Leo tuangalie jinsi ya kupangilia formula nyingi zilizounganishwa.
Kwa kawaida Excel ikikutana na jibu zaidi ya moja, basi huwa inaexcute formula ya kwanza na kuliacha jibu lingine linalofata. Nitaweka mifano miwili ili mnielewe ninachomaanisha
Mfano wa kwanza
Angalia formula ya kwanza na ya pili ktk screen shot hapo chini
Ktk formula ya kwanza, nimeandika mpangilio kutokea ndogo kwenda kubwa.
Hapa majibu utayopata hayatokuwa sahihi kwa sababu IF ya kwanza imezimeza IF zingine zote zilizobaki, na hata ukiandika value yoyote ktk D10 ambayo itakuwa ni kubwa kuliko 0 (lets say 90) basi itakuletea F kwa sababu hata 90 nayo ni kubwa kuliko 0, hivyo excel inaexcute na kustop ktk IF ya kwanza
Ktk formula ya pili nimeanzia kubwa kwenda ndogo
Hapa utapata majibu sahihi kwa sababu, IF ya kwanza haijazimeza IF zilizobaki (kila IF ipo kivyake) mfano ukiweka 90 ktk D10, excel itaanza na IF ya kwanza na kustop bila kuendelea na IF zilizobaki kwa sababu 90 ni kubwa kuliko 81.
Ukiweka value ambayo ni ndogo kuliko 81 (lets say 75),excel itaiexcute IF ya kwanza na kujump kuendelea na IF inayofata kwa sababu 75 ni ndogo kuliko 81. Ikifika kwenye IF ya pili itastop na kuleta jibu kwa sababu 75 ni kubwa kuliko 61. Process itaendelea hivyo hivyo mpaka jibu litakapopatikana, na kama data uliyoweka kwenye D10 hukuizungumzia kwenye formula yako (mfano ukiweka negative number, (D10
Individual formula zinaweza kuwa correct lakini ukibadilisha mpangilio unaotakiwa ,majibu utayoyapata hayatokuwa sahihi.
View attachment 1078210