tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Katika shule/chuo hakosekani mwalimu msumbufu na ambaye huwafuatilia sana wanafunzi hata ktk mambo madogo madogo na kuwapa adhabu za ajabu ajabu.
Leo nataka tuwakumbuke walimu hawa pamoja na kujikumbusha vituko walivyowahi kuvifanya.
Mimi shuleni kwetu Mara Sekondari kulikuwa na mwalimu mmoja aliyeitwa Jigge. Basi siku moja kuna wanafunzi walitoroka kwenda mjini bila ruhusa. Na kibaya zaidi, walipokuwa huko mjini wakafanya fujo na kuharibu mali za wananchi.
Taarifa zao zikafika shuleni. Ilikuwa jioni na kiza kilikuwa kimeanza kukolea. Mwalimu Jigge akapiga kengere. Wanafunzi wote tuliokuwepo shuleni tukakusanyika bwaloni na akaanza kuchuka roll call.
Ili kumkomesha mwalimu huyu, pamoja na kuwanusuru wale wanafunzi 'wahalifu' waliokuwa wamefanya tukio mjini, wanafunzi wakapanga kuzima umeme main switch na kumpopoa kwa mawe. Ghafla tu, umeme ulipozimika, mwalimu alichomoka kama mshale na kutokomea kizani. Wanafunzi walimtupia mawe lakini, kwa ile speed aliyochomoka, hakuna jiwe lililompata. Ana bahati sana.