Mwalimu Mgimwa--Mkwawa High School. Huyu mwalimu alikuwa discipline master. Ni kimwalimu fulani kimbilikimo hivi--kifupifupi. Lakini hiyo shughuli yake ilikuwa baraaaa!
Basi siku moja, kiMgimwa na na Mwalimu mmoja wa Maths anaitwa Mwaipaja, akaamua kuzama eneo moja linaitwa Makanyagio--hapa ndipo wanafunzi watoro walipokuwa wakienda kujificha wakinywa pombe moja ya Kihehe inaitwa ULANZI.
Basi siku hiyo Mgimwa na swahiba wake Mwaipaja (huyu naye alikuwa mnoko sana) wakaamua kuzama huko Mkanyagio na kuwaibua hao 'wahalifu' wakinywa ulanzi. Wakakamatwa wazima wazima, na kuswagwa kama kondoo hadi assembly ground. Walichapwaje!!!!!!!!!!!!!! Walichapwa mpaka wakajuta kusoma shule. Chezea Mgimwa wewe!