Tuliosoma Ligula primary, Mtwara mtakuwa mnamkumbuka Mwl Mayelle, ticha wa hesabu.
Dadekiii.
Dah....yaani mpaka namaliza la saba naenda sekondary nilikuwa bado namuogopa
Mwl alikuwa anapiga yule, sipati kusema jamani
Siku akichoka kupiga, anakukabidhi mbegu za ufuta, anakuonyesha eneo la kupanda, anakwambia tutakutana term ya mavuno.
Term ya mavuno ifike afu hakuna kitu au mazao hahajakomaa....utajinyea.
Ila atakuwa keshakuwa mtu mzima...hana nguvu tena.
Ila tuliosoma Ligula akina Konrani Mmuni, Asha Van Vandame, David Chinguile.mmekula sana bakora zake na hivo mlikuwa watundu.