Maswali.
1) Kweli (Truth) ni nini ama ni kitu gani?
2) Uhalisia (Reality) ni nini ama ni kitu gani?
3) Je, kuna reality nyingine tofauti na physical reality, kama ipo iko wapi na ikoje au inafanyeje kazi?
4) Je asili msingi basic nature ya vitu vyote ni ipi
5) Je, ubongo wa binadamu unaweza kutofautisha kati ya reality na illusion
6) Je, vitu tunavyoviona, kuvisikia, kuvihisi, kuvinusa katika physical world, je ndivyo vilivyo hata kwa asili yake au kwa viumbe wengine au ni namna ya ubongo wa binadamu kutafsiri reality ambayo huenda ikatofautiana na viumbe vingine?
7) Inawezekanaje usione kitu ambacho kipo mbele yako kabisa (e.g mchawi, msukule) au ukaona kitu ambacho kumbe hakipo hata kwenye mazingira yako(e.g mtu kumbe ni gogo) na huku umefumbua macho yote kodo?
8) Je tunaona kwa macho au ubongo?
9) Je mtu aliyekipofu tangu kuzaliwa anaitafsirije physical world katika akili yake, je ni sawa na anayeona au anatafsiri ya kwake mwenyewe kuhusu physical reality ambayo ni tofauti na tunaoona?
10) Kama physical reality hutafsiriwa tofauti baina ya mtu na mtu au mnyama yeyote au kiumbe kingine je yenyewe kama yenyewe bila kutafsiriwa na chochote ni kitu gani? (mfano unaposema mti [emoji268] je ni mti kweli au ni tafsiri ya ubongo wako na kama ni tafsiri ya ubongo wako je mti kama mti bila hiyo tafsiri ya kichwani mwako ni nini ama ni kitu gani?).
Naomba kwa sasa niishie hapa ingawa kuna maswali mengi lakini tuanze na haya kwanza kwa kuyapatia ufumbuzi kwa maelezo bayana ya kina kutoka kwa wajuvi wa mambo kwenye jukwaa letu
Karibuni kwa majibu bayana wanajamii, yenye ithibati pia.