Mkuu, hivi maombi tu ndiyo yanayoweza kubadilisha mtazamo wa taasisi ya Urais, ama ni watu wa kitengo ndio wenye wajibu wa kuwajibika ipasavyo na waishi ktk maadili na weledi wao wa kazi.
Nchi yoyote ile duniani toka zama zile za mfalme Daudi wameweza, taasisi ya Urais ama kifalme imeweza kufanikiwa kupitia weledi wa kijasusi ktk mambo ya ndani na nje. Nao wote waliweza kuwaunganisha wananchi wao kupitia ktk tunu za taifa, wala sio itikadi za kisiasa.
Tupo ktk mkwamo, kwani tumeruhusu itikadi za vyama ziangaliwe kwa jicho la chuki na uadui. Badala ya kuweka utaifa wetu mbele kwa makusudi tumeamua kuangaliana kwa jicho la kikada, yaani wale makada watiifu kwa mfalme ndio wanaaminika na hata kushika nafasi nyeti, nao huziendesha kwa upendeleo wa kikada.
Ubaguzi wa dhahiri haupo tu dhidi ya vyama vya upinzani na wanaharakati, bali pia upo ndani ya makada wa chama tawala, hasa lile kundi linaloonyesha kupingana na fikra za Mwenyekiti. Ubaguzi pia unawahusu makundi yote yaliyobakia kupitia kigezo hicho hicho.
Sasa haijalishi mchango, hoja wala maoni ya kitaalamu, vyote huitimishwa kwa jicho na mtazamo wa kiitikadi. Ukionyesha kasoro yoyote ile hata kwa msukumo wa kizalendo, ni lazima upate shutuma za kutoitakia mema serikali yetu.