Tupeane updates za Ajira za Polisi 2024

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]weka na jina halisi tukujue
 
Sema tu una mbanga mkuu unatupa CHAI isokuwa na sukari
 
living certificate ni kwa ajili ya walio pata zero . hivyo huwa hawana cheti cha form four.. nayo hutolewa na mkuu wa shule hata kabla huja Fanya mtihani wa form four. haitambuliki popote..

hata mimi nilikua naongea kama wewe miaka kadhaa iliyopita na niliamini hivyohivyo ila kuna muda ulifika nikajua kuishi kwenye uhalisia na kuiacha habari ya miujiza yakujifaliji hebu twende na hesabu sikatai kwamba huyo mmoja atakua siyo wewe wala sio kwamba ciujui utofauti baada ya kuingia shida ni kua unaingiaje? chukua hesabu ndogo hapa "ufundi,certificate,diploma na degree zote zilizotajwa Tanzania bara na visiwani hazitazidi jumla ya watu 300 (nakwambia kitu ambacho nimeshuhudia mara nyingi) kama umri unaruhusu kwa Nini usijishushe uanzie kidogo chenye uhakika tena ukikaa miaka mitatu tu unarudi pale ulipostahili tena na ongezeko la daraja, nakuhakikushia endapo unarafiki Yako aliyejishusha kuombea elimu ya chini atamaliza miaka mitatu atabadirika tena kama ni mjanja ahamie dar asome masters kimya kimya open university kwa gharama zake hawatomtiria maanani sana kwa kua wanajua ni elimu ndogo hawezi furukuta akimaliza hiyo masters(mfano sis wa IT unaweza soma hata monotoring and evaluation masters ni mwaka mmoja na huku unasonga na kushika lindo usiku ukiongea vizuri na wakubwa unapangiwa usiku)ukimaliza unawapa masters yako chap unalamba tengo hata kwa kuchelewa muda huo wewe uliyekomaa na kuingilia degree Nafasi zikawa zimeuzwa na ukakaa home utakua na nini?,nakushauri kikubwa ni utimize vigezo hawakupangiii uingilie Nini Moto utauona mwenyewe utakapo kuta rafiki zako wa chuo wapo kweny mafunzo kwa form six utaniamini 😅😅😅
 
tulikua naowengi sana maeneo flani hivi wanaitwagwa baba kanituma utakuta uhakika mwiiiiiingi ngoja wanyiwe hawaonekanagi
Haya wewe kakeshe unasoma ili utoboe 😃😃😃 wakati usaili unataka mbio, kama una mbio basi tukutane CCP
 
Tatizo lako ni hapo unapofikiri mtu akikosa kazi ya Upolisi basi atabaki nyumbani yani ndo maisha yake yataishia hapo 😀😀😀 kwani lazima upolisi? Sijui ndo wewe ulisema umeapply mara 8 ukakosa?kama ni wewe na Kama bado huna mishe nyingine ya kufanya unategemea upolisi basi nikwambie tu Ukweli mchungu inaenda kuwa mara ya Tisa unakosa nafasi! Amini kwamba
 
maana hawa watu wa namna hii hawakawii kuchange from Jeremiah to Fredrick
😂😂😂
Ndo utamu wa Jf huu napost mwenyewe, najitukana mwenyewe, najitetea mwenyewe, najishauri mwenyewe 😃😃😃😃 mambo ya uhalisia pelekeni facebook huku ni mwendo wa kwenda na upepo na kuchangamsha Genge! Niwatoe tu hofu mimi sina connection na mimi pia napambana vile vile na mziki utakuwa mnene haitakuwa rahisi wa connection wapo, wajuaji wapo, wachawi wapo, wazee wa maombi na kukesha kanisi tupo kwahyo show itakuwa kali sana
 
Natamani sana nitaje jina langu na namba zangu kabisa ila bahati mbaya kuna maafande humu isije kesho tukakmiana kisa tu comment ya Jf yenye nia ya kuchangamsha genge mtu akachukulia personal
 
Wakuuu interview fani ya civil engineering maswali yakoje
Kama Ni Bachelor Ya Civil Jiandae Kwa Oral Interview hasa utaulizwa maswali mbalimbali yanayohusu Construction, pia maswali ya Tools mbalimbali za Autocad na jinsi ya kuzitumia....

