Tupeane maujanja ya Excel

Tupeane maujanja ya Excel

Duuh very helpfull mkuu at least kwa maneno hayo napata picha kwa mbaali khs coding maana hua sielewi hata nini kinafanyika.

Kuna sehemu nilikua napitia pitia kuhusiana na mambo ya VBA ndio nikaona watu wanabishana kama kujua coding ni muhimu kwa wanaojifunza au la.


So kuijua VBA ipasavyo ni lazima uwe unajua kutumia excel ipasavyo(no shortcut kwny hilo suala sio mkuu?
Ktk VBA,kuna muda utahitaji uwe na basic za excel formulas hasa pale unapotaka kuandika VBA functions. Mfano kama hujui Vlookup ktk excel formula, na kule ktk uandishi wa codes za VBA function pia itakupa shida. Inakuwa ni mfano wa mtu anayetaka kufanya practical wakati hana theory ya hiyo practical
 
Ktk VBA,kuna muda utahitaji uwe na basic za excel formulas hasa pale unapotaka kuandika VBA functions. Mfano kama hujui Vlookup ktk excel formula, na kule ktk uandishi wa codes za VBA function pia itakupa shida. Inakuwa ni mfano wa mtu anayetaka kufanya practical wakati hana theory ya hiyo practical
Sawa mkuu i appreciate,nimekusoma vyema.
 
CONVERT function

Hii ni function inayotumika kubadilisha unit moja kwenda unit nyingine,mfano unataka ubadilishe mita 100 kwenda ktk futi /inch n.k

Syntax

=CONVERT(Number, from_unit,to_unit)

Ukiwa unaandika hii function yako ktk formula bar na ukatype hiyo alama ya koma ya mwanzo,list za from_unit zitajidisplay zenyewe, utachagua unit yako unayotaka then utaweka tena koma ya pili,utaona list nyingine ya to_unit inadisplay utaselect then utaclick enter

Mfano tukitaka tubadili masaa 24 kwenda ktk siku,tutaandika hivi

=CONVERT(24,"hr","day"), jibu litakuja 1

Alama za double qoute ("") katikati ya units zinakuja zenyewe baada ya kuselect unit yako ktk list zinazojidisplay, huna haja ya kuziandika manually.
 
DEGREES function

Hii ni function inayotumika kubadili angle kutoka ktk radians kwenda ktk degrees

Syntax

=DEGREES(angle)

Eg , tukitaka kubadili pie(π) iende ktk degrees,tutaandika hii formula


=DEGREES(PI()), jibu>>>180°
=DEGREES(PI()/2), jibu>>>>90°

Nb. PI() pia ni function ambayo huwa ina return jibu la Pie (3.14....)



RADIANS function

Hii ni function inayotumika kubadili angle kutoka ktk Degrees kwenda ktk radians


Syntax

=RADIANS(Angle)

Eg tukitaka kubadili 180° kwenda ktk radians tutaandika

=RADIANS(180), Jibu>>>>>3.14....

Trigonometric ratios zote huwa zinacalculate values za angle zikiwa ktk radians

Mfano ukiandika =SIN(30) hutopata 0.50 kama inavyojulikana, lazima uibadili angle yako iende ktk radians kwanza.

Eg. =SIN(RADIANS(30)) Hapa ndipo utapata 0.5
 
Excel ni pana mno mkuu,yaani kumuelezea mtu ambaye ni advanced user inakuwa ngumu kidogo labda ufanye comparison kati ya mtu na mtu ndipo unaweza conclude kwamba huyu ni very advanced kuliko huyu.

Coding sio ngumu mkuu,just upate basics zake tu. Nakupa mfano mmoja wa kukuonesha kwamba code sio ngumu kama inavyoogopwa.

Code ni kama ilivyo English,ktk english kuna nouns/objects,verbs na kadhalika na ktk codes pia iko na mtindo huo

Mfano ktk excel worksheet,cell,workbook n.k zote hizo ni objects na print,select,copy,clear n.k hizo ni verbs

Code ukitaka uielewe isome kuanzia kulia kwenda kushoto kama mas-hafu inavyosomwa.
Kati ya object na verb huwa tunatenganisha na alama ya dot/nukta(.)

