Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Juma Pius Matandula Singer email Secondary School. Huyu akiwa zamu akikuta wanafunzi watapiga kelele aliwapeleka staffroom mbele na kuwapigisha magoti akija hmaster akawarudisha darasani na yeye akirudi asiwakute alikuwa anazira na kwenda Kwake mpk mkuu aende kumbembeleza
 
Tuliosoma Ligula primary, Mtwara mtakuwa mnamkumbuka Mwl Mayelle, ticha wa hesabu.
Dadekiii.
Dah....yaani mpaka namaliza la saba naenda sekondary nilikuwa bado namuogopa
Mwl alikuwa anapiga yule, sipati kusema jamani
Siku akichoka kupiga, anakukabidhi mbegu za ufuta, anakuonyesha eneo la kupanda, anakwambia tutakutana term ya mavuno.
Term ya mavuno ifike afu hakuna kitu au mazao hahajakomaa....utajinyea.
Ila atakuwa keshakuwa mtu mzima...hana nguvu tena.

Ila tuliosoma Ligula akina Konrani Mmuni, Asha Van Vandame, David Chinguile.mmekula sana bakora zake na hivo mlikuwa watundu.
 
Ile adhabu ilikuwa too much mkuu, kumbe unampata vizuri sana.
Yeah...niliiona picha yake kwenye gazeti la Majira akiwa kasimama juu ya mgongo wa mwanafunzi. Hazikupita siku nyingi nikasikia amefukuzwa kazi kwa kitendo kile. Jigge alikuwa mwalimu wangu....ni mwalimu mzuri sana wa English, akiwa miongoni mwa walimu waliosomeshwa Uingereza katika chuo kikuu cha Plymouth.
 
Du ee bwana eeh, huyu alikuwa komesha!
 
Jige alienda Mwanza ,Hilcrest baadae Thaqaffa
hahahaha! unamkumbuka mwal bagile?
 
Morega Mongate kanifundisha Adv.Maths hahahahaaaaa and lafudhi yake iyo utachoka mwenyewe
 
Tulikua tunaiita "Jamahuri ya Watu wa Tech " enzi hizo
 
Nimecheka sana ha ha haaa
 
Hakuna shule yenye walimu wakali kama jitegemee wakikushindwa wanakusakizia wanajeshi ambao ndio kama walezi na wenye shule. Wengi mmeongea lakini hakuna shule inayogusa pale kwa walimu na walezi wakali.
Ndyamkama yule ticha mwache tu ukiingia kumi na nane zake umeisha, halafu kuna Afande anaitwa Ismail. Huyo akikushika kantini kama ulichelewesha muda wa kurudi basi unapigwa bakora A maana kisha unaambiwa uite mzazi. Mzazi akija anaambiwa mwanao unampa hela nyingi za kutumia hadi anahonga madem ndiyo maana anachelewa kutoka breki.
 
Nashangaa sijamwona BAROSHA na MARWA mzee wa makofi TABORA BOYS sitowasau hawa jamaa, kuna kengine kalikuwa kanoko kanafata bendera kalikuwa kanaitwa nyasebwa.
 
mwalimu Mwangoka, baba Kadoda, Masato, Mwaipaja wa mkwawa complex and casino iringa, sitawasahau hawa viumbe
 
Mwaka gani mkuu?kanifundisha pia,ila baada ya utoto nilimpenda,katufaulisha wengi.
2004 mkuu enzi ya kina soko, nondo na akina mbaga na yule jamaaa aliyekunywa aliyemeza bangi kisha akanywa mkojo mbele ya gadiye kufuta ushahidi [emoji2] [emoji2]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…