Tusali watanzania Mungu atuepushe kuwa Zimbabwe

Tusali watanzania Mungu atuepushe kuwa Zimbabwe

TumainiEl

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
7,280
Reaction score
14,342
Ndugu Watanzania wenzangu, Najua Serikali yoyote inawekwa na Mungu na hata Serikali tulio nayo naamini iliwekwa na Mungu. Ila from no where kumetokea sijui na washauri wabaya ama mwenye taifa basi mambo sio mambo.

Mbaya kuliko yote nikuwepo kwa kajikundi samahani lakini mimi nakaita kajikikundi kakiongozwa na kijana mwenzetu wao wamesema wanampenda Rais wetu kuliko awaye yeyote na hapo ndipo balaa limeibuka.

Jamani kama mnavyo juwa Rais ni taasisi na ikiwa ndani ya taasisi kuna watu wananguvu kuliko waliopo kwenye taasisi basi ndipomaajabu hutokea.

Labda niwakumbushe ya Zimbabwe hayatofautian sana na haka kanatokea hapa kwetu. Watu wachache walio ona fursa kwenye utawala wa Mugabe walianza kumpamba na kuwachoma wale ambao walikuwa ktk kumuongoza Mkuu ndipo kakazuka kakikundi kakaenda kuwakusanya watu nakuwatibua Wazungu. Wakimuahidi kumlinda milele yeye ndio baba wa taifa ila Wazungu walicholifanyia taifa lile mpaka sasa Zimbabwe nimaututi kihchumi.

Ndugu zangu Watanzania tusali tusali naomba kila dini na kabila tusali maana kamba inataka kukatika Rais wetu amezungukwa nahako kakikundi hatari kwa usalama wa taifa na chama pia ila mbaya zaid Rais amsikilize nani amuache nani na yeye ndie last say.

Ndugu zangu kunamahali neno linasema pasipo maono taifa uwangamia taifa letu likiangamia tutakao umia nisisi.

Uchumi wetu ndio pigo kubwa ikiwa tunao waita mabeberu watatuminya. Nikweli hawa majama nimabeberu ila nivyema tujikite kuwashughulikia kwa akili kuliko mabavu.

Mwalim Nyerere alitaman angetawala zaid yapale ila alisoma alama za nyakati akajuwa atapotea kwenye picha akampa mwinyi nchi nakweli mwinyi akatekeleza matakwa yao taifa likapona je leo tutaweza kurud kule kulimshinda Bba wataifa?

Bila shaka intelligence yetu haiku usoma mchezo nakama iliusoma na mkuu akapiga chini. Mimi nasali nawaombea vijanamaelfu wasio na ajira na maelfu watapukutishwa just kwa kuharibika uchumi.

Watanzania tusilale tumuombe Mungu tumuombe Mungu.

Mungu ulikumbuke taifa la tanzania na Rais wetu apate maono kuwa kuna watu wanampoteza kwakumsifia nakumtaja jina lake kila kikao ila nyuma taifa linahujumiwa.

Amen

Update..

Siku chache baada ya hii thread naona Mungu anaanza jibu maombi na sala za Watanzania. Ila ngoma bado mbichi... Fukuto limezidi kuwa fukuto wanasema mtu aliekukatili kukutoa uhai wako nivigumu kumuamini tena nakatika hili hali imezidi kuwa tetete... Tuzidi kusali
 
Usemayo ni kweli japo kuna mengi nyuma ya pazia tusiyoyajua sisi watu baki. Wabunge wengi wanajua kinachoendelea. Kutolewa kwa CAG ni kulinda ripoti ijayo.
Redundancy iko karibuni
 
Mkuu, hivi maombi tu ndiyo yanayoweza kubadilisha mtazamo wa taasisi ya Urais, ama ni watu wa kitengo ndio wenye wajibu wa kuwajibika ipasavyo na waishi ktk maadili na weledi wao wa kazi.

Nchi yoyote ile duniani toka zama zile za mfalme Daudi wameweza, taasisi ya Urais ama kifalme imeweza kufanikiwa kupitia weledi wa kijasusi ktk mambo ya ndani na nje. Nao wote waliweza kuwaunganisha wananchi wao kupitia ktk tunu za taifa, wala sio itikadi za kisiasa.

