Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

Pia usisahau Match & index, as lookup function
Watu wengi wanatatizika na lookup functions, siku nikipata muda nitaelezea mbadala wake SUMPRODUCT. Na uzuri wa SUMPRODUCT function ni kwamba ina uwezo wa kufanya multiple lookup
 
Habari mkuu? Unaweza ukaelezea jinsi ya kuitengeneza PAYE formula? Huwa kila nikijitahidi kui-master nashindwa. Hizo comma na brackets nyinginyingi huwa nashindwa kuzielewa kabisa matumizi yake.
PAYE ni nini mkuu? Hili neno ni geni kwangu
 
PAYE ni nini mkuu? Hili neno ni geni kwangu
Mkuu PAYE ni kifupi cha "Pay as You Earn", ni computation ya kucalculate kodi kwa individual. Ipo kama ifuatavyo: Kipato kisichozidi 170,000 hakuna kodi. Kipato kinachozidi 170,000 lakini hakizidi 360,000, kodi yake ni 9% ya kiasi kinachozidi 170,000. Kipato kinachozidi 360,000 lakini hakizidi 540,000 kodi yake ni 20% ya kiasi kinachozidi 360,000 plus 17,100. Kipato kinachozidi 540,0000 lakini hakizidi 720,000, kodi yake ni 25% ya kiasi kinachozidi 540,0000 plus 58,100. Kipato kinachozidi 720,000, kodi yake ni 30% ya kiasi kinachozidi 720, 000 plus 98,100. So, mlolongo wote huu wataalamu wa excel wanakuwekea fomular tu. Sasa mie binafsi huwa inanishinda kuidevelop hii formula.
 
Hiyo D5 ni mfano tu ambapo ndo utakuwa unaweka salary, na hiyo formula utaiandika ktk cell unayotaka idisplay kodi yakoView attachment 1076569
Mkuu, upo sahihi kabisa. Tatizo langu sitaki kukariri. Hiyo formula naweza kuimeza. Ninachohitaji ni interpretation ya hizo alama kwenye hiyo formula ili niweze kuitengeneza mwenyewe. Nikiweza kujua hizo codes nitakuwa kwenye position ya kutengeneza formula yoyote.
 
Vizuri, muhimu kujifunza itakufanya uweze kutatua task nyingi zaidi. Mfano Mimi huo mfumo wa PAYE ndo nimeusikia kwako leo lakini kupitia maelekezo yako, nimetumia basics kucreate formula
 
Wadau,

Kujua Excel Spreadsheets ni muhimu sana...

Tunaweza tukashirikishana tricks mbalimbali katika Excel hapa ili tujifunze wote..

Unaweza pandishwa CHEO au Kupata kazi kirahisi Kwa kujua EXCEL vizuri.. Watanzania wengi udhaifu wao upo hapo.. So Unaifanya WEAKNESS hiyo kuwa Strength kwako.Kwenye Ofisi yeyote mtu ambaye haogopi excel huwa anaonekana ni kichwa sana.. unaweza pia ukamvutia bosi wako kama utaijua kumshinda yeye na atakufanya rafiki yako ili usimuumbue...

Kwenye Interview ndio utawamaliza kabisa ..ukikutana na viherehere wakakuchokoza hapo ndio unawaonesha ujuzi wako wote... wengi huwa hawaijui kwasababu ya uvivu... Kwa hiyo usiogope..Niliwahi ulizwa swali na panelist kwenye Interview nikaenda deep mpaka akaogopa maana kuna vitu alikuwa havijui na yeye akaamua apotezee hilo swali akarukia kitu kingine kukwepa aibu..

Weka Trick yako hapo chini ili wengine wafaidi au kama unaswali uliza nitakujibu mimi au wadau wengine...

Ingependeza sana pale unapokwama uulize swali hapa.. Ili tujadiliane vitu ambavyo ni useful katika mazingira yetu ya shule au kazini...

Dunia ya sasa sio lazima uende darasani.. Unaweza tumia muda wako na MB zako vizuri mtandaoni na ukaongeza Ujuzi polepole

**Kama unatafuta kazi na umeandika Kwenye CV kwamba una ujuzi na Excel fuatilia huu uzi na group uwe updated na vitu mbalimbali ili usije umbuka siku ukiwa unafanya written au Oral Interview

** Nitakuwa naelezea Common questions ambazo waajiri hupenda kuuliza kukupima uelewa wako katika Spreadsheets.. Ni Muda na MB zako tu.. Sihitaji kingine...

Please NOTE

** Usiulize kitu unachokijua kupima watu Bali andika trick unayoijua ili wengine wafaidi na kama unaswali ULIZA wataalam tutakusaidia

PS:
Kama upo Telegram unaweza Ingia Kwenye Public Channel ipo hapo chini Kwa vitu ambavyo haviwezekani kuelezewa hapa vizuri..Kama video na files. Ni public channel ya kusoma na Sio sehemu ya chatting!

gonga hapo >>>> Excel/SpreadsheetsTZ

Naomba kuwasilisha!

