Washabiki wa Yanga ni wengi sana, ila wengi hawaingii mpirani, na wanapenda dezo sana.
Mfano kuna mechi moja ilifanyika hapa Daresalam , Manji akainunua hivyo kuwaruhusu washabiki waingie bure uwanjani siku hiyo washabiki wa Yanga waliujaza uwanja.
Na nje ya uwanja kulikuwa na umati mkubwa wa wapenzi wa Yanga hadi Polisi ilibidi waingilie kati kuwalazimishwa wasiendelee kufulika nje na ndani ya uwanja.
Wanayanga walitoka Kongowe na maeneo mengine ya mbali hadi uwanja wa taifa kwa mguu kuja kuona mpira wa bure.
Tofauti na washabiki wa Simba, ki idadi ni wachache ukilinganisha na wa Yanga, ila wanaingia wengi uwanjani kwa kulipia tiketi.
Washabiki wa Simba wamesha ujaza uwanja mara nyingi tu, katika mechi zao na timu nyingine.
Katika sherehe za Simba Day, wanasimba huwa wanaujaza uwanja bila shida.
Yanga ni wengi sana ila wanashabikia mpira nje ya uwanja, kama kuangalia kwenye TV au ktk Vibanda Umiza.
Natanguliza Samahani kama nimewakwaza.