Tupo ktk mkwamo, kwani tumeruhusu itikadi za vyama ziangaliwe kwa jicho la chuki na uadui. Badala ya kuweka utaifa wetu mbele kwa makusudi tumeamua kuangaliana kwa jicho la kikada, yaani wale makada watiifu kwa mfalme ndio wanaaminika na hata kushika nafasi nyeti, nao huziendesha kwa upendeleo wa kikada.

Ubaguzi wa dhahiri haupo tu dhidi ya vyama vya upinzani na wanaharakati, bali pia upo ndani ya makada wa chama tawala, hasa lile kundi linaloonyesha kupingana na fikra za Mwenyekiti. Ubaguzi pia unawahusu makundi yote yaliyobakia kupitia kigezo hicho hicho.

Sasa haijalishi mchango, hoja wala maoni ya kitaalamu, vyote huitimishwa kwa jicho na mtazamo wa kiitikadi. Ukionyesha kasoro yoyote ile hata kwa msukumo wa kizalendo, ni lazima upate shutuma za kutoitakia mema serikali yetu.
 
Serikali haiwekwi na kiumbe gani sijui hicho, inawekwa na wapiga kura au inachukuliwa kwa nguvu, huyo mungu mnayesema ni mwema kuliko wote alafu amuweke mtu kama mugabe ambaye kaangusha nchi kasababisha mamilioni ya watu kufa njaa, kamuweka mtu ka Idd Amin alafu mnakaa kusema ni mungu mwema? Hehehe sijui watu mna matatizo gani, huyo mungu anayeweka watu hao ana matatizo ya akili.

rais wenu anaombewa kila siku maombi yamegoma, sasa endeleeni kumtegemea huyo aliye angani amekaa anawacheka tu mlivyo vilaza mnaomba daily hehe
 
Mkuu, hivi maombi tu ndiyo yanayoweza kubadilisha mtazamo wa taasisi ya Urais, ama ni watu wa kitengo ndio wenye wajibu wa kuwajibika ipasavyo na waishi ktk maadili na weledi wao wa kazi.

Nchi yoyote ile duniani toka zama zile za mfalme Daudi wameweza, taasisi ya Urais ama kifalme imeweza kufanikiwa kupitia weledi wa kijasusi ktk mambo ya ndani na nje. Nao wote waliweza kuwaunganisha wananchi wao kupitia ktk tunu za taifa, wala sio itikadi za kisiasa.

Tupo ktk mkwamo, kwani tumeruhusu itikadi za vyama ziangaliwe kwa jicho la chuki na uadui. Badala ya kuweka utaifa wetu mbele kwa makusudi tumeamua kuangaliana kwa jicho la kikada, yaani wale makada watiifu kwa mfalme ndio wanaaminika na hata kushika nafasi nyeti, nao huziendesha kwa upendeleo wa kikada.

Ubaguzi wa dhahiri haupo tu dhidi ya vyama vya upinzani na wanaharakati, bali pia upo ndani ya makada wa chama tawala, hasa lile kundi linaloonyesha kupingana na fikra za Mwenyekiti. Ubaguzi pia unawahusu makundi yote yaliyobakia kupitia kigezo hicho hicho.

Sasa haijalishi mchango, hoja wala maoni ya kitaalamu, vyote huitimishwa kwa jicho na mtazamo wa kiitikadi. Ukionyesha kasoro yoyote ile hata kwa msukumo wa kizalendo, ni lazima upate shutuma za kutoitakia mema serikali yetu.
Nikweli ila kalekakikundi
 
Huyu atakuwa kapigwa chini kwenye hako ka-kikundi kao analia njaa sikuhizi akili zimamrudi.
True mtu yeyeto aliyetumbuliwa au mirija yake kukatwa utamjua tu kwenye thread.Huyu bwana hakika anasomeshwa au kafukuzwa kwa shemeji aliyekuwa mnufaika baada ya mirija kukatwa na awapae riziki
 
Back
Top Bottom