Pia uwe Na Idea Ya Kutumia AUTOCAD Na Protastructure Maana Mtapewa Mchoro kisha Mchore kwa dakika 10 au zaidi...


All the best Mkuu...
 
CCP Maximum Navyo fahamu Ni 4000 Haizidi Labda Kama Kutakuwa Na Mabadiliko Mengine
 
Salamu Wakuu Kwa Mara Nyingi Interview Za POLISI Huwa Na Siku Shughuli Tofauti tofauti kulingana na ratiba yao huska kwa mfano:

♂️SIKU YA KWANZA: Kujiandikisha Taarifa Zako Binafsi Mfano (Majina/Miaka/Dini)

♂️SIKU YA PILI: Uhakiki Wa Vyeti (Beba Vyeti Vyako Vyote Original, Usisahau Namba Ya NIDA/Kitambulisho)

KUMBUKA: Usiwe Na Hofu Vya Utofauti Wa Majina Ya Vyeti Nenda DO YOUR BEST, Issue Za Vyeti Zote Utazikuta CCP Kule Kuna Ma expert/Wataalamu Wa NIDA Pamoja Na Wanasheria Watashughulikia Changamoto Zote Pale Patakaposhindikana Ndo Mtu Atakatishwa Mafunzo Yake. Kwenye Suala Hili La Uraia Na Uhakiki Na Vyeti JESHI LA POLISI CHUONI Watawasaidia Sana Hadi Kieleweke.


♂️SIKU YA TATU: Ukaguzi Wa Afya (Hakikisha Una Elfu 10 Kwa Ajili Ya Vipimo Mbalimbali)...

KUMBUKA: Mtafanyiwa Ukaguzi wa mwili mzima kuanzia kuvua nguo kwa sekunde 10 na mabao juu kuonesha Mwepesi wako mbele ya askari wa jinsia huska. Mgomo wowote ukiwa ndani ya chumba hautakiwi, maana umeenda kutafuta ajira. Jiandae kukaguliwa tattoo, mshono, marin*** na mengineyo pamoja na upimwaji wa damu.

♂️ SIKU YA NNE: Kufanya Mtihani Pamoja Na Mtihani Ya Practical Kwa Kutumia Laptop/Computer Software Kwa Fani Huska.

KUMBUKA: Maswali Ya Kawaida Sana Usishinde Ukisoma Sana, Uwe Na Idea Ya Fani Yako....

♂️SIKU YA TANO: Usahili Wa Mahojiano

KUMBUKA: Maswali Ni Ya Kawaida Sana Kwa Kuzingatia Fani Yako Lakini Pia Atleast Mfahamu hata RPC Wa Mkoa wako na kamanda wa Wilaya huska, vyeo vya Jeshi La Polisi muhimu kuvijua pia....

✅MENGINEYO:
1. Zingatia Usafi Wa Mwili Na Utakavyovaa
2. Salimia Pindi Ukiitwa Kwa Mahojiano Ama Utakapo Muona Askari/Afande Mbele Ako (Wale Wa Form 6 Waliopitia Jeshini Wananielewa) Kwa Wale Ambao Hawajua Salamu Za Kijeshi Ukimwona Afande Mwambie "JAMBO AFANDE" Atakuelewa Na Kukuitikia

✔️NOTE:
Jitahidi kujibu maswali hata 3 kati ya 5 au zaidi utakayoulizwa, DON'T PANIC RELAX BROTHER/SISTER

ALL THE BEST WAKUU
 
Hizo nguo za mazoezi vijana walizoambiwa waende nazo ni za siku gani?
Kula yao je?
 
System Ya Nguo Za Michezo Imeanza kwa Usaili Wa Mwaka Huu, Miaka Ya Nyuma Haikuwepo System Hii

Vijana Waende Tu Na Nguo Walizoambiwa Maana POLISI Kitu Kidogo Wanaweza Kuwaondoa Kwenye Usaili

Issue Ya Chakula Ni KUJITEGEMEA
Hizo nguo za mazoezi vijana walizoambiwa waende nazo ni za siku gani?
Kula yao je?
 
CHAI CHAI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…