Tupia jina lako la utani na sababu ya kuitwa jina hilo

Tupia jina lako la utani na sababu ya kuitwa jina hilo

yuzazifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2018
Posts
5,108
Reaction score
9,436
Natumai hamjambo wakuu,

Karibu kila mmoja wetu hupatiwa jina la utani na familia/jamii inayomzunguka kulingana na tabia/matendo yake, karibuni hapa kushare majina yenu ya utani na sababu ya kuitwa majina hayo.

Binafsi jina la utani niliitwa bwana MISOSI sababu nilikua napenda sana kula, jina hili lilivuma sana hasa utotoni maana nilikua sijui kujivunga linapokuja suala la msosi, yaani popote nilipoukuta nilikula bt after kukua tabia imetoweka na hata sijui ilitowekaje japo kwa wanaonijua huendelea kuniita bwana MISOSI.

Sasa uwanja ni wenu kutiririka.
 
Dah! Mtaani mi nilikuwa naitwa majina mengi sana la kwanza nilikuwa naitwa jini kabula😂🤣 kwa sababu ya urefu wangu! So lingine ni Mnywa viroba 🙄😖kipindi kile ndo vimetoka toka kinaitwa kiroba 🤦🤪🏃.
 
Yaani nina nicknames nyingi nikizitaja simalizi[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom