Tupia jina la kocha wa timu yoyote anayekaribia kufukuzwa kazi

Hawa Milan sijui wanakwama wapi miaka hii Timu yangu,au ukata unawazingua?
Mwanzoni timu ilivyokuwa chini ya Silvio Barluscon ukata ilikuwa ni sababu kubwa ya timu kuyumba hasa baada ya asilimia zaidi ya 80 ya kizazi kilichoipatia ac milan mafanikio, umri wao kuwa mkubwa na kupelekea kustafu kuichezea ac milan.

Barluscon akaiuza timu kwa wawekezaji lakini tokea timu imeuzwa hakuna mafanikio yoyote waliopata zaidi ya kufanya matumizi makubwa ya pesa isiyoleta matokeo chanya.

Tatizo la Ac milan ni uongozi kwasasa, wanafanya mambo kwa kubahatisha tu, wanaokoteza okoteza makocha wasiokuwa na cv kubwa mwisho wa siku wanatimua timua tu makocha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…