Changamoto hazifanani, chamsingi ni kuwa na subira. Kila biashara/uwekezaji una changamoto zake. Hivi walionunua hisa za TOL wamewahi pata gawio?Safi na hongera kwa juhudi, muhimu umejua tatizo na umejipanga kwa asiyejua tatizo bado ni changamoto kubwa kwake.
Naam,Hongera sana, naona mambo ya fedha yamekunyookea mpaka kufanya uwekezaji huu.
Mimi nimesitisha shughuli zangu zote na sasa nipo kwenye kilimo mazima 100%. Kuna potential kubwa sana huku iwapo utapata access ya masoko na bei za uhakika. Njombe, iringa, mbeya neema imefunguka tushindwe wenyewe
Karibu sana njombe, utatukuta tunalima parachichi na kuotesha miti ya mbao.Safi sana, najiandaa kuzama njombe
Jirani yangu alikuwa na madeni sugu, vijana wakalipa kisasi kwa kuchoma moto bila kuzingatia kuwa tutakaopata hasara ni wengi. Zaidi ya eka 5000 ziliteketea kule Mgala njombe.Pole sana mdau moto ulitokana na nini?
Nilipoamua kuingia kwenye hii game nilianza na eka moja na nusu kule Kilolo, Mheshimiwa Mbunge Mwamoto alinipa msaada mpaka kufika kile kijiji na nikapata shamba eka moja na nusu kwa Tsh 22,000/.Uwekezaji wa miti ni rahisi sio mpaka uwe na milion 500 pata ardhi Hata kama ni haka 2 anza Utapata hamu na uzoefu a long the way. Lakini usipoamua kuanza kwa kusikiliza wakatisha tamaa kwa excuses mbalimbali. Alafu usisikilize watu ambao wanatoa ushuuda wa watu wengine. Ongea na wasikilize waliokwenye game (hii ni katika venture yoyote ile. Get started kwenye maisha hamna kuchelewa ukikumbuka umewahi
Hapo nimekusoma vema.Naam,
Fedha inatokana na shughuli yenyewe. Huwa naanda vitalu vya miche, nauza miche mingi, faida nanunulia mashamba na kuendeleza, kwa hiyo ni uwekezaji unaojiendesha wenyewe. mwanzo nilikuwa nanunua vimisitu vidogo nafuga, akija mteja napiga bei, kwa hiyo vikaniinua sana. Huku nina miche na kule kamsitu kamepata mteja, basi siku zinasonga.
Niko njombe pia napiga parachichi. Nimeangukia pua mara mbili kwenye parachichi, yaaani miche ilikufa sana. Nikagundua miche ya bei rahisi ni hasara. Sasa hivi natumia miche ya bei mbaya, haifi.
Kule Lutukira niliangukia pua kwenye Tangawizi, ile namalizia camping, bei ikashuka vibaya nikaondoka fasta.
Mgala, ihanga ni wahuni sana wale halafu matapeli sana, ardhi hawana walishawauzia wageni sasa hivi ni migogoro tupu huko wamebaki kuuza mashamba waliyouza miaka mingi iliyopita. Shamba moja linauzwa mara 5.Jirani yangu alikuwa na madeni sugu, vijana wakalipa kisasi kwa kuchoma moto bila kuzingatia kuwa tutakaopata hasara ni wengi. Zaidi ya eka 5000 ziliteketea kule Mgala njombe.
Aisee[emoji22][emoji22][emoji22][emoji22][emoji24]Jirani yangu alikuwa na madeni sugu, vijana wakalipa kisasi kwa kuchoma moto bila kuzingatia kuwa tutakaopata hasara ni wengi. Zaidi ya eka 5000 ziliteketea kule Mgala njombe.
Changamoto hazifanani, chamsingi ni kuwa na subira. Kila biashara/uwekezaji una changamoto zake. Hivi walionunua hisa za TOL wamewahi pata gawio?
Hii inategemeana na unapoishi. Hiyo bei ni miti ya IringaUwekezaji wa miti kwangu mimi hauna tija, unahudumia shamba miaka zaidi ya 10 halafu unakuja kuuza mti kwa sh 20,000 na unapoukata inabidi upande mwingine na kuja kuvuna tena miaka 10 ijayo so elfu 40 kwa miaka 20.
