Kitendo cha kuweka wallet mbele tu kinaonyesha ina hela ndio maana unaichunga sana hivyo vibaka watatumia kila mbinu kuifikia.
Ukiwa umebeba hela kwenye wallet yako usionyeshe wasi wasi na kuikagua sana mara kwa mara hii hutoa alert kwa vibaka pia kwamba jamaa ana mali.
Kama umevaa Jeans weka wallet yako mfuko wa nyuma upande wa kulia (hii ni kwa sababu mtu anapotembea mkono wa kulia hautulii hivyo utakua na wakati mzuri kuilinda wallet yako bila watu kujua kwamba unafanya ulinzi).
Hakikisha wallet yako unaiweka kwa upana (usiisimamishe hii hua rahisi kuchomolewa).
Lakini pia kama umesimama kwenye daladala pendelea kuegemeza upande wenye wallet yako kwenye viti vya abiria waliokaa itakua ngumu mtu kukusogeza ili akuibie.
Inakubidi pia kua mchunguzi kujua nani yuko nyuma yako ikiwa umesimama kwenye daladala au mwendo kasi, hii itampa hofu kwa kujua kwamba ulipomuangalia ulimkariri hivyo kitakachotokea utaanza nae matokeo yake kama sio kibaka anakua mlinzi wako tofauti na tabia ya watu wengi ambao akipanda daladala au mwendokasi hana muda wa kuangalia nani yuko nyuma yake.
Mwisho,
pendelea kuweka kijikaratasi chenye utambulisho wako kwenye wallet kama namba za simu na majina kamili, unaweza ukadondosha wallet muokotaji akawa hana nia ya wizi ila akashindwa kukufikia (hii ilinitokea Mnazi mmoja nilipigiwa simu na binti akanirudishia wallet yangu).