Ndoa nyingi za wasomi ndio huwa zina matatizo. Na matatizo mengi kwa kiasi kikubwa huwa yanasababishwa na akina mama, tena kama mama ana elimu kubwa au ana uwezo mkubwa wa kipesa kuliko baba hapo tena ndo balaa. Ule ubaba unakuwa hauna maana kabisa. Mama ndo atataka kutawala nyumba, ukisema hiki jibu lake usinibabaishe na visa kedekede. Jaribu kufanya kautafiti kadogo tu, hata viongozi na wasomi wengi wanawake aidha huwa hawana waume au ndoa zao huwa zina migogoro mikubwa sana.
Ninayo mifano mingi sana ambayo nimeishuhudia mimi mwenyewe ya wanandoa ambao mama aidha ana uwezo na elimu kubwa kuliko baba au wako sawa. Wengine huwa wanafikia hata hatua ya kulala vitanda tofauti, asubuhi kila mtu anaondoka na gari yake japo wanafanya kazi ofisi moja. Basi ilimradi vurumai.
Akina mama/dada jirekebisheni (siwatuhumu). Fedha na elimu haviwezi kununua mapenzi.