Tupeane Uzoefu: Biashara gani ilikushinda?

Sio biashara hiyo, ila ni ile uonekane tu una biashara!! Pikipiki mpya kwa sasa hadi 2.5 milioni, unampa mtu kwa mkataba wa mwaka ambapo kila siku atakuletea 10,000,kwa mwezi ni 300,000 kwa mwaka ni3. 6 milioni, faida hapo ni kama 1.1 milioni, na sio rahisi kuipata pesa yotekwa mwezibila longo longo, ukitafuta faida halisi hapo kwa mwezi ni kama 100,000/!!!!!!bado wasiwasi wa kuibiwa.
 
Nina shida na ule mchele ulionyooka kama wa Kamsamba
Naweza kupata?
Daaaa!! Kamsamba, umenikumbusha mbali sana, mwaka jana nilikuwa huko, ila daa kutoka hapo mlowo kuitafuta Kamsamba ni shughuri pevu, hizo km 132!! Sio mchezo na kuna poli zito kuna sehemu inaitwa) BOT), kuna kona kali majambazi ndio huwasubilia wafanyabishara na kuwapola pesa!

kiukweli kule kuna mchele mzuri ila kuna sehemu inaitwa MAJIMOTO, ipo mkoa wa katavi(mlele) kule ndio balaa, ni sindano mchele wa kule, na unaweza tokea hapo hapo Kamsamba hadi kule. Nilikuwa kwenye utafiti wa biashara hiyo hiyo ya mchele.
 
Katika changamoto, point yako ya pili imeweka huu mjadala vizuri

Kwa jinsi mjadala ulivyokuwa unaenda karibu kila biashara inaonekana ni ngumu, kumbe inategemeaana na mwenye biashara

Wewe uliiwezea biashara ya Bar, mwenzako katika eneo hilo hilo akafeli

Moise Aimar,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka nikiwa darasa la nne, nilifanyiwa sherehe ya komunyo ya kwanza, zawdi zilitafunwa na wazee ila kuna kiasi kilibaki mfukoni kama elfu 5 hivi, nikaenda dukani kwa mangi nikanunua ile pump ya baiskeli yenye kitank kidogo, kisha nikaandika matangazo kuwa tunajaza upepo wa baiskeli kwa sh. 20.

Biashara haikwenda kama nilivyotaraji, watu walikua wanakuja ila walikua wanaomba kujaza bure, chakushukuru ni ile pump ilikuja kunisaidia sana kwenye kujaza baiskeli yetu ya Avon iliyokua inatumika kubebea chakula cha nguruwe alimaarufu kama pollad.
 
Huu uzi wa kukatishana Tamaa 🤣🤣🤣🤣🤣 Yani kila story inaonesha biashara fulani haifai ila cha kushangaza hizo biashara watu wengine wanazifanya na zinaenda freshi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
LadyRed,
muda unaendelea kwenda,usisahau hilo

2021 ikifika fx ikawa useless tena utakua

umepoteza miaka mingine so jaribu kutumia

muda uliopo kufanya vitu zaidi ya viwili incase

kimoja kikawa hakina maana hivi vingine viweke sawa

na kurudisha hasara zilizopatikana,usi deal na kitu ki 1.
 
Najaribu kukuelewa lakini wapi, yani biashara ni pasua kichwa, hapo hapo inalipa vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CONTROLA,
Soko la forex sio la kufa leo wala kesho
Labda mataifa yaache kufanya biashara na kutembeleana
 

'Kupata japo laki kwa siku kama kipato cha ziada sio Kesiii...'

Daah yaani laki kwa siku unaiongelea kirahisi rahisi kabisa,daah.

dodge
 
'Kupata japo laki kwa siku kama kipato cha ziada sio Kesiii...'

Daah yaani laki kwa siku unaiongelea kirahisi rahisi kabisa,daah.

dodge
Kuiongea rahisi sana
Kuipata sasa hahaha
Lazma usote
 
Biashara ya Taxi na Bajaj ni pasua, kuliko mnavyofikiria. Mafundi, Traffic, Madereva then wewe Mmiliki unakula makombo yatakayobakia Mungu akipenda.

Bajaj mpya, dreva analewa Bar na Totoz za kutosha, anagawa chombo"Deiwaka " hesabu hadi kugombana, mafundi wezi hawatengenezi vifaa, traffic nusu wanifunge, nao wamegawana Gari na Bajaj zangu wanakula hesabu kwa madreva.

Utasikia yule traffic usipompoza Boss, wanasumbua sana.

Niliuza vyote, nimenunua viwanja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…