Mfano nikitaka nifute range flani ya cells,nitainsert button then nitaziandika code hizi

Worksheets ("Sheet2"). Activate
Range("B6:J15"). Select
Selection.Clear


Soma code kutokea kulia kwenda kushoto, line ya kwanza inaactivate sheet2, line ya pili inaselect range yako unayotaka kuifuta na line ya tatu inaifuta range yako. Ni sawa tu na step unazozifanya manually.

Kama upo sheet5 na unataka ufute vitu vya sheet2 manually ni lazima tu utaanza kuclick sheet2 kwenye sheet tab then utaselect cells unazotaka kuzifuta na mwisho utaright click na kuclear contents(ni same na code lines tulivyozipanga hapo juu). Sasa kwa sababu action zote tumezistore kwenye code window basi tukiclick button yetu range inajifuta yenyewe.

Hii button unaweza ukaiweka hata kwenye sheet4(sheet yoyote) na ukiiclick inaenda kufuta data za sheet2 kama ulivyoicommand lakini kama hiyo button umeiweka ktk sheet2 na data unazotaka kufuta ziko sheet2,basi hiyo line ya kwanza ya code inakuwa ni optional (hata usipoiandika ,button itafanya kazi) Hapo ndo utaona kazi ya kuactivate.

Habari Mkuu,
Nimtumiaji sana wa excel hasa formulas naomba ushauri kupata formula ambayo itasolve hii issue

ProductKg 1Kg 2Kg 3
A201525
B152535
A201015
C355020
B204030

Nataka formula ambayo itanipa Average Kg 1 & 3 Kwa product A , nimetumia hii lakini haijafaa
=AVERAGE(IF(a3:a5="A",b3:d5)) kama Array
Nikiitumia kwa Kg 1,2&3 inanipa jibu sahihi lakini nataka nipate average kwa Kg 1&3 tu
Asante,
 
Habari Mkuu,
Nimtumiaji sana wa excel hasa formulas naomba ushauri kupata formula ambayo itasolve hii issue

ProductKg 1Kg 2Kg 3
A201525
B152535
A201015
C355020
B204030

Nataka formula ambayo itanipa Average Kg 1 & 3 Kwa product A , nimetumia hii lakini haijafaa
=AVERAGE(IF(a3:a5="A",b3:d5)) kama Array
Nikiitumia kwa Kg 1,2&3 inanipa jibu sahihi lakini nataka nipate average kwa Kg 1&3 tu
Asante,
Sijakuelewa mkuu, hizo namba ulizoandika ni kama zimeungana. Jaribu kutuma picha ya hizo data zinavyoonekana kwenye screen ya pc
 
Okay poa,niliweka table nadhani kwenye pc ingeonekana vizuri,nimeattach picha tayali mkuu
Sijakuelewa mkuu, hizo namba ulizoandika ni kama zimeungana. Jaribu kutuma picha ya hizo data zinavyoonekana kwenye screen ya pc
table.JPG
 
Okay poa,niliweka table nadhani kwenye pc ingeonekana vizuri,nimeattach picha tayali mkuuView attachment 1177314
Nafanya assumption kwamba column ya kwanza ni column A na hiyo A imeanzia kwenye A2, andika hii formula katika cell unayotaka upate average
=(SUMIF(A2:A6,"A",B2:B6)+ SUMIF(A2:A6,"A",D2😀6))/(COUNTIF(A2:A6,"A")×2)

A6,B6, na D6 unaweza ukazibalisha kulingana na ukubwa wa table yako mfano kama table inaenda mpaka A100 basi range yako pia itabidi iwe inaishia na 100 (eg A100,B100 n.k). Ukihitaji avarage ya B utabadili kwenye formula,sehemu iliyoandikwa "A" utaandika "B"
 
Hapana mkuu.. hapo atakuwa amevuruga mpangilio... Anachotaka ni kumpanga mwanafunzi wa kwanza hadi wa mwisho .. hapo anatakiwa atumie RANK function kama nilivo eleza hapo juu..

Asante kwa upendo wako na kujaribu kutoa mawazo
Hii itapanga tu majina alphabetically
 
Hapa namaanisha mfano unarecord vitu,kufunga hesabu,kupanga matokeo ama kazi nyingine ndiyo unavozidi kujua functionalities zakila parameter
Kwa experience yangu excel ili kuijua vizuri inategemea na kazi ila ukitaka kuijua kitu kimojamoja asee ina mambo mengi kinyama
 
Naomba maujuzi ya kuandika barua kwa ku2mia excell..
 
Back
Top Bottom