Fanya kilimo cha miti ya matunda hutajuta mfano mchungwa mmoja hata ukiuza chungwa 300 kwa sh 50 = 15000 so kwa miaka 10 = 15,000*7= 105,000/=
Ku prone, kuna watu wengi wanataka kuni mkuu, kwanini kwako iwe gharamaUnatakiwa kufanya palizi angalau mara 2 kwa mwaka (Kuna kuchomeana mashamba) na miti ikue vizuri, pia Kuna pruning kila mwaka bei inategemea mahali ulipo. Jumla palizi 30 kwa miaka 15
Kuhudumia shamba kwa miaka 15 bila kuingiza hata shilingi ni rubbish. Mfano njombe/iringa shamba la miti yenye miaka 7 na ardhi wanauza 3-6m, miaka 3-4 laki 5-7
hapo kwenye global gap hapo,Hapo nimekusoma vema.
Tupo pamoja pande hizi.. nafanya organic farming soko ni nje nje na wanunuzi wa nje wanazidi kuongezeka na bei inapanda vizuri, lengo ni kuwauzia wanaoexport Europe.
Avocado nadeal na rungwe avocado kwasababu wao ni global gap certified na seedlings nachukua kwao sababu pia ni global gap certified, nami pia wamenicertify, export market ya Europe inaangalia kuanzia historia ya mche, ukuzaji mpaka uvunaji pia ni lazima ufanye organic farming japo ni gharama sana.
Miche ya mtaani ni ya kuepuka wengi wanaangamia na wanazidi kupotea, huku wanachojua wao avocado ni deal basi mradi mche uwe grafted wanajibebea tu na kupanda mwisho wa siku kwenye kuuza wanabaki kushangaa mzungu amekuja kuvuna na semi shambani kwangu huku mimi nakunywa kahawa chini ya mti nasubiri amalize tupime kilo nipate milioni zangu
Hii inategemeana na unapoishi. Hiyo bei ni miti ya Iringa
Kuna sehemu, kuna miti inaitwa mburumatare (sijui hili jina ni common maeneo yote au laa), hii miti baada ya miaka 5 unavuna na mti mmoja unauza kati ya Tsh 50-70 elfu. Hapo bado unabaki na mabanzi na kuni ambazo pia unaweza kuziuza. Hivyo hiyo biashara si kichaa kama wengine wanavyodhani
Uzuri wa hiyo miti, ukikata, unachipuka mwingine ambao Baada ya miaka 5 mwingine unaweza kuuza tena kwa kati ya Tsh 50-70
Wazo la kupanda miti ya matunda pia ni wazo zuri, kwani ukipanda miti ya matunda ya asili kama miparachichi unaweza kuvuna hata kwa miaka 10 (mazao yakiwa mengi katika peak yake)
Uzuri wa biashara ya miti, ukipanda ikikaa ndani ya miaka 2 bila kusumbuliwa, unaendelea na mambo mengine huku shamba lako likiendelea kukutengenezea utajiri
Sijapotea,
Nipo sana, na Mungu jalia nitaendelea kuotesha miti zaidi. Kama nilivyosema 2019 nimeotesha pines 150,000 sio za watoto ni zangu mwenyewe mkuu. Baada ya anguko la uchumi tumebaki wachache sana kama tulivyoanza. Idadi inapungua sana ila mimi na wenzangu tuliopinda bado tunaweka vitalu vya miche.
Tunapoona matajiri wa Kiarabu na Kihindi katika nchi yetu, ujue misingi yao ilijengwa muda mrefu sana na waliowatangulia. Fuatilia wote utaona. Natamani uwekezaji wangu uje kukivusha kizazi chang kwenda level nyingine kabisa.
Hiyo miti nadhani inaweza kuota sehemu yoyote ambayo miti ya miarubaini inaota (kwa mtazamo wangu) maana kila kitu ni kama miarabainiNi sehemu Gani hiyo ambako hii miti inapandwa?
Jirani yangu alikuwa na madeni sugu, vijana wakalipa kisasi kwa kuchoma moto bila kuzingatia kuwa tutakaopata hasara ni wengi. Zaidi ya eka 5000 ziliteketea kule Mgala njombe.
Hongera mkuu.. ukiwa na kipato cha uhakika ni uwekezaji mzuri sana.Uko vizuri,
Nilipokuwa chuo, niliotesha miti 250 tu nyumbani kwetu, sasa hivi nasumbuliwa mno. Nimewaambia ile nimeiacha kwa ajili ya dharula maana ni hela kiganjani sio benki ukute ni jumamosi hawafungui, yaani nikiinua simu tu, mpunga ndani maana ndo imebaki hiyo tu iliyokomaa. Kila siku Wachina wa Mafinga wanapitia vimisitu vyetu kupitia madalali wao, nasema bado sana. Jirani yangu juzi kavuta mpunga wa maana pale Mapanda, kauza kwa mchina vigogo, miye bado kwanza.