Fujo gani mkuu? Wanafunzi walilipiza?
Nakumbuka Mara Sec kulikuwa na mwalimu mmoja mtata sana. Sasa kabla ya kuingia darasani wanafunzi wakamtega kwa kutumia kiti kilichovunjika.......wakakiungaunga na kukiweka mbele ya meza ya mwalimu. Basi teacher alipokuja kukalia kile kiti kikampiga mweleka nyeti zote zikakaa uchi. Mara moja aligundua kwamba ametegwa na kuwaomba wanafunzi wamtaje aliyefanya mtego ule lakini darasa lilionyesha solidarity ya kufa mtu.....no kutaja mtu.
Kuona vile, teacher akawarepoti wanafunzi kwa mwalimu wa nidhamu; wakala mboko kama zote na kuchimbishwa shimo la maji taka kwa wiki nzima bila kuingia darasani. Ilikuwa balaa unaambiwa, usipime!!!