mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
siyo suluhisho,nmnazungumza,yanaisha.
kama mnazungumza kila siku hayaishi je?????? Huoni unahatarisha maisha yako kimsingi!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
siyo suluhisho,nmnazungumza,yanaisha.
Ukiniacha hautauona Ufalme wa Mbingu.
Maty kuna vitu ambavyo obviously unaweza kuvumilia lakini ndio wife anakung'utwa nje na limjamaa hapo ngumu sana banaa.Nyie watu acheni kuchakachua changieni, tusikie na kutokwa kwenu bana
ni kweli watoto ndo wanapata matatizo na matatizo yapo mengi na wakati mwingine sio lazima mtu awe malaya
Pia inategemea ni mambo gani,yaani nyie kila siku mnazungumza tu na hamfikii muafaka hapo kuna mmoja atakuwa na tatizo au mmoja anajifanya anajua kuliko mwenzakekama mnazungumza kila siku hayaishi je?????? Huoni unahatarisha maisha yako kimsingi!!!
Kudadadeki hebu rudi ndani kuna kitu nimesahau kukwambiaMbona mabegi yako getini tayari?Ahh ntarudi nikikumiss!
Huwa najiuliza mara nyingi lakini nakosa jibu zuri, naomba nipate mawazo tofauti tofauti, inaweza kutusaidia wengi wetu.
Wanandoa wengi hasa wa miaka ya sasa, wakikorofishana korofishana baada ya muda wanachoamua ni tuachane bwana kila mtu ataanza nataka niishi kwa amani, nahitaji furaha mimi maisha yenyewe mafupi haya. Ukute hiyo ndoa baba msomi ana kazi nzuri na mama vile vile ndio balaa, kila mtu anasema usinibabaishe ninaweza kumudu maisha.
Hapo kuna watoto mmezaa, lakini kila mtu utamsikia napenda kuishi kwa amani, ni vipi kuhusu watoto? Je hao hawatakiwi kuishi kwa furaha na amani wakiwa na baba na mama? Hivi hamuwezi kukaa mkazungumza na kuelewana ili mlee watoto pamoja badala yake mnafikiria kuachana?
Hivi kuachana ni suluhisho la matatizo yako? Na je ukiachana na mwenzio ndio kusema hutaki kuoa/kuolewa tena? Na je ukioa/olewa halafu huyo mwingine akawa na matatizo pia pengine kuliko uliyoyakimbia mwanzo utaachana nae pia? Au utavumilia?
Tushirikiane kupeana mawazo wandugu
Unarudi mkekani?Mkishamaliza kushauriana, mje mumwambie babu mlichoshauriana na kukubaliana.
BE nilifikiri unakuja St JosephMaty,
Hii mvua lazima niwahi kuondoka (kuacha) ofisini kuwahi Kanisa La Mtakatifu Kolbe - Mwenge...
Baadaye aka Later
Katika hili naomba tuwe wakweli na wawazi kabisa, mwanamke analaumiwa kwa vile ni mwanamke lakini si ndoa zote zenye matatizo wanawake ndio tatizo, no no no no and big no!!!!!!!!! Nina mfano mzuri kabisa wa mwanaume mwenye gubu lisiloelezeka! Angalia kwanza
Mwanaume form iv
Mwanamke Masters
Mwanaume baba wa nyumbani
Mwanamke anafanya kazi yenye akili
Mwanamke ndo anaendesha familia including yeye mwanaume hadi gari mwanaume kamnunulia na mambo mengine meeeeengi
Lakini cha ajabu na kushangaza mwanaume hajatulia na ana gubu acha tu hadi watu wanamuonea huruma mwanamke. Sasa hapo utasema wanawake wana matatizo jamani? Mwanaume na mwanamke woooooote wanapaswa kuheshimiana kama mke na mume si jukumu la mwanamke pekee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Mpaka niondoke ndo unakua na cha kuniambia??Niandikie barua...Kudadadeki hebu rudi ndani kuna kitu nimesahau kukwambia
Ni dhambi kubwa sana mwanamke kumwacha mwanaume.
Mwanamke anaachwa kama anavyo fuatwa kipindi cha kutongozana.
Mwanamke hapaswi kumwacha mwanaume kamwe bali anaachwa.
maty,
maisha ya ndoa ni mkanganyiko mtupu (confusion). Ukibahatika kuwa na amani basi mshukuru mungu. Ila kwa uzoefu wangu ni watu wachache sana wanayo hiyo amani.
Kuhusu watoto..inabidi wahusika wawafikirie sana ila isiwe kikwazo cha kuachana. Ikionekana kwamba hiyo ndoa haiwezekani kwa hali yoyote ile, basi ni vizuri sana watu wakaachana ili waanze upya. There is life after the first or second marriage ingawa huwezi kujua ipi itakuwa nzuri zaidi. Hata hivyo ni bora kumaliza tatizo la leo bila kujali kama kesho utakutana na kubwa zaidi au la. Kung'ang'ania kwenye ndoa ni hatari sana. Aunt yangu aliuawa na mume wake aliyempiga sana ikiwa ni kama siku 3 toka ajifungue. Inauma sana. Kama angewasikiliza wazee waliomwambia kuwa ile ndoa yake ilikuwa haiwezekani kabisa, labda hadi leo angekuwa hai.
Kuhusu maisha baada ya kutengena huwezi kujua kwa sasa. Ila kama biashara hailipi basi funga duka na kufanya kazi nyingine.
Mzee dc
ni kweli watoto ndo wanapata matatizo na matatizo yapo mengi na wakati mwingine sio lazima mtu awe malaya
r i p roho ya marehemu aunt yako.
imezidi kudhihirisha kuwa siyo kila jambo linavumilika.
Tuwe na kipimo kwa kila jambo.
degree ya uvumilivu kwenye ndoa ni ndogo sana kwa maisha ya sasa
ukizingatia wana ndoa wengi wana'jua' haki zao na hakuna anayetaka kujiweka chini
haya yote nadhani yameletwa na utandawazi..na hii kitu equality wanawake tunaililia pia i think inachangia kwa namna moja au nyingine
hakuna mwanamke wa siku hizi anataka kunyenyekea, wote wana/tuna penda kujilinganisha na wanaume..
mbaya zaidi ukikuta mdada kasoma ndo kabisaa hapo ni maswala ya 'nini nini usinichoshe nisikuchoshe nataka amani'..
tofauti na mama zetu walikuwa ni wanyenyekevu wazuri sana na wao pia walikuwa wanaangalia consequences za kuachana kwa watoto
lifestyle imebadilika generation hii ni selfish haiangalii watoto
in a nutshell, anayeweza kuifanya ndoa iendelee kuwepo ni mwanamke, na mwanamke wa sasa si mvumilivu.
Ni mtazamo tu.
Ukifikiria mara mbili mbili naona kama ni bora kubaki single hivi, nimenufaishwa na mawazo yenu wote, naona bora nibaki single tu