Excel ni pana mno mkuu,yaani kumuelezea mtu ambaye ni advanced user inakuwa ngumu kidogo labda ufanye comparison kati ya mtu na mtu ndipo unaweza conclude kwamba huyu ni very advanced kuliko huyu.
Coding sio ngumu mkuu,just upate basics zake tu. Nakupa mfano mmoja wa kukuonesha kwamba code sio ngumu kama inavyoogopwa.
Code ni kama ilivyo English,ktk english kuna nouns/objects,verbs na kadhalika na ktk codes pia iko na mtindo huo
Mfano ktk excel worksheet,cell,workbook n.k zote hizo ni objects na print,select,copy,clear n.k hizo ni verbs
Code ukitaka uielewe isome kuanzia kulia kwenda kushoto kama mas-hafu inavyosomwa.
Kati ya object na verb huwa tunatenganisha na alama ya dot/nukta(.)
Mfano nikitaka nifute range flani ya cells,nitainsert button then nitaziandika code hizi
Worksheets ("Sheet2"). Activate
Range("B6:J15"). Select
Selection.Clear
Soma code kutokea kulia kwenda kushoto, line ya kwanza inaactivate sheet2, line ya pili inaselect range yako unayotaka kuifuta na line ya tatu inaifuta range yako. Ni sawa tu na step unazozifanya manually.
Kama upo sheet5 na unataka ufute vitu vya sheet2 manually ni lazima tu utaanza kuclick sheet2 kwenye sheet tab then utaselect cells unazotaka kuzifuta na mwisho utaright click na kuclear contents(ni same na code lines tulivyozipanga hapo juu). Sasa kwa sababu action zote tumezistore kwenye code window basi tukiclick button yetu range inajifuta yenyewe.
Hii button unaweza ukaiweka hata kwenye sheet4(sheet yoyote) na ukiiclick inaenda kufuta data za sheet2 kama ulivyoicommand lakini kama hiyo button umeiweka ktk sheet2 na data unazotaka kufuta ziko sheet2,basi hiyo line ya kwanza ya code inakuwa ni optional (hata usipoiandika ,button itafanya kazi) Hapo ndo utaona kazi ya kuactivate.