"Vijana wa makamo,kipindi cha pili kinakaribia kuanza "
TUPEANE RAMANI YA ZILE KAZI AMBAZO ZINAZALAULIWA LAKINI ZINAE KIBUNDA
Kwa hizi kazi zifuatazo kutoboa ni fasta tu:
1. Kuokota makopo na chupa za plastic
Hii kazi huitaji mtaji ni nguvu yako na gunia chafu chafu tu.
2. Ombaomba
Hii nayo kutusua ni fasta tu. TAFUTA kijiwe chenye watu wengi; vaa miwani nyeusi tii na nguo chafu chafu.
Weka kopo lako la sadaka na fimbo nyeupe hapo ulipokaa. Mchezo umeisha.
Ukikosa 200k ni bahati mbaya.
3. Anzisha kanisa feki
Hapa ndiyo utapiga pesa za wajinga balaa.
Soma mistari ya bibilia vizuri hasa ile inayosema Mungu ni kila kitu- yaani: ukitaka nyumba, mke/mume mzuri, pesa, gari, etc muombe Mungu
Baada ya ibada Uzia wajinga hao maji, mafuta na hata chumvi ya upako. Kijiko kimoja cha chai bei isipungue elfu kumi.
Baada ya mwezi tu hiyo mihela utakayokuwa umepiga unaitumia kutafuta kiwanja mbweni au masaki ujenge hekalu.
4. Tumia AI Kupiga pesa za wajinga
Hapa ndiyo unapiga pesa za wasomi uchwara.
Tumia AI kuwaandikia watu business plan, theses, resume,....data analyses and interpretation.
Wewe gharama yako ni kuvaa tai, kiatu mchongoko, suruali na shati safi baaasi...mihela itakuja tu.
Ukiona vipi nitafute nikupe michongo ya kupiga hela.
Kwa hapa bongo kuwa masikini ni kujitakia.