yake, sio workbook moja yenye sheet 168
Ok, ili kuunganisha workbook mbili tofauti inabidi workbook zote uwe umezifungua
Kama ndio upo kwenye workbook2, na unataka uilink na worbook1 unatype = then unaenda pale chini kwenye task bar, ukigusa icon ya Excel zitatokea screen za workbook zote mbili zikiwa na majina yake, so unaselect screen ya workbook 1 then unaselect cell (unaendelea na step zile zile za kutype formula)
Ukibadili data kwenye workbook 1, changes zinatokea na kwenye workbook 2
 
Link nipe
 
Mtabe wa Excel, SPSS, STATA, nk Mwanza atoe Namba yake
 
Hiyo nyepesi sana ndugu
 
Nataka jinsi nitaandaa printed report automatically kwa excel,kusort kuweka madaraja na rank nafahamu ,average nk zote hizo nafahamu
 
Thanks in advance, ngoja nijaribu mkuu, kwa case yangu nitatakiwa kuzifungua zote 168 alafu nifate hizo procedures, yaani niwe nafungua tano tano ili kurahisisha,au naweza kuwa na alternative ingine hapo??
 
Kwanini usiwe na workbook moja yenye worksheet nyingi kuliko kuwa na workbook nyingi zenye worksheet moja moja? Workbook moja ina worksheet ngapi?
 
Kwanini usiwe na workbook moja yenye worksheet nyingi kuliko kuwa na workbook nyingi zenye worksheet moja moja? Workbook moja ina worksheet ngapi?
Haina shaka mkuu, but unakuta ni kazi umeletewa iko katika mfumo huo, workbook moja inaweza kuwa hata na worksheet 1000 au na zaidi kulingana na mahitaji yako
 
MKUU Njuka II nashukuru Sana Kwa msaada wako. Nimetumia ushauri na maelekezo Yako vizuri Sana na nimepata nilichokuwa nakitaka.
Kuna project nilikuwa naifanya ya shule flani hivi na Sasa imefanikiwa kwa asilimia 99. Zimebaki finishing ndogo ndogo TU.
Ubarikiwe.
 
Amin
Asante kwa kushukuru ndg, we are together

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia fill
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…