Tupia jina lako la utani na sababu ya kuitwa jina hilo

Tupia jina lako la utani na sababu ya kuitwa jina hilo

Hahaaa ila nmekumbuka kipindi cha nyuma baba yangu alikua anapenda sana kuniita mkungumuya, half too bad hata sikuwahigi kumuuliza maana yake ni nini so hata sikujua lina maana gani.
we mrembo jitokeze, wakalimani washatupa tafsiri ya mkungumuya
 
Cindelela, niliitwa na wanafunzi wangu enzi nafundisha nilistukia naitwa madam cindy.nishatokaga huko ila bado jina lipo
 
nipo Secondary, wenzangu wanavaa masweta kipindi Cha mvua Mimi nikawa naenda na mkoti mtumbani mrefu hadi kweny viatu. Wakanibatiza jina Undertaker
 
Aisee mimi utotoni, nilipachikwa jina la "Doctor Kizinja"! Niliitwa jina hilo mpaka umri wa shule nilpoandikishwa std I ndipo taratibu likaanza kufifia lakini kuna kina mama wa kitongoji nilikozaliwa mpaka leo nikikutana nao huniita jina hilo!
KISA CHA KUPACHIKWA JINA HILO
Ilikuwa kati ya umri wa miaka 4 hadi 5, Aisee niliugua nafkiri ilikuwa malaria au sulua, basi mama yangu alinipeleka hospitali kupatiwa matibabu. Huko hospitali alikuwepo Dr. akiitwa Doctor Kizinja, nilikua muoga wa sindano so alipotaka kunidunga sindano nilisumbua kidogo, basi akanichimba mkwara akisema wanijua mimi, mimi ni Doctor Kizinja, nitakuchapa fimbo! Basi nikatulia mtalaam huyo ambaye kwa sasa mstaafu akanidunga sindano aina ya KRISTA PENI, sindano hii kwa miaka ya nyuma kabla ya kupunguzwa nguvu ilikuwa inauma ni ajabu na imeshasababisha vilema kwa watu wengi sana! Ndugu yangu unaambiwa nililia njia nzima na toka siku hiyo mtu alikuwa akitaja jina la DR Kizinja, natimua mbio ndefu bila kugeuka nyuma mpaka ndani!
 
Mkono wa jini....yani kila task ngumu au manz mgumu apatikane ...maana mkono wa jini unapita kila sehemu
 
Back
Top Bottom