Ethos
Ahsante kwa darasa
 
Leo tuangalie jinsi ya kupangilia formula nyingi zilizounganishwa.
Kwa kawaida Excel ikikutana na jibu zaidi ya moja, basi huwa inaexcute formula ya kwanza na kuliacha jibu lingine linalofata. Nitaweka mifano miwili ili mnielewe ninachomaanisha

Mfano wa kwanza
Angalia formula ya kwanza na ya pili ktk screen shot hapo chini

Ktk formula ya kwanza, nimeandika mpangilio kutokea ndogo kwenda kubwa.
Hapa majibu utayopata hayatokuwa sahihi kwa sababu IF ya kwanza imezimeza IF zingine zote zilizobaki, na hata ukiandika value yoyote ktk D10 ambayo itakuwa ni kubwa kuliko 0 (lets say 90) basi itakuletea F kwa sababu hata 90 nayo ni kubwa kuliko 0, hivyo excel inaexcute na kustop ktk IF ya kwanza

Ktk formula ya pili nimeanzia kubwa kwenda ndogo
Hapa utapata majibu sahihi kwa sababu, IF ya kwanza haijazimeza IF zilizobaki (kila IF ipo kivyake) mfano ukiweka 90 ktk D10, excel itaanza na IF ya kwanza na kustop bila kuendelea na IF zilizobaki kwa sababu 90 ni kubwa kuliko 81.
Ukiweka value ambayo ni ndogo kuliko 81 (lets say 75),excel itaiexcute IF ya kwanza na kujump kuendelea na IF inayofata kwa sababu 75 ni ndogo kuliko 81. Ikifika kwenye IF ya pili itastop na kuleta jibu kwa sababu 75 ni kubwa kuliko 61. Process itaendelea hivyo hivyo mpaka jibu litakapopatikana, na kama data uliyoweka kwenye D10 hukuizungumzia kwenye formula yako (mfano ukiweka negative number, (D10
Individual formula zinaweza kuwa correct lakini ukibadilisha mpangilio unaotakiwa ,majibu utayoyapata hayatokuwa sahihi.

IMG_20190422_150139_129.JPG
 
Ninauliza uwezekano wa kuwa na template ya excel ambayo unaingiza data, baada ya kuclear data ulizoingiza zinabakia ili uweze kuingiza nyingine na zifanye increment kwa data za awali zinazobakia. Mwongozo tafadhali.
 
View attachment 1078210
Vipi kama kwenye formula yakwanza nikaondoa hiyo greater ">" nakuweka less "<" ?
 
Ninauliza uwezekano wa kuwa na template ya excel ambayo unaingiza data, baada ya kuclear data ulizoingiza zinabakia ili uweze kuingiza nyingine na zifanye increment kwa data za awali zinazobakia. Mwongozo tafadhali.
Itabidi uwe sheet mbili, moja ya data entry na nyingine ni ya kuextract data kutokea sheet 1 (data entry). Ktk sheet 2 itabidi utumie lookup with criteria. Data zako zitaji-save kulingana na criteria zako. Mfano unasema kama G10 itaandika FORM 1 basi lookup ianzie kwenye S/N 1 mpaka 50 kama ni FORM 2, lookup ianzie S/N 51 mpaka 100 n.k. Ukiita value ya G10 list itajiupdate bila kuifuta list ya kwanza
 
Bravo mkuu
 
Wataalam naomba msaada kwa anaefahamu VBA ya xls, ni siku nyingi nafanya kazi na xls sheet naifahamu kiasi fulani ila inapokuja issue ya developing program through xls nashindwa hata kutengeneza form ama kiprogram kidogo cha kuwasaidia end user wengine. Msaada tafadhali kwa wanaojua kupiga code za VBA xls
Kama hujui code kabisa unaweza ukatumia default form ya excel.
Kwanza kabisa customize Quick access toolbar(QAT) yako kwa kufata hizi step

Click tab yoyote kwenye ribbon hapo juu (eg home, file,view,insert n.k), then rightclick >> customize QAT
Badilisha hiyo default option ya Popular commands iwe All commands, utaona list imejiupdate. Kwenye list yako,tafuta kitu kimeandikwa form. Ukiipata,iclick then add (add button ipo katikati ya hizo list mbili, list ya kulia na list ya kushoto)
Malizia kuclick OK, utaona icon ya form imejiadd kwenye QAT yako

Baada ya hapo,select row yako yenye titles (mf. Row inaweza ikawa na hizi details>> s/n,name,age,place of birth n.k) then click hiyo icon ya form kwenye QAT, form yako itadisplay ikiwa na labels za title yako na text field za kufill data.
Ukijaza details zako kwenye hiyo form, details zinajiadd chini ya title row
 
Maswali hayo wanatoboa great thinkers
Kutumia excel haishindikani, nafikiri walikuwa wanamjaribu kama anajua kutumia Merge na Wrap. Kwenye excel ukiandika kitu kikazidi upana wa column, kile kilichozidi kinajificha, sasa nadhani walitaka aandike docs bila kufanya autofit ili atumie marge na wrap
 
Back
Top Bottom