Tupeane uzoefu: Siku yako ya kwanza kununua gari ilikuwaje?

Sijawahi kumiliki gari uchumi hauniruhusu ila nikiwa nasoma nilinunuliwa baiskel na shangazi usiku naiingiza chumbani kwangu naifunika shuka
Siku nikinunua gari ntailaza ndani mi ndo nilale nje
Hahahahaha Kama baskeli tu hvyo gari itakuwa balaa.
 
Hata tulionunuliwa tuchangie?

Mimi siku ya kwanza kumiliki usafiri wangu haikunisumbua maana kabla ya hapo nilikuwa nimeshazoea magari ya kugongea.

Ila nilichojitahidi ni kuhakikisha kila mtu anajua lile ni langu na sio kwenye harakati za kugongea.
Ulifanya nini mpaka ukanunuliwa gari
 
Na mimi nililifunga alarm ilikuwa inasumbua kweli si usiku si mchina maana eneo nililokuwa naishi kulikuwa na watoto wakipita wanaligusagusa linapiga kelele. Nilipozoea nikaona alarm upimbi nikayachomoa kwanza yanaharibu betri.

Halafu baada ya kulizoea likawa gari la masela kila mwenye kutaka nampa hadi wakalipiga na mzinga kabisa lakini hapo lishakongoroka kinoma ndani ya mua mfupi.

Nikaliuza kwa hasara na kununua lingine hapo nilikuwa nishajifunza sitaki mtu aje kuazima.
 
Mimi nina guta langu, kila jumapili navaa kofia yangu ya mkeka na tshirt ya Voda naingia viwanja, nikifika kilabuni nadrift wazee wanapiga miluzi na wanawake wanapiga vigelegele.

Nikifika kilabuni nafunga guta langu na lock halafu naning'iniza funguo kwenye pensi langu la jeans.

Hapa nasubiri saa 10 ifike nikanywe mbege na ulanzi.
 
Duh hilikuwa balaa
Ilikuwa zaidi ya balaa mkuu, siku ya tatu nipata ajali pale science nikiwa nimekutana na mtu anatoka tegeta anaenda magomeni kama kawaida panda nikupeleke, ile tumesimama mataa katoka jamaa huko speed alikuwa ana jimama kwenye gari sijui linamnyonya utami ukazidi akambamiza aliyekuwa nyuma yangu naye akaserereka na kunibamiza mimi.
 
M nakumbuka nilivyonunua cmu nilikuwa cpati ucngiz nakijiona mm niwa juu sana,mwishowe ikaibiwa ,nikapata funzo ishi kawaida na Si kujionyesha.
 
Mimi nlinunua gari nkiwa bado nakaa hom,so nikawa namuachia binamu wangu nalo ili hom wasijue mana nlikutana na biashara flani ya ujanja nikapiga 2.7m kwa mnyarwanda flani hakua raia istoshe demu wake ndio alinipa mchongo huo...nkanunua toyota carib hiyo ni 1999..ila hiyo gari binamu alinidhulumu mana alijua siwezi kumshtaki popote
 
Kawaida tuuuu,kwanza niliipiga tinted kaliii nisionekane,nilikuwa napaki mtaa wa pili na ofisini natembea mpaka ofisini baada ya miezi 4 watu kujua ofisini ndo nikawa na confidence ya kwendanayo!

!ila nilinunia kwa ajili ya ya issue za shule na ofisi kurahisisha maisha maana nilikuwa nachoka ana kutoka ofisini kudandia madlaladala kwenda chuoni etc,ila sikuwehuka ww tunaelewa ushajisema msukuma hatushangai!
 
Sijawahi kumiliki gari uchumi hauniruhusu ila nikiwa nasoma nilinunuliwa baiskel na shangazi usiku naiingiza chumbani kwangu naifunika shuka
Siku nikinunua gari ntailaza ndani mi ndo nilale nje
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wagongeaji tupo pamoja T...DVB [emoji1614]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…