Kuna msemo wa kiingereza unasema "Managers are hired to be fired". Yaani Makocha wameajiriwa kwaajili ya kufukuzwa.
Kocha unapopewa timu, watu wanachotaka ni mafanikio tu na si kingine. Msimu mpya umeanza na kasi, kuna makocha kadha wa kadha hali za timu zao si nzuri sana hivyo kupelekea kuwa katika hatari ya kufukuzwa vibarua vyao.
Tukumbushane makocha ambao wamekalia kuti kavu kwenye timu zao, yaani muda wowote ule vibarua vinaweza kuota nyasi.
Mimi naanza na huyu Marco Silva wa Everton...
View attachment 1224462View attachment 1224463