Tupeane mbinu za kujikinga na wezi kariakoo. Nimechomolewa wallet ina elfu 80/-

Tupeane mbinu za kujikinga na wezi kariakoo. Nimechomolewa wallet ina elfu 80/-

Kitendo cha kuweka wallet mbele tu kinaonyesha ina hela ndio maana unaichunga sana hivyo vibaka watatumia kila mbinu kuifikia.
Ukiwa umebeba hela kwenye wallet yako usionyeshe wasi wasi na kuikagua sana mara kwa mara hii hutoa alert kwa vibaka pia kwamba jamaa ana mali.

Kama umevaa Jeans weka wallet yako mfuko wa nyuma upande wa kulia (hii ni kwa sababu mtu anapotembea mkono wa kulia hautulii hivyo utakua na wakati mzuri kuilinda wallet yako bila watu kujua kwamba unafanya ulinzi).

Hakikisha wallet yako unaiweka kwa upana (usiisimamishe hii hua rahisi kuchomolewa).

Lakini pia kama umesimama kwenye daladala pendelea kuegemeza upande wenye wallet yako kwenye viti vya abiria waliokaa itakua ngumu mtu kukusogeza ili akuibie.

Inakubidi pia kua mchunguzi kujua nani yuko nyuma yako ikiwa umesimama kwenye daladala au mwendo kasi, hii itampa hofu kwa kujua kwamba ulipomuangalia ulimkariri hivyo kitakachotokea utaanza nae matokeo yake kama sio kibaka anakua mlinzi wako tofauti na tabia ya watu wengi ambao akipanda daladala au mwendokasi hana muda wa kuangalia nani yuko nyuma yake.

Mwisho,
pendelea kuweka kijikaratasi chenye utambulisho wako kwenye wallet kama namba za simu na majina kamili, unaweza ukadondosha wallet muokotaji akawa hana nia ya wizi ila akashindwa kukufikia (hii ilinitokea Mnazi mmoja nilipigiwa simu na binti akanirudishia wallet yangu).
 
Kaliakoo hata uwe na panga na bundiki huniibii o level hapo hapo Uhuru mchanganyiko advance hapo hapo Benjamin mkapa high school labda uwe na kifaru
Shule zote ulizosoma hazipo Kariakoo pimbi wewe.
 
Kaliakoo hata uwe na panga na bundiki huniibii o level hapo hapo Uhuru mchanganyiko advance hapo hapo Benjamin mkapa high school labda uwe na kifaru
Mkuu unatutisha sisi wezi sasa nakwambia nitakuibia hapo hapo utaleta mrejesho humu
 
Mi nilinunua nguo vi brauz nilivion vzr kweli pale banana tu ukonga cha ajabu Kila nikichagua nazid kuzion nzuri mno nikanunua mzigo mzima brauzi 45 ivi kwajil ya kuvaa nikatoa pesa kufik home uwez amini brauz zote ni manyalunyalu wakat nilizijalibu afu nikashtuka why nimenunua brauz nying ivi
Jaman watu wachawi sana wanatumia dawa aseeee dah nilijikuta nalia
Hakuna uchawi wala ndumba, ulipigwa chenji kota hiyo.
 
Kaliakoo hata uwe na panga na bundiki huniibii o level hapo hapo Uhuru mchanganyiko advance hapo hapo Benjamin mkapa high school labda uwe na kifaru
Njoo msimbazi utaibiwa tu wenzako walikuwa wanajiona wajanja kama ww tukawaibia ..
 
Usiweke hela kwenye wallet.

Usivae vimodo hivi visuruali vya kubana ndiyo vinafanya wallet ibaki juu na ijichore.

Kama unajijua wewe mtu akikuona tu anaconclude kua ni mshamba pesa weka kwenye begi la mgongoni. Zipu ya ndani.

Epuka muonekano na miondoko ya kishamba.
Hio kwenye begi aweke ndani ya mfuko mdogo labda ila kuweka tu ndani ya begi mbaya haswa msimbazi pale nashuhudia sana watu wakifunguliwa begi na mie nilimdaka mmoja akitaka kunifungulia tena nilimdaka sabb ile njia najua tabia zao nilikuwa onguard muda wote nikitizama side mirror
 
Wezi wanaangalia sura....ukiwa kishambashamba wanakujua na utaibiwa tu! Mimi naweka wallet mfuko wa nyuma na nazunguka kariakoo yote siibiwi.
 
Wewe naye pokea ushauri huo huo..usifike kariakoo. Ukiwa na hitaji huko nitafute nitakuendea kwa niaba yako.

You are welcome.
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] jamanii
 
Mwizi wako alikubana na inawezekana walikuwa wawili mbele na nyuma kwa hiyo wewe ulichukulia ile kubanwa ni kawaida lkn kumbe ndio ilikua chance kwa kaka jambazi
 
Back
Top Bottom