Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Muungano uliotengeneza nchi ya Tanzania ni muungano unaochanganya sana, hauleweki na pia wenye changamoto nyingi sana kwa pande zote mbili. Muungano wetu unaweza kurekebishwa kwa kuiga mfumo wa muungano uliopo kati ya Denmark and Greenland, ambapo Greenland ni sehemu ya nchi ya Denmark ikiwa na serikali yake kamili lakini masuala ya ulinzi wa mipaka, mambo ya nje na rasilimali ndio yanaamuliwa Copenhagen.
Zanzibar iachwe na serikali yake kamili ijiamulie mambo yake yote kasoro Ulinzi wa mipaka na mambo ya nje tu ndio yabaki kuwa mambo ya muungano, katiba ya Tanzania irekebishwe kuondoa kifungu cha kutaka Rais au Makamu wa Rais kutoka Zanzibar, wabunge wa Zanzibar wabaki Zanzibar tu badala yake watume wawakilishi wachache kama itakavyoafikiwa kwenye kamati ya bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama.