Tupeane uzoefu: Siku yako ya kwanza kununua gari ilikuwaje?

Eh siku iyo mzee mbaba ile natoa tu chombo kwa agent, nikaipeleka pale kwa dick sound migomigo sijui bado yupo palee

Basi nikaweka miguu mipyaaa na sport rim kali + mziki wa kibabe natoka pale sijui saa 3 usiku nafika ubungo mataa (enzi izo interchange bado ) niko ktk lane ya kuelekea kimara basi kuna daladala ilikuwa inatoka ubungo maziwa kule kujifanya anapenya penya akaigusa chombooo aiseee nilikiwasha pale fasta nilivyo shuka nikachukua funguo ya ile daladala

Ilikuwa vagaaa tukaita trafik kupima ajali ila ajabu sasa ile daladala ilikuwa imeigusa kidogo tu ile chombo Harrier tako la nyani ila nikawachomoa 250k


Aiseee usichezeee chombo ikiwa mpyaaaaa
 
Fanya yoote ila avoid kuazimisha mtu gar ambae si ndugu yako wa damu.. utakuja lia mzee.. mim nilikua na kagar kangu fulan hiv aisee.. kuna bwege mmoja tumeenda club tuko ndan akanambia bro naomba funguo nikachukue pombe kwenye gar et aliiacha nyag yake.. nikampa kumbe alikua na plan za kusepa na gar.. af alikua kalewa flan.. akachkua kaenda nayo sinza kutoka posta.. akala mzinga ku.ma ma.ke.. had leo sjamsamehe na urafik uliisha... Mnduku kabisa yule bwege .. na alikua best friend
 
🤣🤣🤣Pole sana ndugu, hata mimi aliyekipiga mzinga alikuwa rafiki yangu na alinifanyia umafia ambao sikutegemea.
Gari kalipiga mzinga kalirudsha kalipaki likiwa ovyo na kakana kabisa kuwa kalichukua hivyo. Yani kilichoniuma sio kuharibika gari maana nilikuwa najua hana uwezo wa kulipa au kurekebisha, ila kukana yani sijui alinichukuliaje.
Toka kipindi hicho things between us have never been the same again.
 
Nasoma comments maana hata ndoto ya baiskeli Sina
 
Uko darasa la ngapi sasa hivi?
 
Dah nakumbuka mchuma wangu wa kwanza kumilikishwa aseee nilivuta route ya ufunguzi Arusha to Dar baada ya hapo ilikuwa hadi safari fupi za ndani ya 4km lazima niende na mali yangu but ilinichukua mwezi kuondokana na ile hali
 
Me ninalo muda tu, ila hadi leo watu wanahisi kama nimeazima au kuna mtu kanipa bure, na nilipo nunua kuna baadhi ya watu wanao nijua ilipita miezi mitatu hawajui kama nina gari...
Kwasabab naishi maisha simple sana nikiamua natembea kwa miguu hasa jioni nikitoka kazin naweza kutoka home hadi mjini kwa miguu, siku nyingine naenda kazini na daladala watu huniuliza gari iko wapi nawaambia ipo home sina hela ya mafuta 😂😅 maana ndio majungu ya watu wakikuona upo kwa miguu watakujadili hana hela kanunua gari ona kakosa mafuta...
Naishi maisha simple baada ya kujifunza kutoka kwa mzee wangu na babu yangu, walikua na magari ila waliishi life style ile ile ya mwanzo Kutembea kwa miguu, kusalimia watu, kutembelea watu, kufanya kazi ndogo ndogo za nyumban na kijamii... Hata nyakat ambazo walikua wameishiwa pesa watu hawakujua kabisa. Waliona ni kawaida yao kuishi simple...
Kuna watu wanasema kumiliki gari ni gharama kubwa 😅😂 namilik gari ya cc 2000 kwa mwezi nikilitumia effectively naweka mafuta ya elfu80 tu. Service ni hizi za kawaida kumwaga oil na kuongeza coolant ambazo nafanya maybe kila baada ya miezi 4-6. GARI IKIWA MPYA AU KTK HALI NZURI UTAKAA NAYO HATA MIAKA 10 HAIJAKUTIA HASARA YA SERVICE ZAIDI YA LAKI 5 KWA MWAKA.
NUNUA GARI ACHA UOGA WA MAISHA, NYUMBA ZIPO TU
 
Ebhana siku ya kwanza navuta kausafiri kangu kwanza nilikua na furaha sana jamaa yangu ndio alinipeleka home japo nilikua najua kuendesha kitambo ila nilitamani aniendeshe niiskilize gari sikuwasha redio wala ac. Nakumbuka nilikua naamka usiku nawasha gari naenda mpka karibu na bagamoyo alafu nageuza ilimradi nifurahishe nafsi yangu.

Nakumbuka nilishasemwa sana kipindi hicho ulitokea msiba kijijini nikasepa mwenyewe usiku watu wananitafuta nawaambia nipo milimani muda mrefu wanahoji kwann uende mwenyewe nikabaki nacheka tu.

Kilabmtu naamini ana kaushamba kake ila mimi nilijitahidi kujificha japo kuna muda hata ofisini nilikua naenda kukojoa ilimradi nikitoka nje nione gari yangu. Haikua rahisi ila kile kipindi kilipita salama nashukuru hakuna alieniona limbukeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…