Tupeane mbinu za kujikinga na wezi kariakoo. Nimechomolewa wallet ina elfu 80/-

Sometimes wanatumia mbinu gani sijui, kulaumu ni basi tu.
 
Jaribu hii
1. Weka wallet lililotuma upande mmoja wa suruali lakini likiwa halina kitu ndani, na hela weka upande mwengine.
2. Pendelea sana mikono yako isitoke maeneo ya usawa wa mifuko, marakwa mara (sio kutia mikono mifukoni mara kwa mara). Na vile vile sio unatembea unarusha mikono kama mgambo wapo kwenye ruti machi[emoji13] [emoji13] [emoji13]
3. Ukishindwa kabisa nunua key holder yenye lock pande mbili, upande mmoja lock pochi yako na upande mwingine lock ndani ya suruali.
4. Unapoweka hela mfukoni usipende kujishtua, maana wezi ni rahisi sana kumsoma mtu.
5. Usipende kupita au kujibananisha kwenye makutano ya watu, maana wezi hutumia mwanya huo kwa urahisi sana.
6. Ukiwa kariakoo, usipende kugombea gari, iwe kupanda ama kushuka, maana hiyo ni fursa nzuri sana kwa wezi.
7. Ukimuona mtu anakucheki kwa umakini muoneshe dole la kati, maana wezi hupenda sana kujifanya kama wanakushangaa kumbe ndio wanakusoma personality yako, so ukimuonesha dole la kati wanakujua we ni muhuni wa kitaa, so wanakupotezea.
8. Usipende kununua vitu ovyo njiani maana wezi pia hutumia mwanya huo kukusoma na kukufatilia
9. Ukiingia kwenye duka lolote, usijifanye una haraka na kufanya manunuzi, angalia mtu anayekuja nyuma yako au kama uko ndani ya duka angalia hakuna mtu aliesimama nje ya duka anaetizama ndani
10. Chunguza, ukiona mtu mara mbili tatu kila ukizunguka yuo nyuma yako au unapishana nae mshtukie sana, muda mwingine wezi anaekusoma ni mwingine na anaekuja kukuibia ni mwingine, wanapeana michongo.

Ukiibiwa tena hapo, basi wewe usiende tena kariakoo au fanya huduma za manunuzi kupitia Tigopesa, M-pesa, Airtel money, halopesa au ezzypesa [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji377] [emoji377] [emoji377] [emoji124] [emoji125] [emoji125]
 
Ila hapo kwenye kujaa cards mmh[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Mimi nikiwa mjini kila baada ya sekunde moja mkono unakua umegusa kitu cha thamani nilicho nacho..
Yaani nikirusha mikono kutembea mkono mmoja ukirudi unagusa kwenye wallet na simu... mpaka leo sijawahi ibiwa hata 100...
Lkn kariakoo hakuna mbabe labda uwe mwizi ndio hautaibiwa lakini raia wa kawaida ni kwa neema tu
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] we noma naona umeipa mikono kazi ya guard
 
Usiweke hela kwenye wallet.

Usivae vimodo hivi visuruali vya kubana ndiyo vinafanya wallet ibaki juu na ijichore.

Kama unajijua wewe mtu akikuona tu anaconclude kua ni mshamba pesa weka kwenye begi la mgongoni. Zipu ya ndani.

Epuka muonekano na miondoko ya kishamba.
 
Kuwa serious unapoingia kkoo na usikubali kusongwa na mtu pia mwendo uwe mkali daaah umenikumbusha 2009
 
Jamaa ni ma expert,mimi nilichomolewa simu kwenye mfuko wa shati,tena ni muda kama wa dkk 2 nilikuwa nimetoka kujishika ili kukagua kama ipo,ile naingia kwenye taxi simu haipo,yaani mpaka leo sijiui ilitokaje ile simu,unaweza hisi ni ushirikina lakini wapi inafanyika kitaalamu sana...
 
Elfu 80 pesa ya kitanzania unaweka kwenye wallet?Hiyo Si pesa kidogo tu ya kuweka kwenye mfuko wa shati hapo mbele!Na kama una T-shirt weka tu mfuko wa suruali,wallet zinatunza card za bank dolar na vitu kama hivyo..si hii pesa ya madafu!
Hahahahaha my footage u cracking my ribs
 
Haya ni moja ya mateso ya kuishi Dar,huku mikoani maisha ni raha sana...
 
Mi nilinunua nguo vi brauz nilivion vzr kweli pale banana tu ukonga cha ajabu Kila nikichagua nazid kuzion nzuri mno nikanunua mzigo mzima brauzi 45 ivi kwajil ya kuvaa nikatoa pesa kufik home uwez amini brauz zote ni manyalunyalu wakat nilizijalibu afu nikashtuka why nimenunua brauz nying ivi
Jaman watu wachawi sana wanatumia dawa aseeee dah nilijikuta nalia
 
hii yako kali ila aujaibiwa we umenunua blauz mbaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…