Tupige kura, timu ipi ina washabiki wengi kati ya SIMBA na YANGA!

Tupige kura, timu ipi ina washabiki wengi kati ya SIMBA na YANGA!

Huwezi fananisha washabiki wa timu ya wananchi na vitu vya kijinga.
 
Nawashangaa wana Yanga mlioamua kujibishana na mbumbumbu wa Rage.
 
Poll counter IPO wapi ? Consult wabobezi wakuelekeze
 
Cc wabobezi.

We weka tu kura yako, hata physically itaonekana tu washabiki wa timu gn wengi.
Mkuu sikatai mwisho wa siku kura zitahesabiwaje ? Inabidi zoezi liwe LA uwazi unapiga kura unaona Na matokeo on the spot. Kama mleta maada ananirusu nianzieshe Uzi kama huo wenye poll
 
Ni ngumu kuamua wingi wa mashabiki wa simba na yanga kupitia ,kuangalia uchangiaji wa nyuzi zihusuzo timu hizo au kwa kupiga kura hapa
kwa sababu;

1.hata kama kura zikipigwa haziweki kufikia angalau 1000,
~hii ni kutokana na sababu ya mda, maana wapiga kura humu jukwaani hawawezi kupiga kwa mkupuo ni siku baada ya sku kadiri uzi unavyozidi kutrend

2.wachangiaji kwenye nyuzi zihusuzo simba na yanga, mfano ule uzi maalumu wa simba unaonekana kuwa na wachangiaji wengi kuliko ule wa yanga, lakin bado hiyo haitoshi kuamua wingi wa mashabiki,
kwa sababu;
~wachangiaji wanakuwa wana comment kwa kujirudia rudia walewale

~unakuta mchangiaji wa yanga ana comment uzi wa simba tena kwa kasi, & vice versa.

3.mtoa mada kuwa na wazo murua na zuri kabsa kama hili lakin watu wana mu ignore (mpuuza)
 
Hata mtoto wa darasa la pili anajua kirefu cha CCM.

Ukimdanganya kuwa Mapinduzi ninsawa na Wananchi atakucheka ...[emoji16][emoji16]
Ni kama kumwambia yanga ni mwananchi badala ya mahindi ya njano kutoka emerica.
 
Washabiki wa Yanga ni wengi sana, ila wengi hawaingii mpirani, na wanapenda dezo sana.
Mfano kuna mechi moja ilifanyika hapa Daresalam , Manji akainunua hivyo kuwaruhusu washabiki waingie bure uwanjani siku hiyo washabiki wa Yanga waliujaza uwanja.
Na nje ya uwanja kulikuwa na umati mkubwa wa wapenzi wa Yanga hadi Polisi ilibidi waingilie kati kuwalazimishwa wasiendelee kufulika nje na ndani ya uwanja.
Wanayanga walitoka Kongowe na maeneo mengine ya mbali hadi uwanja wa taifa kwa mguu kuja kuona mpira wa bure.

Tofauti na washabiki wa Simba, ki idadi ni wachache ukilinganisha na wa Yanga, ila wanaingia wengi uwanjani kwa kulipia tiketi.
Washabiki wa Simba wamesha ujaza uwanja mara nyingi tu, katika mechi zao na timu nyingine.
Katika sherehe za Simba Day, wanasimba huwa wanaujaza uwanja bila shida.
Yanga ni wengi sana ila wanashabikia mpira nje ya uwanja, kama kuangalia kwenye TV au ktk Vibanda Umiza.

Natanguliza Samahani kama nimewakwaza.
 
unadhani inavyoitwa timu ya wananchi wana maana gani, hao simba watasubiri sana
Kabisa, waache kufananisha timu ya wananchi na hicho kijitimu kilichorithiwa kutoka kwa wakoloni
 
Back
Top Bottom