Tusamehe sana Sheikh; tulipuuza maneno matakatifu ya Quran

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Haikuwa ni bure kuwapatia uongozi wanaume juu ya wanawake ndani ya Uislamu. Huu ni uongozi wa kimaumbile ambao unakubalika ndani ya makabila na mataifa mengi duniani; kwamba mwanamme ndio mkuu wa shughuli za mwanamke.

Allaah Anasema ndani ya Qur-aan Tukufu (tafsiri):
الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ

Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. [An-Nisaa: 34]

Waislamu tofauti wamekuwa wakifanya harakati za kurudisha utamaduni wa Kiislamu. Hata hivyo, kibarua hichi kimeonekana kuwa ni kigumu mno. Tatizo kubwa linalotukabili ni wanaume wenyewe kukosa muelekeo pamoja na kuacha muongozo sahihi wa Uislamu.

Wanawake wamekosa hayaa hadi kutembea utupu. Heshima baina ya mume na mke zimeporomoka, halikadhalika baina ya baba na binti. Haya yote yanasababishwa na mwanamme mwenyewe. Yareti kama mwanamme atakuwa na msimamo mbele ya mwanamke, hatayumbishwa.

Ni nani anayemvizia mwanamke hadi kumuingiza ndani ya mtego wa panya? Nani anayemfadhili na kumtembeza mwanamke mithili ya kinyago? Bila ya shaka yoyote, majibu ya masuala haya ni mwanamme!

Kwani mwanamke anapovaa Hijaab, ni mwanamme ndiye aendae kumwambia yu mshamba. Anapovaa jeans na mini skirt, mwanamme atampigia kofi za kila namna. Sasa mwanamke anapotembea bila ya kufuata misingi ya Kiislamu nani tumlaumu? Wa kwanza ni mwanamme.

Hivyo sivyo kwa upande wa Uislamu, kwani mwanamme ndio anatakiwa kuwa kinara wa tabia nzuri. Hapo inakuwa ni rahisi kufuatwa tabia hizi njema kwa mwanamke: “Muumini aliyekamilika kwa imani ni yule mwenye tabia njema, na mbora wenu ni yule aliye mbora kwa wake zake kwa tabia.” [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy].
 
FB_IMG_1757160741569.jpg
 
Upuuzi kuishi na kuendelea kuamini tamaduni zilizopitwa na wakati,
Nyie ndio mnaoenda beach na majuba kila jambo lifanyike kwa weledi na uelewe sio kualzimisha mazingira ya sasa yafanane na mazingira ya wajinga na washamba wa kalr ambao hata hawakujua kusoma na kuandika.

Ukikaa ukatafakari huo usilam ni mfumo wa kitamaduni na kisiasa uliofalishwa vazi la dini ambao ulitokea katika mazingira magumu ya jangwani ndio mana wanawake walivaa hijabu na wanaume kuvaa bharagashia ili kulinda nywele zao zidi ya upepo mkali wa mchanga wa jagwa.

So tumia akili acha kwenda kama nyumbu.
 
hahah hao (wahuni) ndo aliosema shehe lzm wawe juu yake ...
Dah,
Ni bora kuongozwa na mtu anayejulikana na kuwajibika wazi kuliko huu mfumo wa mtawala anayeburuza nchi nzima kinyemela kwa remote kutokea nyumbani kwake.

Kwa hili nasimama na Polepole..

#KataaWahuni
 
Nmekuelewa vyma na si dini tu hta mila na desturi hazikuwahi kumtambua ke kam mtu mwnye utashi wa kuwa kichwa..ke ameumbwa kuongozwa na me na nisis wenyewe me tumeyapandkiza haya et fifte fifte! Matokeo ndo haya sasa..mfano tunao wnyewe!
 
Haikuwa ni bure kuwapatia uongozi wanaume juu ya wanawake ndani ya Uislamu. Huu ni uongozi wa kimaumbile ambao unakubalika ndani ya makabila na mataifa mengi duniani; kwamba mwanamme ndio mkuu wa shughuli za mwanamke.

Allaah Anasema ndani ya Qur-aan Tukufu (tafsiri):
الرِّجَالُ قَوَّامُونَ عَلَى النِّسَاءِ بِمَا فَضَّلَ اللَّـهُ بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ وَبِمَا أَنفَقُوا مِنْ أَمْوَالِهِمْ ۚ

Wanaume ni wasimamizi juu ya wanawake kwa kuwa Allaah Amefadhilisha baadhi yao kuliko wengine na pia kwa ambayo wanatoa katika mali zao. [An-Nisaa: 34]

View attachment 3467502

Waislamu tofauti wamekuwa wakifanya harakati za kurudisha utamaduni wa Kiislamu. Hata hivyo, kibarua hichi kimeonekana kuwa ni kigumu mno. Tatizo kubwa linalotukabili ni wanaume wenyewe kukosa muelekeo pamoja na kuacha muongozo sahihi wa Uislamu.

Wanawake wamekosa hayaa hadi kutembea utupu. Heshima baina ya mume na mke zimeporomoka, halikadhalika baina ya baba na binti. Haya yote yanasababishwa na mwanamme mwenyewe. Yareti kama mwanamme atakuwa na msimamo mbele ya mwanamke, hatayumbishwa.

Ni nani anayemvizia mwanamke hadi kumuingiza ndani ya mtego wa panya? Nani anayemfadhili na kumtembeza mwanamke mithili ya kinyago? Bila ya shaka yoyote, majibu ya masuala haya ni mwanamme!

Kwani mwanamke anapovaa Hijaab, ni mwanamme ndiye aendae kumwambia yu mshamba. Anapovaa jeans na mini skirt, mwanamme atampigia kofi za kila namna. Sasa mwanamke anapotembea bila ya kufuata misingi ya Kiislamu nani tumlaumu? Wa kwanza ni mwanamme.

Hivyo sivyo kwa upande wa Uislamu, kwani mwanamme ndio anatakiwa kuwa kinara wa tabia nzuri. Hapo inakuwa ni rahisi kufuatwa tabia hizi njema kwa mwanamke: “Muumini aliyekamilika kwa imani ni yule mwenye tabia njema, na mbora wenu ni yule aliye mbora kwa wake zake kwa tabia.” [Abu Daawuud na At-Tirmidhiy].
 
Dah,
Ni bora kuongozwa na mtu anayejulikana na kuwajibika wazi kuliko huu mfumo wa mtawala anayeburuza nchi nzima kinyemela kwa remote kutokea nyumbani kwake.

Kwa hili nasimama na Polepole..

#KataaWahuni

word ...
 
USA na China hayo ni mataifa makubwa sana yaliyoendelea kuliko taifa lolote kwa sasa.

Hayajawahi kuwa na kiongozi mwanamke katika level za urais.

Marekani juu ya demokrasia yao yote lakini hawajawahi kuwa na rais mwanamke.

Sio kwa bahati mbaya wanajua madhara yake.
 
Back
Top Bottom