MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Nimeona kweye mitandao ya kijamii watu wanarushiana vijembe full, mipovu balaa. Jameni nchi hii itabaki kuwa Kenya. Ndani ya siku 60 tunarudi kwenye uchaguzi, cha msingi kila mmoja wetu ahifadhi kadi yake ya kura na tujitokeze kwa wingi siku ikifika.
Siku ya leo inafaa kuwa ya furaha kwetu sote kwamba imedhihirishwa uhuru wa mihili upo na sitegemei kama ipo siku itakuja tucharangane mapanga kwajili ya uchaguzi. Uhuru wa mahakama umeonekana na umesimama wazi na wima. Watakaoshindwa siku za usoni wamepata wapi pa kupeleka malalamiko yao maana watalindwa ilmradi wana hoja za msingi.
Binafasi pamoja na kwamba nilimuunga na nitazidi kumuunga rais Uhuru mkono na kumpigia kura, lakini ushindi wake ni bora uwe wa kukubalika ili sote tusonge mbele kwa pamoja bila majungu au machungu.
Ikitokea ashindwe kwenye marudio, sisi tunaomuunga mkono tuwe tayar kumpokea Raila Odinga kama rais wetu kwa miaka mitano ijayo, nao pia mlengo unaomuunga Odinga pia uwe tayari kukubali wakishindwa kihalali.
Uzalendo wangu kwa nchi yangu unazidi kuongezeka kila uchao kwa ajili ya hatua kama hizi.