Salamu Wakuu Kwa Mara Nyingi Interview Za POLISI Huwa Na Siku Shughuli Tofauti tofauti kulingana na ratiba yao huska kwa mfano:
♂️SIKU YA KWANZA: Kujiandikisha Taarifa Zako Binafsi Mfano (Majina/Miaka/Dini)
♂️SIKU YA PILI: Uhakiki Wa Vyeti (Beba Vyeti Vyako Vyote Original, Usisahau Namba Ya NIDA/Kitambulisho)
KUMBUKA: Usiwe Na Hofu Vya Utofauti Wa Majina Ya Vyeti Nenda DO YOUR BEST, Issue Za Vyeti Zote Utazikuta CCP Kule Kuna Ma expert/Wataalamu Wa NIDA Pamoja Na Wanasheria Watashughulikia Changamoto Zote Pale Patakaposhindikana Ndo Mtu Atakatishwa Mafunzo Yake. Kwenye Suala Hili La Uraia Na Uhakiki Na Vyeti JESHI LA POLISI CHUONI Watawasaidia Sana Hadi Kieleweke.
♂️SIKU YA TATU: Ukaguzi Wa Afya (Hakikisha Una Elfu 10 Kwa Ajili Ya Vipimo Mbalimbali)...
KUMBUKA: Mtafanyiwa Ukaguzi wa mwili mzima kuanzia kuvua nguo kwa sekunde 10 na mabao juu kuonesha Mwepesi wako mbele ya askari wa jinsia huska. Mgomo wowote ukiwa ndani ya chumba hautakiwi, maana umeenda kutafuta ajira. Jiandae kukaguliwa tattoo, mshono, marin*** na mengineyo pamoja na upimwaji wa damu.
♂️ SIKU YA NNE: Kufanya Mtihani Pamoja Na Mtihani Ya Practical Kwa Kutumia Laptop/Computer Software Kwa Fani Huska.
KUMBUKA: Maswali Ya Kawaida Sana Usishinde Ukisoma Sana, Uwe Na Idea Ya Fani Yako....
♂️SIKU YA TANO: Usahili Wa Mahojiano
KUMBUKA: Maswali Ni Ya Kawaida Sana Kwa Kuzingatia Fani Yako Lakini Pia Atleast Mfahamu hata RPC Wa Mkoa wako na kamanda wa Wilaya huska, vyeo vya Jeshi La Polisi muhimu kuvijua pia....
✅MENGINEYO:
1. Zingatia Usafi Wa Mwili Na Utakavyovaa
2. Salimia Pindi Ukiitwa Kwa Mahojiano Ama Utakapo Muona Askari/Afande Mbele Ako (Wale Wa Form 6 Waliopitia Jeshini Wananielewa) Kwa Wale Ambao Hawajua Salamu Za Kijeshi Ukimwona Afande Mwambie "JAMBO AFANDE" Atakuelewa Na Kukuitikia
✔️NOTE:
Jitahidi kujibu maswali hata 3 kati ya 5 au zaidi utakayoulizwa, DON'T PANIC RELAX BROTHER/SISTER
ALL THE BEST WAKUU