Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Mwl. Kimaro na Mwl. Palangyo, dadeq hawa wamama walikuwa balaa la kufa mtu.
 
Mwl Nyankulumbwe Mnyangalandimbwi , sitamsahau huyu ticha kwa mistick yake [emoji4]
 
Mwl Nyankulumbwe Mnyangalandimbwi , sitamsahau huyu ticha kwa mistick yake [emoji4]
Kama ulikua unajaribu kulitamka hili jina na umejing'ata ulimi, utanisameh bure. Halikua lengo langu
 
Mwanza sec kulikuwa na ki discipline master hicho pambaffff kabisa
kilikuwa kinanikera yani kuwa discipline anajiona kama vile afisa elimu
namchukia hadi kesho alikuwa na unoko wa kifamba sana
anaitwa mkumbo
Naona umeamua kunitangaza mbele ya hadhara
 
Mapinduzi PS..... alikuwa wa kuitwa Kiyumbi...mzee wa fegi, anakwambia naitwa kiyumbi wa kuyumba, sivuti bangi ni kasport tu
 
yani nakumbuka Ashira kulikuwa na mwalimu wa kike anaitwa mwalimu Mbele anasura ngumuje sasa alikuwa hapendi watu kuvumisha chakula dom na wadada weng wanapenda kwenda kulia dom akikukamata yani hafu alikuwa ana roho ngumu

kuna siku marafki zangu walivusha uji kila mtu ana chupa mbili aliwaambia wanywe wote na haukuwa na sukari yani chuoni sasa kulikuwa kuna Dr anaitwa Saanane alikuwa anafundisha proposal ni mkali unaenda kupresent unatetemeka mpaka basi Dr yule alinipa pressure hadi semister inaisha ckuamini aise kila mtu alikuwa ana mwogape
Du unoko wa huyu mwalimu ulikuwa unasadifu roho yake aisee!! 😀 😀 😀
 
Katika shule/chuo hakosekani mwalimu msumbufu na ambaye huwafuatilia sana wanafunzi hata ktk mambo madogo madogo na kuwapa adhabu za ajabu ajabu.

Leo nataka tuwakumbuke walimu hawa pamoja na kujikumbusha vituko walivyowahi kuvifanya.

Mimi shuleni kwetu Mara Sekondari kulikuwa na mwalimu mmoja aliyeitwa Jigge. Basi siku moja kuna wanafunzi walitoroka kwenda mjini bila ruhusa. Na kibaya zaidi, walipokuwa huko mjini wakafanya fujo na kuharibu mali za wananchi.

Taarifa zao zikafika shuleni. Ilikuwa jioni na kiza kilikuwa kimeanza kukolea. Mwalimu Jigge akapiga kengere. Wanafunzi wote tuliokuwepo shuleni tukakusanyika bwaloni na akaanza kuchuka roll call.

Ili kumkomesha mwalimu huyu, pamoja na kuwanusuru wale wanafunzi 'wahalifu' waliokuwa wamefanya tukio mjini, wanafunzi wakapanga kuzima umeme main switch na kumpopoa kwa mawe. Ghafla tu, umeme ulipozimika, mwalimu alichomoka kama mshale na kutokomea kizani. Wanafunzi walimtupia mawe lakini, kwa ile speed aliyochomoka, hakuna jiwe lililompata. Ana bahati sana.
Mazengo sekondari enzi za headmaster Silvester Mkoba palikuwa na second headmaster mnoko kweli kwa jina la Msasa akisaidiwa na mnoko mwingine alijulikana kwa jina la Mkwizu.
Ila S. Mkoba alikuwa mtu poa sana na humble person.
Wahenga mliopita Mazengo kule Dodoma mnawakumbuka hawa watu?
 
Back
Top Bottom